Mkapa uso kwa uso na Profesa Issa Shivji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa uso kwa uso na Profesa Issa Shivji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OKW BOBAN SUNZU, Apr 12, 2012.

 1. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,810
  Likes Received: 17,910
  Trophy Points: 280
  BAADA ya kuongoza kampeni za uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki bila mafanikio, rais mstaafu, Benjamin Mkapa, anatarajiwa ‘kupambana' katika mjadala kuhusu "hali ya dunia ilivyo leo na mustakabali wa Afrika, akikabiliana na mwanazuoni.

  Profesa Issa Shivji ambaye ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Julius Nyerere pamoja na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Ng'wanza Kamata.

  Katika mjadala huo utakaofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Tamasha la nne la Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Julius Nyerere, Mkapa atashiriki kama Mwenyekiti wa Taasisi ya South Centre.

  Mkapa anatarajiwa kuwa kivutio kwa sababu mbalimbali ambazo licha ya kukabiliwa na fikra za kisomi kutoka kwa Profesa Shivji, ni yeye aliyekuwa bingwa wa kutetea utandawazi lakini pia kinara wa sera za ubinafsishaji zilizoasisiwa na nchi tajiri kwa kusimamiwa na mashirika yao, ambayo ni Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia (WB).

  Source: Raia Mwema
   
 2. M

  Mnyama Hatari JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo kuna mdahalo baina ya Mkapa na Shivji?
   
 3. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii post istick hadi baada ya mjadala.
  ila tuambie ni lini mkuu!
   
 4. Ork

  Ork Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ni kesho
   
 5. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,810
  Likes Received: 17,910
  Trophy Points: 280
  Ni kesho mkuu.Tayari Taasisi ya Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere imethibitisha kushiriki kwa Mkapa, ambaye atahudhuria siku ya pili ya tamasha hilo, Aprili 13. Katika siku ya kwanza ya tamasha hilo litakalofanyika kwa siku mbili mfululizo, mada nyingine mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa.
  Mada kuu ya siku hiyo ni itawasilishwa na Profesa Micere Mugo. Profesa Mugo atawasilisha mada kuhusu nafasi ya wasanii na sanaa katika ukombozi wa Bara la Afrika.
  Mbali na mijadala inayotarajiwa kuwa na mvuto mkubwa na hasa kutokana na umahiri wa waendesha mijadala sambamba na umahiri wa washiriki wa mijadala hiyo, kitabu cha Profesa Issa Shivji kitazinduliwa, ambacho ni mkusanyiko wa makala mbalimbali alizowahi kuandika Profesa Shivji.
   
 6. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,810
  Likes Received: 17,910
  Trophy Points: 280
  Ni kama mdahalo kutokana na tofauti za kiitikadi kati ya Mkapa na Prof.Shivji, itikadi za Mkapa ni za ubinafsishaji wa kifisadi while Prof. anaamini ktk J.K Nyerere
   
 7. A

  Awo JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 793
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Who invites Mkapa to grace anything in Nyerere's memory? He is not a good role model having done business in the State House (mahali patakatifu)! Nyerere must be turning in his grave!
   
 8. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,810
  Likes Received: 17,910
  Trophy Points: 280
  Mi nadhani pale ni mahali pazuri kummalizi huyu Pimbi, njooni tujumuike
   
 9. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Kuna watu tukisikia neno Mkapa tunapoteza appetite!
   
 10. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,817
  Likes Received: 36,921
  Trophy Points: 280
  I hope Mwl Nyerere atanena kupitia kinywa cha Prof. Shivji.
   
 11. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Pia atakuwa kivutio maana alishiriki kuutoa uhai Mwl ili aiuze NBC kwa bei ya kutupa
   
 12. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wewe lazima utakuwa pacha wa Jenerali Twaha Ulimwengu!!
   
 13. Micro E coli

  Micro E coli JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkapa anasema taasis zinazohusika na ubinafsishaji ziwaeleze wananchi jinsi nchi ilivyo nufaika na ubinafsishaji,huyu mzee namuona sasa kaanzakuchanganyikiwa yeye ndio alikuwa Rais ndio msimamia sera hiyo mkuu,halafu suala la kwenda kuwasimulia wananchi maendeleo ya kusadikika kwa matakwimu ya kuchakachua wakati maendeleo hawayaoni eti mpaka taasisi hizo ziwasimulie ni ajabu kbs.
   
 14. The Eagle2012

  The Eagle2012 Senior Member

  #14
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Ukiona Faida hazionekani mpaka zielezwe saana basi Ujue hazipo in the first place!!
  Benjamin is way too stupid to have led a country!!!
   
Loading...