Stream line
JF-Expert Member
- Apr 22, 2015
- 393
- 243
Sote tuna jua wakati wa awamu ya 3 vigogo walikuwa wako bize kujigawia mashirika yetu ya umma. Mbali na kuletewa Ma-boa toka kusini mwa Afrika ili kuisimamia Tanesco. Kuna sakata kubwa la waziri karamage kujitwalia bandari. kulikopelekea kuzaliwa kwa TICTS. Leo Mh. rais MAgufuli ameagiza mkataba upitiwe upya. tukumbuke TICts imepigiwa kelele jamvini humu toka inaanza akina TAIKUBWA,BAK nk nk wameongea mengi mno juu ya ticts. Tunawaomba wafanyakazi wa bandari kuungana na kutuonyesha umoja wenu dhidi ya ticts kama walivyofanya Tanesco na TRL hadi ma-boa na wagoa wakaondoka.