• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Mkataba wa kuuza Kongo huu

kibavu

kibavu

Senior Member
Joined
Oct 15, 2008
Messages
136
Points
195
kibavu

kibavu

Senior Member
Joined Oct 15, 2008
136 195
Nikiangalia yanayotokea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati huu, nashawishika kuamini kwamba yaliyoandikwa kwenye Makal hii ( Mwanahalisi, February 9, 2009) yana ukweli mkubwa tu! Tuilinde Tanzania yetu, I hope viongozi wetu hawaingii mikataba kama huu wa Laurent Desire Kabisa.Mkataba wa kuuza Kongo huuNa Mwandishi Maalum - Imechapwa 11 February 2009KINACHOITWA vita vya sasa nchini Kongo ni utekelezaji wa
"Makubaliano ya Lemera" ya mwaka 1996 yenye shabaha ya kuigawa nchi hiyo kubwa kuliko yoyote ile Afrika Mashariki na Kati.

Makubaliano yalifanywa kati ya Laurent Desire Kabila, akiwa kiongozi wa chama cha "kuikomboa Kongo" kutoka utawala wa dikteta Mobutu Sese Seko, kwa upande mmoja; na wapiganaji wa Kinyarwanda kutoka Rwanda na Mashariki mwa Kongo.

Makubaliano ambayo yalifanyika kwenye vilima vya Lemera vilivyoko Kivu ya Kusini na kujulikana kwa jina hilo, yalitaka Kabila, baada ya kuwa rais wa Kongo, aruhusu mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kuwa makazi ya Wanyarwanda wa kabila la Kitutsi.

Taarifa zilizopo zinaonyesha makubaliano yaliandaliwa mapema mjini Kigali na pale Lemera yalikuwa yanazinduliwa tu. Ilikubaliwa wakati huo kwamba
hiyo ndiyo ingekuwa "asante" kwa Rwanda "kwa ukombozi wa Kongo."

Desire Kabila alikuwa tayari amechoka. Kwa takriban miaka 20 alikuwa akipambana na utawala wa Mobutu Sese Seko. Alikuwa amefikia hatua ya kukata tamaa na kutulia jijini Dar es Salaam.

Mwaka 1996, mjini Kigali, Rwanda kilikuwa kimeundwa kikundi cha wapiganaji waliojiita "wapinzani wa dikiteta Mobutu." Hawa walikuwa Wakongomani na Wanyarwanda kutoka Rwanda na wengine waliokuwa wakiishi mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa Kongo.

Katika kundi hilo alikuwemo Mkongomani, Jenerali Andre Kisasi Ngando; askari mtaalam wa kusomea. Anadaiwa kupata mafunzo nchini Cuba, Ujerumani na Bulgaria. Alikuwa akiongoza Wakongomani wapatao 600 katika kikundi hicho.

Wakati kikundi hicho kinataka kuanza vita, kilitaka kuwa na msemaji. Mungu akupe nini! Hakuna uthibitisho wowote, lakini taarifa zinaeleza kiliomba ushauri wa Mwalimu Julius Nyerere "ambaye aliwapa Laurent Desire Kabila kuwa msemaji wa wapiganaji."

Mwanzoni mwa vita ya kumg'oa Mobutu kikundi hiki kilijulikana kama cha Wanyamulenge. Dunia nzima ikaambiwa na kuaminishwa kuwa hayo yalikuwa "maasi ya Wanyamulenge."

Wanyamulenge ni watu wanaodaiwa kutoka kwenye vilima vya Mulenge vilivyoko wilaya ya Uvira katika mkoa wa Kivu Kusini. Makabila ya asili ya hapa ni Wavira na Wafuliro.
Wanaojiita Wanyamulenge ni Wanyarwanda wakuja.

Vita vilianza kwa propaganda kuu kwamba serikali ya Mobutu haitambui Wanyamulenge ambao walidai ni raia wa Kongo; inawanyanyasa na inawanyima uraia. Haya yalikuwa madai makubwa sana yaliyovuta hisia kali na huruma kwa wapiganaji.

Wapinzani, chini ya
Jenerali Andre Kisasi Ngando, na msemaji mkuu wao Laurent Kabila waliteka, kama mchezo, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Goma. Wakavuka Ziwa Kivu na kuingia Kivu Kusini.

Ilikuwa baada ya kukamata mji wa Bukavu, makao makuu ya Kivu Kusini na sehemu nyingi za mkoa huo,
wapiganaji wa Kinyarwanda waliingiza pendekezo la rais ajaye wa Kongo, kutoa Kivu Kaskazini na Kusini kwa Rwanda.

Lakini kabla suala hilo nyeti kupewa uzito unaostahili, wapiganaji wa Kinyarwanda, baada ya kuteka Bukavu, wanadaiwa kuanza kupora mali – magari, vifaa vya nyumbani, dawa katika maduka – hatua ambayo ilielezwa kuwa uhamishaji wa mali za wakazi wa Bukavu na maeneo mengine.

Alikuwa Jenerali Ngando anayeripotiwa kupinga uporaji usiomithilika, jambo ambalo lilimletea uhasama kwa baadhi ya wapiganaji. Kuona hivyo, Laurent Kabila akamwasi Ngando.

Ngando anasemekana kuuawa siku chache baada ya kutofautiana na wapiganaji juu ya uporaji. Inaelezwa kuwa alimiminiwa risasi na kuuawa na mwili wake kuchomwa moto katika mbuga ya wanyama ya Virunga.

Kabila aliulizwa mara nyingi juu ya Ngando. Alikuwa na majibu tofauti. Akiwa bado msituni alisema Jenerali Ngando amekamatwa na majeshi ya serikali na mara ametekwa na wanamgambo wa Mai Mai.

Baadaye Kabila alisema Ngando alijeruhiwa na kupelekwa Ujerumani kwa matibabu. Na wakati akiwa rais, aliwaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa kuwa Ngando alikuwa askari kama askari wengine na kwamba alikufa kwenye mapambano.

Ilikuwa baada ya kifo cha Jenerali Ngando ndipo Kabila aliingizwa kwenye makubaliano ya kumega Kongo. Kwanza, kikundi cha wapiganaji kiligeuzwa kuwa chama – AFDL – Alliance de front Democratique pour la Liberation du Congo.

Kabila akapanda cheo na kuwa kiongozi wa chama cha ukombozi wa Kongo kutoka kuwa msemaji tu wa wapiganaji.

Baada ya kuundwa kwa AFDL, jina la Wanyamulenge likatoweka kabisa. Wapiganaji wakaitwa waasi wa Kongo. Taarifa zinasema kabla wapiganaji kutoka Bukavu na kuanza safari iliyomfikisha Kabila madarakani, waliingia katika mkataba ambao ndio umekuja kuitwa
"Makubaliano ya Lemera."

Kuna madai kwamba viongozi wakuu wa wakati huo wa baadhi ya nchi walipata nakala ya makubaliano hayo ya kumega Kongo. Miongoni mwa nchi hizo ni Namibia, Uganda, Burundi, Zambia, Ethiopia, Eritrea, Zimbabwe, Angola, Namibia, Sudan na baadhi ya nchi za Ulaya na Marekani.

Imeelezwa kuwa makubaliano ni pamoja na kufanya mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini kutawaliwa na Wanyarwanda wa Kitutsi kutoka mataifa ya Rwanda, Burundi na Uganda; na kwamba utawala huo ambao ungefanya kazi kwa ushirikiano na serikali ya Kabila, ungetekelezwa kwa awamu tatu katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 1998.

Chini ya mpango huo, raia wa Kongo, wakazi wa Kivu Kaskazini wangehamishiwa Kivu Kusini, "taratibu na kwa utulivu huku makazi yao yakichukuliwa" na wavamizi.
Imeelezwa kuwa hatua ya kwanza isingekuwa ngumu kwani Rwanda ingedai kuwa inapambana na wanamgambo wa Kihutu walioitwa Interhamwe ambao itaelezwa kuwa wanatishia amani nchini Rwanda. Hivyo ndivyo imekuwa ikifanya hadi sasa.

Makubaliano yanadaiwa kueleza kuwa kuchukuliwa kwa miji ya Goma na Butembo mkoani Kivu Kaskazini, sharti iwe hatua ya kwanza kwa kuwa hayo ndiyo maeneo yenye upinzani mkubwa. Kufanikiwa kwa awamu ya pili, kungetegemea mafanikio ya awamu ya kwanza, makubaliano yanadaiwa kueleza.

Wafuatiliaji wa mahusiano ya Rwanda na Kongo wanasema ingawa mpango huo ulishindikana kutekelezwa kuanzia mwaka 1998, kuingia kwa majeshi ya Rwanda nchini humo hivi sasa, ni utekelezaji wa hatua ya kwanza ya Makubaliano ya Lemera; na tayari miji ya Goma na Butembo iko chini ya kile kinachoitwa "majeshi ya ushirikiano" ya Rwanda na Kongo.

Kwa mujibu wa masimulizi juu ya makubaliano hayo, awamu ya pili ingekuwa kujaza wakazi wa Kaskazini katika Kivu Kusini na kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo wazawa wangeenguliwa, kukosa uongozi na hivyo kunyimwa sauti.

Hatua nyingine ilikuwa kuanzisha benki ya kusaidia wavamizi katika Kivu mbili, kujenga nyumba zipatazo 600,000 na kujiimarisha katika nchi ya kigeni – Kongo.

Imeelezwa kuwa Kabila alikubaliana na masharti ya makubaliano kwa kuwa lengo lake lilikuwa moja tu: Kuingia ikulu ya Kinshasa kwa msaada wowote kutoka kwa yeyote; Mungu au shetani.

Ilikuwa baada ya makubaliano hayo,
Kabila alisonga mbele na hatimaye kushinda na kuingia ikulu ya Kinshasa akiwa na wapiganaji wa Rwanda, akiwemo mkuu wa sasa wa majeshi wa Rwanda, James Kabarebe.

Baada ya kuingia ikulu, Kabila anadaiwa kuwageuka wenzake. Ilikuwa baada ya miaka miwili ya urais, alitangaza, tena kwa jeuri, kuwa wageni wote waondoke nchini. Aliongeza kwa kufafanua, kwamba Wanyarwanda warudi kwao na kusema anawashukuru kwa kazi waliyofanya.

Kabila alikuwa tayari amesoma mwelekeo wa makubaliano yake na kuona kuwa yanatoa mwanya kwa kile kilichoitwa "Nchi ya Ahadi" ya Watutsi kutoka Rwanda, Burundi, Uganda, Somalia, Ethiopia, Eritrea na Tanzania.

Alitakiwa atangaze, akiwa rais, kuwa Kivu mbili zote ni makazi ya Watutsi; ili hata wananchi wa Kongo watakaobaki humo, wawe wanafahamu kwamba siyo kwao.

Kabila alinukuliwa akisema kuwa hayo (Makubaliano ya Lemera) ni "makubaliano ya porini" na kwamba yeye hakuwa na madaraka ya kuuza nchi. Alisema hakatai kuwepo mkataba, lakini akataka hilo "lipelekwe kwa wananchi – kupitia bungeni – ili wananchi wenyewe waamue."

Kilichomshangaza zaidi Kabila, baada ya kutangaza kuwa Wanyarwanda warudi kwao, ni kwamba aliyekuwa wa kwanza kuondoka na kukimbilia Afrika Kusini, alikuwa waziri wake wa mambo ya nje aliyeitwa
Bizima Karaha (Bizimana Karahamuheto).
Katika mshangao na labda kejeli, Kabila alisema,
"Kumbe nchi ilikuwa imevamiwa! Hata waziri wangu wa mambo ya nje alikuwa Mnyarwanda?"

Hiyo ilifuatiwa na kufukuzwa kwa
James Kabarebe aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Kongo na sasa mkuu wa majeshi ya Rwanda. Hatua hizi na nyingine, ndizo zilisababisha kutotekelezwa kwa Makubaliano ya Lemera.

Lakini wachunguzi na wafuatiliaji wa mahusiano ya nchi hizi mbili wanasema, makubaliano yameandikwa na yapo; hayajafutika. Kilichofanyika ni "ukaidi wa Kabila" wa kutotaka kutimiza ahadi yake baada ya kuingia ikulu.

Kabila anasemekana alikuwa amesoma kitabu cha Raphael Ntibazokiza kikieleza mahusiano ya Watutsi na wabantu, kiitwacho
Plan de la colonisation tutsi au Kivu et region centrale de l'Afrique – Mpango wa ukoloni wa Kitusi katika Kivu na eneo la Afrika ya Kati.

Raphael anaandika, "Mhutu ameumbwa kufanyia kazi watu wengine; hawezi hata kujaribu kupata uongozi. Chukua nafasi zote za mikoa na wilaya na atakayekuwa mtawala ahakikishe kuwa analinda maslahi yetu... Baadaye watakapokuja kustuka, watakuwa wamechelewa…"

Mmoja wa waliokuwa karibu na Laurent Kabila amenukuliwa akisema hakuna kitu kilichomsononesha Kabila kama kauli ifuatayo ndani ya kitabu cha Raphael:
"Tutumie ukarimu wao. Tujinyenyekeze kwao kama sisi ni watumishi wao.

Tukiishachukua nafasi zao tuwatelekeze na ‘kuwalipa ujira wa nyani'- payez-les en monnaie de singe pour montrer leur incapacite – ili kudhihirisha kuwa hawana uwezo."

Kabila aliuawa kabla hajamaliza kunyukana na Rwanda. Aliuawa na mmoja wa "watoto" wake – vijana wadogo waliokuwa watu wa karibu sana na waliomlinda tangu akiwa msituni.

Kuna maelezo tatanishi juu ya kifo chake. Kuna wanaodai aliyemuua alitumwa na waliokuwa wakitaka atekeleze makubaliano ya Lemera; lakini wengine wanadai ni karata za nchi za Magharibi.

Kwa kuwa Jonas Savimbi aliuawa katika wiki moja tu baada ya kifo cha Kabila, inadaiwa kulikuwa na mkono wa mataifa makubwa; hili likitaka kuingia Kongo na hivyo kuomba msaada wa kuondoshwa kwa Kabila huku likiwezesha kukamatwa na kuuawa kwa Savimbi. Siasa hizi hazijafafanuliwa.

Kuingia kwa Joseph Kabila, anayedaiwa kuwa mtoto wa kufikia wa Laurent Kabila, kunaonekana kuleta mgeuko mwingine kuelekea kule ambako "baba" yake alikataa.
Kinachoitwa makubaliano kati ya serikali ya Rwanda na ile ya Kongo kinaonekana wazi kuwa utekelezaji wa mpango wa awali ambao Laurent Kabila alikataa.

Aidha, kukamatwa kwa
Jenerali Laurent Nkundabatware na kuhifadhiwa nchini Rwanda kunaelezwa kuwa sura kamili ya "kuheshimu kazi ya maandalizi aliyokuwa akifanya nchini Kongo."

Kuna madai kuwa Nkundabatware, Mnyarwanda kutoka Rwanda, lakini Rwanda inasema ni Mkongomani, hakuwa na jeshi lolote nchini Kongo. Aliongoza majeshi ya Rwanda hadi hapo ilipoonekana kuwa mazingira yamekuwa mazuri kwa Rwanda kuingilia kwa kisingizio cha "kufukuza Interhamwe na kuweka usalama mpakani."

"Hata akipelekwa Kongo leo hii, Kabila atamlinda Jenerali Nkundabatware, labda kama wakuu wa Kongo na Rwanda watakuwa wamegundua kuwa amewasaliti," kimeeleza chanzo cha habari hizi mjini Goma.

Rwanda imeingia Kongo. Nani ataiondoa? Baadhi ya nchi jirani zimekuwa watazamaji tu wakati nyingine zikiwa katika maandalizi ya kunufaika kutokana na mgogoro wa nchi hii.

Moses Byaruhanga, waziri katika ofisi ya rais (Siasa) nchini Uganda, amesema nchi yake inaunga mkono "shirikisho la Kivu na Kisangani" na kwamba wanasubiri kuona serikali ya Kinshasa inalionaje suala hilo.

Katika siku za karibuni kumekuwa na taarifa za kukamilisha kumegwa kwa mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kutoka Jamhuri ya Kongo na kuzifanya muungano wa Jamhuri ya Kivu.

Kauli ya msemaji wa ikulu Uganda inaongeza uwezekano wa kuimega Kongo pale inapohusisha jimbo jingine la Kisangani ambako majeshi ya Uganda yanadai kuwinda waasi wa Lord's Resistance Army (LRA).

Kiongozi wa LRA, Joseph Kony amekuwa akipambana na majeshi ya serikali ya Yoweri Museveni kwa zaidi ya miaka 15. Uganda sasa inadai kuwa Kongo inatumika kama kichaka cha waasi hao.

Kauli ya Uganda haipishani na mipango inayodaiwa kufanywa na Rwanda ingawa Rwanda, kupitia balozi wake mjini Dar es Salaam ilikaririwa ikisema haina mpango wowote wa kuigawa Kongo.

Jumuiya ya kimataifa imetekwa kwa propaganda za Interhamwe, Wanyamulenge, waasi wa LRA na kumbukumbu za mauaji ya kimbari.

Isipokuwa Barrack Obama ambaye angalau amesema anataka Kongo tulivu na kwamba atasaidia kuleta hilo, mataifa mengine, pamoja na Ufaransa, yanataka kuimega Kongo.
 
M

mourad77

Senior Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
177
Points
0
M

mourad77

Senior Member
Joined Sep 13, 2012
177 0
Namna hii ndio tunataka Bonge la Uzi hili uchambuzi na upembuzi yakinifu sijui wapi nikugonge like
 
Tango73

Tango73

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2008
Messages
1,678
Points
1,195
Tango73

Tango73

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2008
1,678 1,195
Namna hii ndio tunataka Bonge la Uzi hili uchambuzi na upembuzi yakinifu sijui wapi nikugonge like
SAWA MZEE NIMEKUSIKIA! huyu raisi Kagame , analilia ardhi ya wakongo utadhania vile mtoto mchanga aliliavyo ziwa la mama kunyonya.

South africa, Tanzania, Kenya na Uganda zote zimo katika dili la kutaka kongo igawiwe mtutsi. Ndio maana unaona mgogoro huo hauna mwisho wala hautatuliki. Hao no watutsi ndugu yangu. ni watu wakorofi saaaaaanah saaaanah.Leo wameshika Uganda, Rwanda na Burundi na sasa wanataka kuiteka kongo. Je kwa nini Kenya na Tanzania zinataka kuungana nao kuunda jumuia ya africa mashariki pampja na watu wahuni kama hao?
 
J

jossy chuwa

Member
Joined
Apr 4, 2012
Messages
93
Points
0
J

jossy chuwa

Member
Joined Apr 4, 2012
93 0
Sasa kama hilo mwanahalisi lililoleta hiyo bonge ya ukweli wa kina limefungiwa tutapata wapi habari kwa kuna jinsi hiyo? Asante mkuu. vita hivyo ni vigumu kumalizika kirahisi.
 
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined
Oct 4, 2007
Messages
14,208
Points
2,000
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined Oct 4, 2007
14,208 2,000
Nimesoma sana habari za Kongo kuanzia enzi za Patrice Lumumba, Joseph Mobutu, Joseph Kasavubu na Moise Tshombe na waasi kama Pierre Mulele. Kisha nikasoma habari za wapinzani kama akina Jean Nguza Carl i Bond, na Etienne Tshikedi. Pia kuna wanafiki kama Kengo wa Dondo. Historia ya Congo inasikitisha sana.

Katika habari zote ambazo zimekuwa zikiandikwa humu JF kuhusu vita ya Congo wakati wa Ukombozi wa pili wa Congo chini ya Joseph Desire Kabila naona hii habari ina ukweli mwingi na ina uchambuzi wa uhakika. Imegusa Bahima Empire (japo haijatamka) lakini mkataba wa Lamera unaonyesha jinsi ambavyo Watutsi walikuwa wanajipanga kuunda the Bahima Empire. Walimhadaa Mzee Kabila na kama kawaida viongozi wetu huwa hawaangalii mbele linapokuja suala la kwenda Ikulu. Iwe kwa msaada wa Mungu ama Shetani wao ni Ikulu tu. Mzee Kabila akaingia kichwa kichwa akapewa akina Kabarebe na Bizima wakamwingiza mamlakani. Akakengeuka na kuwafukuza kabla hajajipanga vizuri! Masikini wakamshughulikia.

Mwanaye na Kabila anajua ni nini Wanyarwanda wanakitaka na huo mkataba anaujua. Ndio maana kila maasi yanaanzia Bukavu. Kiu ya Bahima Empire ni Janga kwenye eneo la Maziwa Makuu.
 
M

MIGNON

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2009
Messages
3,058
Points
2,000
M

MIGNON

JF-Expert Member
Joined Nov 23, 2009
3,058 2,000
SAWA MZEE NIMEKUSIKIA! huyu raisi Kagame , analilia ardhi ya wakongo utadhania vile mtoto mchanga aliliavyo ziwa la mama kunyonya. South africa, Tanzania, Kenya na Uganda zote zimo katika dili la kutaka kongo igawiwe mtutsi. Ndio maana unaona mgogoro huo hauna mwisho wala hautatuliki. Hao no watutsi ndugu yangu. ni watu wakorofi saaaaaanah saaaanah.Leo wameshika Uganda, Rwanda na Burundi na sasa wanataka kuiteka kongo. Je kwa nini Kenya na Tanzania zinataka kuungana nao kuunda jumuia ya africa mashariki pampja na watu wahuni kama hao?
"Mbega aliponzwa na uzuri wake" na hivyo ndivyo ilivyo kwa Congo.Congo ni tajiri mno na kama una muda na nafasi kitafute kitabu kiitwacho,King Leopord ghost na hapo utaona jinsi Congo ilivyojenga Belgium.
 
Ami

Ami

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Messages
1,984
Points
1,250
Ami

Ami

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2010
1,984 1,250
Picha ninayoipata ni mgogoro wenye matawi mengi.Kubwa ni ujinga wetu waafrika na roho mbaya.
Hatuhurumiani wenyewe ndio maana mataifa ya nje hayakomi kututawala.
Hivi tukiona wakongo wakibeba magodoro na mabegi yao mgongoni hatuumi.Kwanini hatupendi tuwaona na wao wakibeba laptop zenye maandishi ya akili zao?.
Swali jengine baada ya kusoma makubaliano hayo ni hivi Tanzania tukifikiria kuingia kijeshi Kongo tunakusudia kuvuna nini?.
 
mangikule

mangikule

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2012
Messages
3,818
Points
2,000
mangikule

mangikule

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2012
3,818 2,000
Nimesoma sana habari za Kongo kuanzia enzi za Patrice Lumumba, Joseph Mobutu, Joseph Kasavubu na Moise Tshombe na waasi kama Pierre Mulele. Kisha nikasoma habari za wapinzani kama akina Jean Nguza Carl i Bond, na Etienne Tshikedi. Pia kuna wanafiki kama Kengo wa Dondo. Historia ya Congo inasikitisha sana.

Katika habari zote ambazo zimekuwa zikiandikwa humu JF kuhusu vita ya Congo wakati wa Ukombozi wa pili wa Congo chini ya Joseph Desire Kabila naona hii habari ina ukweli mwingi na ina uchambuzi wa uhakika. Imegusa Bahima Empire (japo haijatamka) lakini mkataba wa Lamera unaonyesha jinsi ambavyo Watutsi walikuwa wanajipanga kuunda the Bahima Empire. Walimhadaa Mzee Kabila na kama kawaida viongozi wetu huwa hawaangalii mbele linapokuja suala la kwenda Ikulu. Iwe kwa msaada wa Mungu ama Shetani wao ni Ikulu tu. Mzee Kabila akaingia kichwa kichwa akapewa akina Kabarebe na Bizima wakamwingiza mamlakani. Akakengeuka na kuwafukuza kabla hajajipanga vizuri! Masikini wakamshughulikia.

Mwanaye na Kabila anajua ni nini Wanyarwanda wanakitaka na huo mkataba anaujua. Ndio maana kila maasi yanaanzia Bukavu. Kiu ya Bahima Empire ni Janga kwenye eneo la Maziwa Makuu.
Nimeipenda hii hasa hapo penye nyekundu MAFISI_URAIS wapo kila mahali teh teh teh teh! Beware tunao hapa kwetu!
 
Tai Ngwilizi

Tai Ngwilizi

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2010
Messages
781
Points
170
Tai Ngwilizi

Tai Ngwilizi

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2010
781 170
Kivu,... wanaohangaika zaidi sasa ni wanawake na watoto, wanajeshi wana tumia rape kama njia za makusudi za kuwatisha na kuwacontrol wakongo.
huwa inaniuma sana napofikiria kuna vijana wa Kivu, wenye miaka 20 na kitu waliozaliwa katika hali hii na kukulia katika hali hii, maisha yao yote hawajui amani maskini......
 
B

Bukyanagandi

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2009
Messages
7,959
Points
2,000
B

Bukyanagandi

JF-Expert Member
Joined Jun 24, 2009
7,959 2,000
Nimesoma sana habari za Kongo kuanzia enzi za Patrice Lumumba, Joseph Mobutu, Joseph Kasavubu na Moise Tshombe na waasi kama Pierre Mulele. Kisha nikasoma habari za wapinzani kama akina Jean Nguza Carl i Bond, na Etienne Tshikedi. Pia kuna wanafiki kama Kengo wa Dondo. Historia ya Congo inasikitisha sana.

Katika habari zote ambazo zimekuwa zikiandikwa humu JF kuhusu vita ya Congo wakati wa Ukombozi wa pili wa Congo chini ya Joseph Desire Kabila naona hii habari ina ukweli mwingi na ina uchambuzi wa uhakika. Imegusa Bahima Empire (japo haijatamka) lakini mkataba wa Lamera unaonyesha jinsi ambavyo Watutsi walikuwa wanajipanga kuunda the Bahima Empire. Walimhadaa Mzee Kabila na kama kawaida viongozi wetu huwa hawaangalii mbele linapokuja suala la kwenda Ikulu. Iwe kwa msaada wa Mungu ama Shetani wao ni Ikulu tu. Mzee Kabila akaingia kichwa kichwa akapewa akina Kabarebe na Bizima wakamwingiza mamlakani. Akakengeuka na kuwafukuza kabla hajajipanga vizuri! Masikini wakamshughulikia.

Mwanaye na Kabila anajua ni nini Wanyarwanda wanakitaka na huo mkataba anaujua. Ndio maana kila maasi yanaanzia Bukavu. Kiu ya Bahima Empire ni Janga kwenye eneo la Maziwa Makuu.
Well said, mimi niliwahi kutadhalisha kuhusu HIMA Empire zaidi ya miaka mitatu lilyopita - na hii aitaishia North/South KIVU tu ina-cover na part ya TANZANIA, kama ulivyo sema eneo la maziwa Makuu - sioni kama viongozi wetu hilo wanaliona au kulishtukia wako blind KABISA: Kuna jamaa mmoja wa Mombasa alimejaribu kufanya analysis ya kitu kinacho endelea sasa hivi kinacho shangaza wengi - hisipokuwa viongozi wetu wa Kiafrica I guess ambao hawaoni janga linalo tunyemelea ina our lifetime: Mkuu soma linki hii:https://www.jamiiforums.com/international-forum/359191-leaders-betray-africa-on-m-23-rebels.html

Nakushukuru kwa kuona mbali mkuu, oh one more thing hivi wakina Kengo wa Dondo na Jean Nguza Carl i Bond walihishia wapi? Are they still alive!
 
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined
Oct 4, 2007
Messages
14,208
Points
2,000
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined Oct 4, 2007
14,208 2,000
Well said, mimi niliwahi kutadhalisha kuhusu HIMA Empire zaidi ya miaka mitatu lilyopita - na hii aitaishia North/South KIVU tu ina-cover na part ya TANZANIA, kama ulivyo sema eneo la maziwa Makuu - sioni kama viongozi wetu hilo wanaliona au kulishtukia wako blind KABISA: Kuna jamaa mmoja wa Mombasa alimejaribu kufanya analysis ya kitu kinacho endelea sasa hivi kinacho shangaza wengi - hisipokuwa viongozi wetu wa Kiafrica I guess ambao hawaoni janga linalo tunyemelea ina our lifetime: Mkuu soma linki hii:https://www.jamiiforums.com/international-forum/359191-leaders-betray-africa-on-m-23-rebels.html

Nakushukuru kwa kuona mbali mkuu, oh one more thing hivi wakina Kengo wa Dondo na Jean Nguza Carl i Bond walihishia wapi? Are they still alive!
Kengo wa Dondo bado yu hai na yupo Congo ila Nguza Carl i Bond hatukonaye tena yuko mbele za haki.
 
K

Koba

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Messages
6,140
Points
1,500
K

Koba

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2007
6,140 1,500
Hivi hizi garbage mnatoaga wapi? pls fanyeni research muelewe hii Congo crisis nawashauri achaneni na hizi street talk, propaganda/fake politics...hivi mnajua hata kuna factions ngapi zinapigana kule Congo and why?Congolese wakiamua hii vita iishe itaisha bila msaada wa mtu yeyote kutoka nje ila selfish/greed and stupidity ndio inawamaliza,hii vita has nothing to do na hizo garbage zenu za Hima empire or Kigali...ningekuwa kagame ningefunga mpaka na kuwaambia hao UN waje wakae hapo mpakani then uone kama vita itakwisha na amani kupatikana.
 
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined
Oct 4, 2007
Messages
14,208
Points
2,000
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined Oct 4, 2007
14,208 2,000
Hivi hizi garbage mnatoaga wapi? pls fanyeni research muelewe hii Congo crisis nawashauri achaneni na hizi street talk, propaganda/fake politics...hivi mnajua hata kuna factions ngapi zinapigana kule Congo and why?Congolese wakiamua hii vita iishe itaisha bila msaada wa mtu yeyote kutoka nje ila selfish/greed and stupidity ndio inawamaliza,hii vita has nothing to do na hizo garbage zenu za Hima empire or Kigali...ningekuwa kagame ningefunga mpaka na kuwaambia hao UN waje wakae hapo mpakani then uone kama vita itakwisha na amani kupatikana.
Mkuu acha kutukana watu toa facts. Alichokisema mwandishi wa Makala ndicho kinaimaliza Kongo. Ni Bahima Empire na madini ya Congo basi. Kama si Bahima Laurent Nkunda yupo wapi? Huyu si alikamatwa Rwanda ameishia wapi? Hukubali pia kwamba Rwanda iliingia Kongo wakati wa Kabila kwa makubaliano Maalum? Hujui pia kwamba baada ya Kabila kushtuka akiwa Ikulu aliwafukuza Wanyarwanda na kuomba msaada wa watanzania? Huamini kwamba akina Bizima Karaha na Kabarebe walikuwa wakiitumikia Kigali?

Toa facts tuone Kongo inamalizwa na nini kama siyo Bahima iliyotawanyika kuanzia Ethiopia, Uganda, Kongo, Rwanda, Urundi na viunga vya Tanzania?
 
COURTESY

COURTESY

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2011
Messages
2,009
Points
1,225
COURTESY

COURTESY

JF-Expert Member
Joined Jun 16, 2011
2,009 1,225
Hivi hizi garbage mnatoaga wapi? pls fanyeni research muelewe hii Congo crisis nawashauri achaneni na hizi street talk, propaganda/fake politics...hivi mnajua hata kuna factions ngapi zinapigana kule Congo and why?Congolese wakiamua hii vita iishe itaisha bila msaada wa mtu yeyote kutoka nje ila selfish/greed and stupidity ndio inawamaliza,hii vita has nothing to do na hizo garbage zenu za Hima empire or Kigali...ningekuwa kagame ningefunga mpaka na kuwaambia hao UN waje wakae hapo mpakani then uone kama vita itakwisha na amani kupatikana.
Elezea facts ulizonazo na si kupinga facts za watu kwa weak points zako.Toa hoja zako bana
acha kubwabwaja mkuu
 
malema 1989

malema 1989

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Messages
1,310
Points
1,500
malema 1989

malema 1989

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2012
1,310 1,500
Namna hii ndio tunataka Bonge la Uzi hili uchambuzi na upembuzi yakinifu sijui wapi nikugonge like
nisikuchukie kama kagame na ndugu yake museveni, ipo siku yao tu!!!!!!
 
Nyalotsi

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Messages
6,409
Points
2,000
Nyalotsi

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2011
6,409 2,000
Kengo wa Dondo bado yu hai na yupo Congo ila Nguza Carl i Bond hatukonaye tena yuko mbele za haki.
kabila mtutsi, museven mtutsi, kagame mtutsi, wa burundi mtutsi ambao ukifuatilia wamma historia moja na wasomali ambao kinana amepewa chama cha kuiba kura. Unategemea eac tutasalimika?
 
Nyalotsi

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Messages
6,409
Points
2,000
Nyalotsi

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2011
6,409 2,000
Elezea facts ulizonazo na si kupinga facts za watu kwa weak points zako.Toa hoja zako bana
acha kubwabwaja mkuu
huyu yawezekana anawazungumzia kina bemba waliokuwa wanapingana na utawala wa kinyarwanda ulioletwa na kabila pamoja na zile za wanufaika wa mobutu.
 
Songambele

Songambele

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2007
Messages
4,419
Points
2,000
Songambele

Songambele

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2007
4,419 2,000
Sasa ndio utajua kama hao jamaa ni sehemu ya Tanganyika lakini wananguvu mpaka waliweza kutoka kupata eneo lao then watapata sehemu congo ndio wanaongoza sasa manake Jose ni mtoto wao. Uganda ni kwa wajomba zao Tz tulitakiwa kuanzisha zengwe la kudai mikoa yetu ya Rwanda na Burundi kwanza na kuchukua Malawi.

Matatizo ya Wacongo bado waachiwe wenyewe kuyatatua na hakuna shaka the country is too big kwa serikali ya kabila kusimamia given the distance between north and south na hakuna miundo mbinu. Nchi kubwa sana ilikuwa congo na sudan sasa congo inatakiwa kugawiwa mara nyingine na diversity ni kubwa kama bongo kuna masai, luo, tutsi, makonde then hata tutsi watakuwa pia ndani ya congo.

Kabila ameshindwa na Afrika sasa ijifunze kusema ukweli kwa kumwambia dogo kashindwa na awezi ongoza peke yake na uasi ni jina la kudumu tu hata baba yake kabila aliitwa hivyo, na libya pia waliitwa hivyo.
 
majany

majany

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2008
Messages
1,224
Points
1,225
majany

majany

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2008
1,224 1,225
Elezea facts ulizonazo na si kupinga facts za watu kwa weak points zako.Toa hoja zako bana
acha kubwabwaja mkuu
Usingizi wa mchana sio mzuri sana!!!Yaelekea jamaa ndo katoka kwenye kitanda!!
 
Forum statistics

Threads 1,402,764
Members 530,977
Posts 34,404,375
Top