Mkasa uliowahi kumpata "PENDO"

Mkasa uliowahi kumpata "PENDO"

exalioth

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2016
Posts
2,395
Reaction score
4,152
Pendo alikuwa mhudumu wa baa katika maeneo fulani ambapo alifanya hiyo kazi akiwa kama kaunta, katika baa ile ilikuwa ni mwisho saa 6 usiku ndio wanafunga

Siku1 walipata wateja ambao ilipelekea wakafunga muda umeenda sana wahudumu wenzie walienda kulala Pendo alibaki peke yake na wateja ambao alikuwa anawahudumia yeye ilifika kama muda wa saa7:30 hivi wale walevi wakaondoka na yeye akaingia ndani wakati huo walikuwa wakilala palepale baani kulikuwa na vyumba vyao wahudumu wote

Pendo alilala kama nusu saa akabanwa kukojoa akaamka alivyofungua mlango alishituka kuona watu kama kumi hivi katikati ya uwanja wa baa wamevalia mavazi meusi huku wakiongea kwa kunong'onezana aliogopa akafunga mlango polepole akalala huku roho ikimdunda baada ya muda kama dakika15 mlango uligongwa akiitwa "pendo"pendo"aliijua ni sauti ya bosi wake mmiliki wa baa akamwambia atoke nje,


Alivotoka akafatwa na watu watatu pamoja na bosi wake akiwa hapo wakamuuliza:

Tumekuona ukifungua mlango baadae ukafunga uliona nini?

Pendo: Sikuona kitu

Pendo aliwekewa bastola kuanzia kichwani mpaka miguuni kisha akapewa onyo kuwa wakisikia amevujisha alichokiona watamuua pia hata bosi wake alimwambia afanye kazi asiyaongee masuala yasiyomhusu alienda kulala ila mazungumzo waliokuwa wakizungumza ni ya kihalifu walikuwa wanaenda kuvamia sehemu

Hivyo Pendo amejikuta akifanya kazi katika ile baa hadi umri umeenda sana akihofia kuacha kazi atauliwa.
 
Ikawaje sasa...!
Mbona huyo Pendo alikupa hadithi yote ya kilicho tokea..!?
 
Wapi mkuu
Hili jina LA Pendo linatumika sana na wahudumu wa baa (kwa uzoefu wangu lakini) maana hata nilipo sasa hivi baa kaunta anaitwa Pendo sasa sijui ni yeye?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom