Reincarnation haiwezi kutokea wakati roho yake bado imo mwilini mwake. Reincarnation is the soul rebirth.Na kama kulikuwa na rais mbishi mbabe na asiyeambilika yeye aliongoza.... and now I can see the reincarnation of him at this phase
Then anashauri wengine wasikilize wakati Yeye hakusikiliza pamoja na watu kupiga kelele. Latina vitu atajibu Huyu mheshimiwa ni kumsingizia baba wa Taifa Kuwa alikuwa happy na huo uwejezaji wake ikiwemo bank ya Taifa na wish angekuwepo amjibu. Hivi Kama kosa analotubu tu ni ubinafsishwaji hivi Bado hajaguswa na uuzwaji wa nyumba za serikali?? Ama nao ni ubinafsishwaji basi Kama Bado atakuwa na Ngozi Ngumu sanaNa kama kulikuwa na rais mbishi mbabe na asiyeambilika yeye aliongoza.... and now I can see the reincarnation of him at this phase
Nakumbuka alikuwa mbishi ka nini eti Leo ndo anaomba msamaha basi tutarajie na jk kuomba msamaha baada ya miaka kadhaa mbele.
Mali gani alinibinafsishia yeyeKumsamehe hatuwezi mpaka aanze kurejesha mali alizo jibinafsisha kwanza. Hichi kilio cha mamba tu
Waafrica bado tunahaki ya kutawaliwa hatujaweza kabisa kujitawala zaid ya viongozi kuwa wababe katika madaraka na mijizi ikimaza muda huomba msamaha Africa yote zaid ya Gaddafi hakuna kiongoziKama kuna kitu mwalimu alipinga kwa nguvu zote ni hili la kubinafsishwa kwa NBC Benki iliyokuwa ina mtandao mkubwa zaidi nchini (upo ushahidi kwenye hili)na mzimu wake unamuandama mpaka sasa
Yes na Kama jk asingekuta magangwe ya ufisadi yaneshaota mizizi nadhani mpaka Leo angekuwa one of the best leaders. Jk amefanya mambo mengi sana ya kizalendo kaacha vitu vingi vya kizalendo Kabisa tofauti na cartel za kiunyonyaji zilizoshamiri before him. Ubinafsishwaji ulikosa uzalendo Kabisa Wala si issue ya sera .kwani mzarendo ingemuuma aka rectify hata kabla ya kuagaKuna mchangiaji h anaendeleza uleule unafiki kwa kusema " eti BWM hilo ni fumbo anataka JK naye aombe msamaha" tuache unafiki watanzania matatizo yakiutendaji aliyoyaacha BWM yamesababisha makovu kwa kizazi mpaka kizazi karne mpaka karne, " ubinafsishaji bila usimamizi,uzalendo na uwajibikaji" matokeo yake ni failure ya miaka Mingi mno maana hatuna chetu leo ukivunja mkataba tumeliwa. Makosa ya JK ni yapi hebu yasemwe, maana kubwa linaloonekana ni hilo la ufisadi na wizi ambao nalo ni kaa la moto alilolikuta kama matokeo ya kufail kwa ubinafsishaji.
Tuache unafiki tuwe wakweli.
Hahahaha shetani ni shetani tu hawi malaika mijizi ikisha iba ndio huomba msamaha tuikatae msamaha wao Leo Hosp hata panadol hamna halafu linakuja kuomba msamaha inakera kweliShetani akizeeka anakuwa malaika .... kumbuka kauli hii toka mmoja wa wale alokuwa nao kwenye uongozi
"Ndege ya rais lazima inunuliwe hata kama wananchi watakula nyasi"
Yes
Yes na Kama jk asingekuta magangwe ya ufisadi yaneshaota mizizi nadhani mpaka Leo angekuwa one of the best leaders. Jk amefanya mambo mengi sana ya kizalendo kaacha vitu vingi vya kizalendo Kabisa tofauti na cartel za kiunyonyaji zilizoshamiri before him. Ubinafsishwaji ulikosa uzalendo Kabisa Wala si issue ya sera .kwani mzarendo ingemuuma aka rectify hata kabla ya kuaga
Binafsi khali hii ya viongozi wetu kufanya makosa yanayo gharimu maisha ya watu na kuchukulia is simple thing and normal DAIMA SITOKUBALIANA NA KAULI HIZI NA SITAKI KUWA MMOJA WATAKAO PATA HUKUMU HII.
Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Tanzania
Mkapa: Najuta
Posted by: Wolfram Mwalongo 16 hours
RAIS Mstaafu, Benjamin Mkapa haachi kujuta kutokana na baadhi ya yale aliyoyatenda kwenye utawala wake, anaomba Watanzania wamsamehe, anaandika Wolfram Mwalongo.
Kinachomfanya kujuta ni hatua ya utawala wake kukabidhi ‘injini ya uchumi’ wa taifa hili kwa wawekezaji chini ya ‘sera ya ubinafsishaji.’ Mkapa alikabidhi mashirika ya umma mikononi mwa wawekezaji bila kuwa na mkakati wa kusimamia ili sera yake iwe na tija kwa taifa.
Rais Mkapa alihudumia nchi hii kama rais kuanzia mwaka 1995 hadi 2005. Alipokea madaraka hayo kutoka kwa Rais Ali Hassan Mwingi aliyehudumia nchi kuanzia 1985 mpaka 1995, aliyeanza kuhudumia taifa hili kwenye ngazi hiyo ni Mwalimu Julius K. Nyerere tangu Uhuru 1961.
Akiwa kwenye Tamasha la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofayika kwenye Ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana Mkapa amekiri kwamba, hatua ya kuleta sera ya ubinafsishaji bila kuweka chombo maalum cha kudhibiti kumesababisha hasara.
Si mara ya kwanza kiongozi huyo mstaafu kusema maneno hayo hasa anapozungumzia maswala mazito katika utawala wake.
“Kukosekana kuundwa mfumo mzuri wa udhibiti kumesababisha kuwepo kwa watu waliotumia fursa hiyo kwa maendeleo yao binafsi na si kwa Taifa.
“Kwenye uongozi wangu kitu ambacho mpaka sasa ninajuitia ni kuanzisha sera ya ubinafsishaji na kushindwa kuweka mfumo au chombo cha kuudhibiti,”amesema Mkapa.
Mara kadhaa wachumi wa kitaifa wamekuwa wakikosoa utawala wa Mkapa kwa kuita wawekezaji na kuwapa ‘mali’ za taifa katika misingi mibovu ya uangalizi wake na kusababisha kuteketea kwa mali hizo. Miongoni mwayo ni viwanda, mashirika ya umma pamoja na Benki.
Mkapa kwenye tamasha hilo amesema “kuhusu ubinafsishaji huo ndio kitu naweza kukiri nilikosea na ninachoweza kuwaomba Watanzania msamaha.”
Mashiriki mengi ya umma pamoja na viwanda vilivyokabidhiwa kwa wawekezaji kutoka nje vilikufa na wengine kutumia mali hizo za taifa katika kujipatia mikopo na kufanya mambo mengine nje ya malengo yaliyokusudiwa.
Hata hivyo, Mkapa amesema “nilifanya kosa lakini hatuwezi kusema ubinafsishaji haufai kwa sababu ulisaidia kuleta mabadiliko na na kuongeza uzalishaji katika mashirika yaliyokuwa yameshindwa kuendeshwa na serikali.”
Ametoa mfano kwamba, “wakati mimi naingia madarakani viwanda vya sukari vya Mtibwa, Kagera, na Kilombero vilikuwa vikizalisha tani 120,000 hadi 130,000 lakini wakati naondoka niliacha vinazalisha tani 300,000.
“Mtibwa ilikuwa imeishakufa kabisa, lakini tuliweza kukirudisha na baada ya mimi kuondoka vimeendelea kuzalisha lakini inashangaza kuona miaka 17 wameshindwa kuongeza uzalishaji.”
Hata hivyo Mpaka alirudisha lawama kwa Watanzania kwamba, wana hulka ya kuzungumzia zaidi watu kuliko kuzungumzia sera na kuziboresha ili ziwe na tija kwa taifa.
Kwenye hotaba yake Mpaka amesema kuwa, Mwalimu Nyerere alishughulishwa katika kutafuta maendeleo ya Watanzania na kwamba, hakupinga ubinafsishaji kwenye taifa hili.
“Mwalimu Nyerere alikubali dhana ya ujasiriamali, uwekezaji, ushindani, ubunifu, ufanisi na utengenezaji wa faida vitu ambavyo viko sambamba na Ubepari,” amesema Mkapa na kuongeza;
“Vitu alikuwa anavitaka Mwalimu ni baadhi ya mambo mabaya ya Ubepari ikiwemo unyonyaji na mgawanyo wa faida usio sawa na ndio maana akaweka Azimio la Arusha akilenga kuwa na jamii ya usawa isiyo na unyonyaji.”
Akizungumzia ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) amesema, Mwalimu Nyerere aliona faida za ubinafsishaji na kwamba, aliona umuhimu wa kuibinafsisha benki hiyo.
“Kuhusu NBC Mwalimu si kwamba alikuwa anapinga kuibinafsisha bali ni namna ambavyo inaweza kuwanufaisha wananchi baada ya kuibinafsisha,” amesema Mkapa.
Tunaweza kudhani kaomba msamaha katika hali ya kawaida ya majuto ya kibinadamu, tunaweza kudhani kwamba kaamua kuwa muungwana na kufanya kitubio ili abaki na amani LAKINI katika picha pana ni salamu kwa Jakaya ni salamu za kutaka naye ajitokeze na kukiri pale alipokosea....halafu?
Ni salamu pia kwa Magufuri kwamba a jifunze kutokana na makosa ya watangulizi wake na kikubwa ASIKILIZE maoni ya wengine ASIKILIZE wananchi wanataka nini kwakuwa huko tuendako hakutakuwa na nafasi ya kuomba msamaha ukiwa jukwaani umevaa suti unasikilizwa bila kuhojiwa huku ukipigiwa makofi..!
Hapana hawezi kwenda hivyo kwakuwa yeye ni ndani yao sio mpinzani na anatumia lugha ya diplomasiaHata mimi naona hivyo hivyo, lakini sasa hao anaowatumia salamu naona kama angesema tu moja kwa moja tena kwa kuwataja majina ili wajue kuwa anawatumia salamu wao kwasababu, mh! sidhani kama hayo maono wanayo
Hapana hawezi kwenda hivyo kwakuwa yeye ni ndani yao sio mpinzani na anatumia lugha ya diplomasia