Mkapa na JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa na JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 22, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,607
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFFFFF"]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Mkapa, JK walipuliwa

  na Sitta Tumma, Mwanza
  Tanzania Daima

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]CHAMA cha Alliance for Demokratic Change (ADC), kimewalipua Rais Jakaya Kikwete na mtangulizi wake, Benjamin Mkapa, kwa madai kwamba wamehodhi rasilimali nyingi za taifa kwa maslahi yao binafsi na familia zao, kinyume cha taratibu na sheria za nchi.

  Katika utawala wake, Mkapa aliweza kujimilikisha shamba kubwa la miwa la Mtibwa huko Morogoro pamoja na mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, huku Rais Kikwete akituhumiwa kuhodhi rasilimali za madini.

  Akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Igoma jijini Mwanza juzi, Katibu Mkuu wa ADC, Lucas Limbu, alisema umaskini uliokithiri nchini unatokana na watawala kujali maslahi yao binafsi badala ya taifa.

  Alisema kuwa kitendo cha Rais Kikwete kushindwa kufumua mikataba ya kifisadi katika sekta ya madini ni kielelezo tosha kwamba na yeye ana maslahi katika mikataba hiyo.

  "Watanzania tunalalamika mikataba ya madini ni mibovu. Lakini Rais Kikwete amekaa kimya. Hawa watu wamejipanga kunyonya rasilimali za taifa. Mkapa akiwa madarakani aliingiza marafiki zake Ikulu ili wanyonye nchi. Alijimilikisha mgodi wa Kiwira na shamba kubwa la miwa la Mtibwa. Kwa hiyo ADC inawaomba Watanzania waichukie na wainyime kura CCM mwaka 2015," alisema.

  Katika mkutano huo zaidi ya wanachama 200 walijiunga na chama hicho kwa kukabidhiwa kadi mpya, huku kukiwa na upinzani mkali kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA, waliokuwa wakiitikia ‘Power' kila ilipotamkwa salamu ya ADC kwa kunyoosha vidole viwili vya alama ya ‘V' juu.

  Kwa upande mwingine, Limbu alimshukia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akimtuhumu kushindwa kusimamia vema majukumu yake na kwamba kwa sasa hawezi kumsimamisha kazi mkuu wa wilaya wala mkoa.

  Alisema Pinda ni muoga wa kuchukuwa hatua, huku akitolea mfano sakata la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, aliposhindwa kumwajibisha bungeni baada ya kudaiwa kukusanya fedha kinyume na utaratibu.

  Limbu alifafanua kuwa ADC ikiingia madarakani itahakikisha inasimamia na kuboresha zaidi sekta ya elimu na kuwa mradi wa kwanza wa serikali yake, kwani kwa sasa sekta hiyo imetelekezwa wakiwemo walimu.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Juzi nilitoa uzi hapa nikasema tuujadili mfumo wa ujamaa na kujitegemea lakini sikupata washabiki, lakini haya ya kujikusanyia mali huenda ikawa ni moja ya mapungufu ya mfumo huo. hapa watu wanaacha ujamaa wanafanya kujitegemea tu (kujilundikia mijimali) na kutusahai sisi wakulima na walipa kodi!
  Kwahiyo chama kitakacho ingia madarakani kiweke wazi mfumo wa rerikali itakayo ongoza nchi
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mkapa, si shamba tu la miwa. Hivi sasa anatafuta soko la korosho zake Marekani. Analo pia shamba la korosho.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,607
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jasusi kuna ufisadi mwingi tu wa Mkapa ambao Watanzania bado hatujaufahamu...Jamaa alikuwa mwizi sana kwa kutumia wadhifa wake kama Rais...Hata EPA, Meremeta na Kigoda lazima kutakuwa na mkono wake.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  yaani ni kama vile kuna ushindani....kila rais anataka amzidi mwenzie kwa kuchota mali nyingi za taifa hili....naona mwinyi ana hamu wakati wa enzi zake kungekua na gesi na mafuta ya kuiba ka wenzie wafanyavyo
   
 6. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,275
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  moendazoe alikuwa anaonekana kichaawakati anaonge ukweli kuhusu mkapa
   
 7. bysange

  bysange JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 4,378
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Tubadili mtizamo juu ya haya kwani mimi binafsi nimechoka kusikia ufisadi,ufisadi then no action,nani wa kumfunga simba kengele,Maana na kumbuka utotoni tuiliimba na kucheza hivi"smba ni mkali aliuwa mama akauwa baba watoto wangu..."hapa ,mashujaa walikuwa wakipatika kwa kuwapitawaliokuwa wakisimama kama simba,hawa wako wapi leo hii au ndio hawa tuitao mafisadi leo hii?
   
 8. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kwani haruhusiwi kuwa na shamba la korosho???
   
 9. ugolo wa bibi

  ugolo wa bibi JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 1,228
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kweli nchi hii nimeamini ni shamba la bibi, hakuna raisi aliyekuja zaidi ya mwlm!, akaonyesha kwa zati ya moyo wake kwamba anaumia na umaskini wa watanzania,sasa nimeamini watanzania tusipo amka sasa wajukuu zetu watakua watumwa tena kwa watanzania wenzao! inauma sana! jana nimeona gali la mtoto mmoja wa kiongozi,bila kushauliwa na rafiki yangu nilikua nalipiga mawe!inakera!
   
 10. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mwisho wao umekaribia watalia na kusaga meno.
   
 11. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Magamba hawatosheki! kila siku wanawaza kujilimbikizia mali!
   
 12. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180

  Jasusi mimi sina hakika juu ya Mkapa kuwa na shamba la korosho bali nina uhakika wa asili mia moja juu ya mama Mkapa kupitia NGO yake alinunua kiwanda cha kubangulia korosho kilichoko huko kusini!! Inawezekana korosho toka kwenye kiwanda hicho ndio zinatafutiwa soko huko marekani!! Kikwete anamiliki mgodi wa chuma na makaa ya mawe huko Ludewa kwa kupitia mgongo wa Subash Patel!! Hawa jamaa ni walafi wa mali wanakula mpaka wanatapika na bado wanaendelea kuila nchi.
   
 13. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Badala ya kuchoma makanisa waandamane kuharibu mali za hao walafi, potelea mbali tukose wote.
   
 14. Nyanya mbichi

  Nyanya mbichi JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 3,214
  Likes Received: 1,335
  Trophy Points: 280
  We hutaki kuandamana
  mbona wajitoa
   
 15. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kumiliki shamba la miwa na korosho ni makosa?
   
 16. f

  findu fiki JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lini??????
   
Loading...