Mkataba wa ovyo wa Bandari, una neema yake

Mkataba wa ovyo wa Bandari, una neema yake

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,949
Waumini tunafundishwa kumshukuru Mungu kwa kila jambo, hata kama kwa utashi wetu tunaliona ni baya, maana kuna wakati ubaya wa kitu huweza kukuletea neema. Ujambazi ni mbaya, lakini umesababisha watu wengi kujenga nyumba imara, ambazo baadhi kama kusingekuwa na hofu ya ujambazi zingejengwa katika hali dhaifu sana, kiasi kwamba hata kingekuja kimbunga kingeweza kuzivunja na kuangamiza familia nzima.

Mkataba wa hovyo wa bandari, umeonesha na kutufumbua macho juu ya nini tunatakiwa kufanya ili nchi yetu iweze kuwa mahali salama na panapompa matumaini kila raia:

1) Mkataba wa hovyo wa bandari, umetukumbusha haja ya kufuta kinga ya viongozi wakuu kutoshtakiwa wanapofanya makosa ya makusudi wanapokuwepo madarakani. Viongozi wakuu wa umma wasingekuwa na kinga ya kutoshtakiwa, kabla ya kufanya jambo lolote wangekuwa wanajipa muda wa kutafakari kama jambo wanalolifanya ni halali au ni kinyume cha katiba na sheria.

2) Mkataba wa hovyo wa bandari umetukumbusha uhovyo wa jeshi la Polisi na umuhimu wa kulifanyia mabandiliko makubwa. Tunakumbuka wakati George Simbachawene akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, baadhi ya wananchi walilalamikia juu ya sifa za polisi kuweza kuajiriwa. Watu walioonekana wana ufaulu wa juu kwenye masomo, hata kama wakiomba kuajiriwa kuwa polisi walikuwa wananyimwa, huku wakichukuliwa wale waliofeli masomo. Na waliofaulu vizuri masomo yao wakiambiwa wamekosa sifa. Waziri Simbachawene katika kulitolea ufafanuzi jambo hilo allisema kuwa hawawezi kuwachukua watu wenye ufaulu mzuri wa masomo kwa sababu hawatakubali kuwa walinzi. Hiyo ilimaanisha kuwa mtu akionekana ana akili kubwa na amefaulu vizuri masomo yake hawezi kuajiriwa kuwa polisi kwa sababu kazi hiyo ni ya watu wenye akili ndogo. Na hiyo ilikuwa akiashiria kuwa kazi kubwa ya polisi ni kuwa korokoroni. Lakini ukweli ni kwamba kazi za polisi ni zaidi ya kuwa korokoroni, na baadhi zinahitaji akili kubwa. Madhara ya kulifanya jeshi la polisi kuwa ni mahali pa watu wenye akili ndogo, madhara yake tunayaona. Mtu mwenye akili ndogo, pamoja na mapungufu mengine, huwa hajiamini. Na kwa sababu hajiamini hufanya kazi kama tarishi, siyo kwa kuangalia sheria. Watu wenye akili ndogo au ujuzi mdogo mahali popote huwa ni hatari, huwa wanatafuta namna ya kuziba pengo lao la uwezo mdogo wa akili. Na hawa, mahali popote pale pa kazi, hufanya kazi kwa kujipendekeza. Hawa ndiyo huwa wapo tayari kufanya uovu wa aina yoyote ili kumfurahisha bwana wake.

3) Miaka mingi, wakati wa mfumo wa chama kimoja, kulikuwa na vuguvugu kubwa la kutaka kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika, hadi Bunge la chama kimoja likafikia kwenye azimio la kauli moja kuwa Serikali ya Tanganyika ianzishwe. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, kwa kutumia tu ubabe, alilifuta azimio la Bunge. Mkataba wa hovyo wa bandari, umetukumbusha kiporo hiki. Sasa ni wakati wa kuhakikisha Serikali ya Tanganyika inaanzishwa haraka, na mipaka ya kila Serikali kwenye Muungano inawekwa wazi ili kuepuka migongano.

Uhovyo huu wa mkataba wa bandari uamshe ari ya kuhakikisha Taifa letu linakuwa na katiba mpya iliyo nzuri na inayorudisha mamlaka yaliyoporwa na watawala, kwa wananchi. Mkataba wa hovyo wa bandari ni mvua iliyotuonesha ubovu wa paa na msingi wa nyumba yetu. Lazima sasa tutengeneze nyumba imara na iliyo bora ili tusiangamie.
 
4.mkataba mbovu wa bandari umetuonyesha chuki za watu na udini katika nyoo za baadhi ya watu nchini, wengine kua tayari kupindua serikali halali ya raia wanatamani tuende kwenye kumwaga damu kwa masilahi yao binafsi.
Ulichokiongeza hakina tofauti na mazungumzo ya mlevi wa komoni iliyochanganywa na wanzuki.
 
Hata walioko Mirembe wametambua CCM haifai tena kuendelea kubaki madarakani.

Si hivyo tu, hata watoto wadogo mashuleni wametambua CCM wanahatarisha future yao na kwamba haifai kabisa.
 
4.mkataba mbovu wa bandari umetuonyesha chuki za watu na udini katika nyoo za baadhi ya watu nchini, wengine kua tayari kupindua serikali halali ya raia wanatamani tuende kwenye kumwaga damu kwa masilahi yao binafsi.
Chuki za udini zipo tu kwa wote Wakristu na Waislam. Wamezificha tu vifuani mwao. Wakati wa Magufuli tuliona hadi list ya Madokta na Maprof Waislam ilitolewa kudhihirisha Waislam wamesoma hivyo wanastahili teuzi. Na sasa tunaona hivyo hivyo Wakristu wakilalamika. Hii hali haitaisha labda kama nchi itagawanywa kama India na Pakistan.

Vinginevyo tujifunze kuishi kwa kuvumiliana. Kusema eti watu wamedhihirisha chuki za dini kwa sasa ni unafiki wa hali ya juu kwani hata huko nyuma hali ilikuwa hiyo hiyo.

Pia tujiandae kabla mama hajatoka madarakani lazima kutatokea vurugu za kidini kama zile za Mbagala kwa Wakristu kushambuliwa na Waislam. Kwa Mzee Mwinyi ilitokea pale Waislam walipovamia bucha za Ngurue Kigogo na kuleta tafrani kubwa. Sijui kwa SSH itatokea wapi lakini itatokea.
 
Hahahaaa!
JamiiForums608282686.jpg
 
4.mkataba mbovu wa bandari umetuonyesha chuki za watu na udini katika nyoo za baadhi ya watu nchini, wengine kua tayari kupindua serikali halali ya raia wanatamani tuende kwenye kumwaga damu kwa masilahi yao binafsi.
Serikali halali kwa uchaguzi ule wa kihayawani wa 2020?
 
Waumini tunafundishwa kumshukuru Mungu kwa kila jambo, hata kama kwa utashi wetu tunaliona ni baya, maana kuna wakati ubaya wa kitu huweza kukuletea neema. Ujambazi ni mbaya...

Hongera umeandika vema
 
Mimi pamoja na uzee wangu wa miaka 93 nimeshuhudia mikataba mingi mibaya lakini huu wa bandari ni wahovyo kuliko mikataba yote mibovu kuwahi kutokea Tanzania
Sio kweli Mkataba mbovu kuliko Mikataba yote Tanzania ni Mkataba wa Muungano kauli ya Makoma wa kwanza wa Raisi wa Zanzibar mhe Othman Masoud Othman
 
Huu nkataba ukituwezesha kuingiza vitu bila bughdha TRA na kodi za kksengee.....poa tu manake hata faida ya hiyo bandari hainiletei misosi mezani kwangu kkmmamae🤪😜🤪😜
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom