T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 10,720
- 35,243
bad bila bila
Siku hizi hauko active sana. Mada zako nzito nilizisoma nikiwa sina akili sana, ulinishawishi kujiunga JF.Duh! Weye mchawi nini Mkuu? nilikuwa kwenye uzi huu huu sekunde chache zilizopita mara napata notification yako. Nishazuka Mkuu.
Siku hizi hauko active sana. Mada zako nzito nilizisoma nikiwa sina akili sana, ulinishawishi kujiunga JF.
Endelea mkuu..UPDATE NO 2: THURSDAY 14/05/2020
Kikao cha dharura cha wanaume kilichofanyika hivi karibuni kinaonekana kugongana sawia kabisa na mambo mawili makubwa
Kwa hiyo ukizingatia mambo hayo mawili hapo juu, ukiunganisha na mood aliyokuwa nayo mwenyekiti wakati anafungua kikao, inaonyesha KAMA:
- Kilifanyika J2 iliyofuatia ile ya mgogoro wa Sanitizer
- Klilifanyika katika wiki ambayo J3 ya wiki hiyo, mhusika wa taarifa hizi aliamua kuanza kutoa rasmi taarifa za matendo anayofanyiwa yasiyomridhisha na mengine pia yanayoendelea Kanisani hapo, kupitia mtandao huu
Na kama ni kweli kwamba yeye alikuwa ni potential target:
- Mwenyekiti aliamua kutumia lugha ya ukali na kufoka sehemu ambayo haistahili, yaani kanisani, na kwa sababu ambazo hazikuwa za msingi, akiwa na lengo la kutafuta targets ambao alijua huwa hawawezi kuvumilia kusikiliza ujinga, mhusika wa taarifa hizi akiwa mmoja wao
- kwa vile mhusika wa taarifa hizi alikuwa tayari ameshaazisha kitu ndani ya wiki hiyo, inaonyesha pia KAMA mojawapo ya potential targets zilizokuwa zimekusudiwa alikuwa ni yeye
Kwa hiyo iwapo kungeweza kutokea fujo mahli pale, uwezekano mkubwa ni kwamba fujo hiyo ilikuwa imepangwa, na possibly kuna watu ambao tayari walikuwa wameandaliwa kwa ajili ya kuianzisha
- haina shaka kuwa kulikuwa na kitu kikubwa kilikuwa kimeandaliwa kwa ajili yake nyuma ya pazia, ambacho yeye alikuwa hakijui, na ndiyo maana hata viongozi karibia wote walikuwepo, akiwemo kiongozi mkuu mwenyewe.
- Kuna kitu kikubwa kilkuwa kimendaliwa nyuma ya pazia, yawezekana hata fujo ambazo zingelazimu hata vyombo vya dola kuwasili mahali pale kwa ajili ya kuja kuituliza ghasia
Mhusika anadai kuwa hawa viongozi ni wa hatari mno na huko nyuma wameshawahi kupanga matukio mengi tu ya hatari kwake ambayo baadhi atayaleta kwenu kadri habari hizi zitakavyokuwa zinawajia. Karibia mara zote wamekuwa katika mipango yao, wakishirikiana na staff mate wake ambaye naye huwa anaabudu mahali pale. Huyu mtu siku hiyo ghafla alionekana amekaa pembeni ya mhusika ila wakati wa Ibada hakuwa amemuona. Mhusika anadai ataleta angalau tukio moja kuthibitisha hatari iliyoko mahali pale
Hata hivyo, mhusika siku hiyo aliamua kuondoka kikaoni hapo baada ya kuona kinaelekea kule ambako yeye hakuwa ametarajia, akarudi nyumbani
MWANDISHI WENU ATARUDI TENA
UPDATE 18/05/2020