MKATABA MPYA WA DOWANS KUJADILIWA NA WANANCHI kwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MKATABA MPYA WA DOWANS KUJADILIWA NA WANANCHI kwanza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AMARIDONG, Mar 1, 2011.

 1. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  WAZIRI MKUU AMESEMA MKATABA MPYA AMBAO SERIKALI INAINGIA NA DOWANS ILI KUWASHA MITAMBO YAKE KABLA YA MWISHO WA MWEZI HUU UTAWEKWA HADHARANI NA KILA MTANZANIA ATAKUWA NA NAFASI YA KUUONA NA KUUJADILI KABL YA MITAMBO HIYO KUWASHWA

  bora tuuchambua kwanza
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Washirikishwe wataalamu wa tanesco na pia TLS ama UD faculty of law,TRA na Treasure
  kwani wakiyanunua itakuwa tabu? Wakipata umeme si watayapeleka tandahimba na kwingineko ambako grid ya taifa bado ni ndoto?
  I am afraid capacity charges zitakuwa high na pia sio suluhisho la kudumu
   
 4. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hakuna kuujadili kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na PM. soma mada kwenye link #2
   
 5. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Semeni yote
   
 6. w

  warea JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini iwe Dowans tu! Kwani hakuna makampuni mengine yanayoweza kuzalisha umeme duniani?

  Bora tenda itangazwe na makampuni yanayoeleweka yachukue hii kazi. Dowans asiruhusiwe kabisa na tena achukue mitambo yake.
   
 7. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  hapo mengi atanuna weeee
   
 8. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  AMESEMA NAFASI ITATOLEWA YA KUJADILI KABLA YA KUINGIA MKATABA MPYA NA DOWANS

  alaaaaaaaaa
   
 9. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kimsingi, Neno DOWANS tunataka litoweke Tanzania. Ni bora tuwe giza kuliko kuhalalisha mkataba uliongiwa kifisadi. Kinachonishangaza mimi, kwa nini serikali isiruhusu private sector kusambaza umeme na tukawa na makampuni mengi tu ambayo mtu anachagua yeye binafsi aingie mkataba na kampuni gani. Tanesco ibakie kwenye miuondo mbinu tu yaani kufunga nyaya na za kusambaza umeme nchi nzima Hii itakuwa kama hivi

  1. Miuondo mbinu yote inabakiwa kuwa ya TANESCO na Kazi yao ni kuhakikisha kuwa inasimamiwa kwa ufasaha

  2. Kampuni binafsi zenye Magerator au reactors au Dams zinazalisha umeme na kuwa connected kwenye Grid ya Taifa ambayo at the point of entering inakuwa monitored na TANESCO ili wasije kusema wameuza umeme mwingi kwa wateja wao wakati wao wameingiza kwenye Grid units chache, kiwango kinachoingia kwenye Grid si kipimo cha kulipwa kwa Kampuni bali watakusanya madeni yao kutoka kwa wateja wao moja kwa moja

  3. Mteja anakuwa na option ya kubadili kampuni kama anaona inauza umeme kwa bei ya juu ukilinganisha na kampuni ingine

  4. Makampuni haya yatatakiwa kuilipa TANESCO kwa kutumia miundombinu yao, ila nani anatumia kiasi gani na kwa muda gani hiyo si kazi ya TANESCO.

  5. TANESCO inakuwa na kazi pia ya ku-monitor/detect kwa kutumia meter zao kwa kila supplier Kama kampuni haizalishi basi mapato yake yanakwenda kwenye makampuni yanayozalisha umeme wakati huo kwa proportion ya nini wanaingiza kwenye grid out of total. Hii itaondoa mchezo wa kukatakata umeme bila sababu maana kama kampuni ikizima mitambo basi zile inayoendelea kusupply ndiyo zinakuwa na haki ya kupata mapato ya masaa ya kampuni ingine wakati ipo idle.

  Katika Mazingira kama haya Pesa ya mlipa kodi haitatumika hata chembe na hakutakiwi kuwa na Mkataba wa Ki-Carl Peters kama wa Dowans, Maana unaingia mkataba wakati mabwawa hayana maji by the time Maji yanajaa na hamuhitaji umeme then unatakiwa kuendelea kulipa tu the so called capacity charges etc, ila kama hawa jamaa wangeruhusiwa kujitangaza na kutafuta wateja miongoni mwa watumiaji wa umeme huu upuuzi wote usingekuwepo. Tatizo la Tanzania viongozi wapo kwa masilahi binafasi na wanaona kuliachia kampuni kama TANESCO kuwa free na kukaribisha wawekezaji halali watapoteza ulaji wao.
   
 10. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,713
  Likes Received: 3,122
  Trophy Points: 280
  Dowans ni hivi mitambo yenu ni mali ya watanzania hakuna mkataba hamtaki nendeni na mitambo yenu wacha tuendelee kukaa na giza mpaka kieleweke. Mmekosa hivi ni million au billion whatever sasa mnataka tuwalipe kwa njia moja au nyingine.
   
 11. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,289
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Akumbushwe arejee taarifa yake aliyoisoma bungeni tarehe 28 Agosti 2008. Hivi hawa viongozi wetu wamerogwa na nani? CHADEMA kazeni kamba!
   
Loading...