Mkapa, Malecela, Sumaye wamkimbia Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa, Malecela, Sumaye wamkimbia Kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ujengelele, Oct 6, 2010.

 1. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkapa, Malecela, Sumaye wamkimbia Kikwete


  [​IMG]
  Na Saed Kubenea - Imechapwa 29 September 2010

  [​IMG][​IMG] [​IMG]


  VIGOGO waastafu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali, wamekacha kampeni za mgombea urais Jakaya Kikwete, MwanaHALISI limeelezwa.
  “Nakwambia kuna mgomo baridi ndani ya chama. Wastaafu wamekacha kampeni. Baadhi yao waligoma hata kuhudhuria siku ya ufunguzi wa kampeni,” amesema kiongozi mmoja wa chama hicho huku akitweta.
  Amesema, “Hata wale waliokuja siku ya ufunguzi pale Jangwani, wengi walifika kutimiza wajibu tu, lakini ukweli ni kwamba wamesusa kampeni.”
  Taarifa kutoka ndani ya CCM zinasema, uamuzi wa viongozi hao wastaafu unatokana na kile walichoita “Kikwete kuwa kichwa ngumu.”
  Kwa mujibu wa taarifa za waliokaribu na viongozi wastaafu, hatua hiyo imefuatia Kikwete kushindwa kutekeleza maagizo na ushauri mbalimbali wa chama na viongozi hao.
  Vigogo ambao wanadaiwa kukacha kampeni za Kikwete ni rais mstaafu Benjamin Mkapa, waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, Mama Maria Nyerere na makamu mwenyekiti mstaafu, John Samwel Malecela.
  Wengine wanaodaiwa kukacha kampeni ni rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salim Amour, mawaziri wakuu wastaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, Cleopa Msuya, Jaji Joseph Warioba na katibu mkuu mstaafu, Philip Mangula.
  Moja ya mambo yanayotajwa kutofurahisha wastaafu ni pamoja na serikali ya Kikwete kushindwa kupeleka bungeni muswada wa sheria ya “kutenganisha biashara na siasa” kabla ya uchaguzi mkuu mwaka huu.
  Tangu mapema baada ya kuingia madarakani, Kikwete aliahidi kurejesha nidhamu, uadilifu, uwajibikaji na hasa maadili ya uongozi kwa jumla, katika serikali na chama chake kwa njia ya kutenganisha siasa na biashara.
  Pamoja na kwamba Kikwete alilitaja hilo, ndani na nje ya mikutano ya chama, na hata kukaribia kujiapiza kuwa atalitenda, hakulitekeleza.
  Jingine ambalo linatajwa kukasirisha wastaafu ni hatua ya Kikwete kuhamishia kampeni za uchaguzi katika familia yake.
  Inadaiwa kuwa walioshika usukani wa kampeni za Kikwete ni mkewe, Salma na watoto wake, huku wakitumia rasilimali za umma.
  Wakati Salma anazunguka nchi nzima kukutana na akinamama, Ridhiwani anazungukia vijana na baadhi ya wazee anakoelekezwa na baba yake.
  Miraji Kikwete, mtoto mwingine wa Kikwete anadaiwa kushika mkoba wa fedha za kugharimia wasanii wanaozunguka na baba yake.
  Sababu nyingine ambayo inadaiwa kuwakoroga wastaafu ni Kikwete kuendelea kumkumbatia Yusuf Makamba katika nafasi yake ya katibu mkuu.
  Taarifa zinasema viongozi wastaafu walimtaka Kikwete kumwondoa Makamba katika wadhifa wake kwa maelezo kwamba hana uwezo wa kusimamia chama wakati huu wa uchaguzi.
  Makamba amekuwa akilalamikiwa na baadhi ya wanachama, wabunge na wajumbe wa NEC, kwamba anavuruga chama na anatenda kinyume na maagizo ya vikao vya chama.
  Bali kinachoelekea kuwastua wastaafu ni taarifa kwamba shughuli za chama zimehamishiwa mitaani Dar es Salaam badala ya kufanyika makao makuu madogo yaliyoko Mtaa wa Lumumba.
  Mtoa taarifa ambaye ametaka jina lake lisitajwe gazetini amesema, Miraji anaendesha shughuli za baba yake kutoka ofisi iliyoko Mtaa wa Undali, Na. 175, Upanga, Dar es Salaam.
  “Hapa ndipo imehamia timu nzima ya kampeni,” ameeleza mtoa taarifa.
  Miongoni mwa watu ambao wameonekana wakiingia na kutoka kwenye jengo hilo la ghorofa moja, ni Mwenyekiti wa Kampeni, Abdulrahman Kinana, Katibu wa rais, Rajabu Luhwavi na Ofisa Habari wa kampeni za Kikwete, Muhingo Rweyemamu.
  Wengine ni baadhi ya maofisa usalama wa taifa wanaofuatana na msafara wa Kikwete katika kampeni za uchaguzi na wengine wakiwamo wapigadebe wake wa mwaka 2005.
  Ni katika jengo hili inadaiwa kituo kimoja cha televesheni nchini, kilifanyia mahojiano na Aminiel Mahimbo anayedai kuwa mke wake Josephine Mushumbusi “amechukuliwa” na mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa.
  Mwaka 2005 mtandao wa Kikwete ulihamisha shughuli za kampeni za urais kutoka Lumumba na kuzipeleka katika ofisi binafsi iliyokuwapo Mtaa wa Mindu, Upanga.
  Inadaiwa ni katika ofisi hiyo, ilifanyika mipango ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi kutoka Benki Kuu (BoT) kupitia kampuni ya Kagoda na washirika wake.
  Kuhusu kampeni kufanywa na chama, mtoa taarifa amemnukuu mmoja wa vigogo akisema, “Tulitaka kampeni zimilikiwe na chama…lakini hatukusikilizwa. Sasa mtandao wake hauheshimiki. Chama hakiheshimiwi. Badala yake kampeni ziko mikononi mwa familia,” anasema.
  Chanzo chetu kilicho karibu na wazee hao kinahoji, “Sasa unataka wazee wastaafu waingie kama nani?”
  Alipoulizwa Tambwe Hizza, Naibu Mkuu wa Idara ya Propaganda ya CCM, juu ya tuhuma za kuhamishia shughuli za kampeni mitaani alikiri, “Waliohamia huko ni watu wa IT - mawasiliano na habari tu - na si kwamba timu nzima ya kampeni imehamia hapo.”
  Hata hivyo alisema “mambo yote yanafanyika hapa ofisi ndogo za makao makuu na hata hivi sasa ukija hapa utamkuta mzee Kinana akifanya shughuli za chama.”
  Mjumbe mmoja wa Halmashauri Kuu ya taifa (NEC) ambaye yupo karibu na Kinana ameliambia gazeti hili kuwa mwenyekiti huyo wa kamati ya kampeni ya Kikwete, amekataa kuhamishia shughuli zake mitaani.
  “Mzee Kinana huwa anakwenda pale mara mojamoja lakini hajahamishia shughuli zake pale. Anaogopa yasije kutokea ya mwaka 2005 na halafu jina lake likachafuka kwa jambo asilolijua,” kimesema chanzo chetu cha habari.
  Kuhusu kutenganishwa kwa siasa na biashara, mtoa taarifa anasema baadhi ya vigogo wastaafu wanadai kuwa kumekifanya chama kupitisha idadi kubwa ya wagombea ubunge na udiwani ambao ni wafanyabiashara na ambao hawafahamiki hata uadilifu wao.
  Habari zinasema, tofauti na mwaka 2005 ambapo CCM ilijaribu kuchuja baadhi ya wafanyabiashara, katika uchaguzi huu, karibu ya asilimia 70 ya wanaogombea ubunge ni wafanyabiashara.
  Mstaafu huyo ambaye hakutaka kutajwa jina anasema, “Kwa hali ya sasa, kusema chama hiki kinamilikiwa na wakulima na wafanyakazi ni kudanganya wananchi. Siwezi kushiriki katika kitu ambacho hata dhamira yangu inanisuta,” alieleza.
  Aidha, kutoonekana kwa vigogo wastaafu kunahusishwa na jinsi ambavyo baadhi ya viongozi wa sasa wamekuwa wakichukuliwa na chama.
  Wakati kuna madai kuwa Mkapa analalamikia kuchafuliwa na baadhi ya wanamtandao wa mwaka 2005, Jaji Warioba amekuwa akitishiwa kupelekwa mahakamani, jambo ambalo linadaiwa kulenga kumchafua.
  Vilevile Warioba amekuwa akidaiwa kumuunga mkono Dk. Salim katika kinyang’anyiro cha mwaka 2005; na mwaka jana alihusishwa na kuunga mkono maazimio ya kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere yaliyotaka rais achukue maamuzi mazito kurejesha heshima ya taifa.
  Naye, Dk. Salim amekuwa majeruhi mkuu wa mtandao wa Kikwete. Katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2005, ambapo alitwishwa zigo la tuhuma za kuwa mwarabu na kushiriki mauaji ya rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume.
  Kwa upande mwingine, Malecela anadaiwa kuchafuliwa wakati wa kampeni za kura za maoni jimboni mwake, kitu ambacho inadaiwa pia kiliandaliwa na baadhi ya viongozi ndani ya chama.
  Phillip Mangula ni mhanga wa siasa za mtandao. Alitupwa nje mara baada ya Kikwete kuingia madarakani na baadaye kushindiliwa wakati wa kugombea uenyekiti wa mkoa ambapo alishindwa na diwani.
  Kudondoka kwa Mangula kulifuatia Kikwete kukabidhiwa mikoba ya uenyekiti na mtangulizi wake, Benjamin Mkapa. Duru za gazeti hili zinamnukuu Kikwete akisema, “Leo hii usiku, Mangula si katibu mkuu tena wa CCM.”
  Mangula aliibuka wiki iliyopita mjini Njombe kwenye mkutano wa kampeni za rais na kunukuliwa akisema amefurahishwa na uamuzi wa Kikwete wa kufanya Njombe kuwa mkoa.
   
 2. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Watanzania tufanye uamuzi wa busara mwaka huu. ccm imesambaratika, haiwezi kuongoza nchi. Kikwete anatawala nchi kama sultani yeye na familia yake akizungukwa na walii wake wanaoibia nchi. Ndio maana hataki mabadiliko. Sasa kwa sababu nchi ya Tanzania ni yetu, na sio yake peke yake, tumwambie: HATUMTAKI!!
   
 3. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  what a shame...! huyu kikwete chama kitamfia mikononi...! anataka kuleta dynasty katika nchi hii...! RIP
   
 4. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Mungu amlinde kikwete, pengine bila ya yeye mabadiliko ya kweli yasingelitokea.... endela kuvurunda mkuu JK mpaka watanzania wenyewe waamke na kuipigania nchi yao...
   
 5. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,468
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Inawezekana labda Raisi Kikwete aliona hakuna haja ya hao wastaafu,sio mgeni wa kampeini,hizo ni mbinu za medani.Kuwashirikisha hao wastaafu kungetafsiliwa na wapiga kura kama bila kuwepo hao wastaafu Kikwete hajiamini wakati ameishatawala miaka mitano.
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,382
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  hawawezi kuisaliti katiba inayotaka awe mtu mwenye AFYA..........sasa huyu kikwete anawapa wasiwasi viongozi waliopita na hasa ukiangalia alivyodhaifu kiuongozi mpaka anadiliki kuwaambia watz kuwa akina rostam wakikamatwa na kushitakiwa i=nchio itatikisika!...........anawasamehe mafisadi !.......anawanadi walafi na walevi wa madaraka wa nchi?.................what kind of shame is this?
  HATA MIMI NINGEKUWA NDIYO WAO KAMWE NISINGETHUBUTU KUPANUA MIDOMO YANGU NAMPIGIA DEBE KIKWETE
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  tumeshawachoka hao wazee bana aaaaaaaaaaagh miaka yote wanakula wao tu Cream ya nchi hii siye tunaaendelea kukondeana tuu. sasa mkate u kinywani mwetu wadau tushindwe wenyewe kumeza CHAGUA CHADEMA!
   
 8. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda hii.
   
 9. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280

  Siyo wao tu mpaka watoto na vitukuu vyao!!!Nafikiri kama JKN angekuwa kama hawa waroho wa siku hizi, basi Makongoro kwa sasa asingekuwa na kanafasi ka uwenyekiti wa chama wa mkoa.
   
 10. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Hawa ndiyo design ya waandhishi wa habari tunaowahitaji nchi hii siyo akina Maggid!!!
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hauziki
   
 12. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Duu wazee wanaakili sana haya hata mimi ningekimbia tuu, Kazi ngumu kumuuza!!
   
 13. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  :loco::loco::loco::loco::loco:
   
 14. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #14
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 586
  Trophy Points: 280
  MAKAMBALA anammtetea kuwa baba akiwa dereva kuna ubaya gani na mtoto nae akiwa dereva!! eti huo ni wivu, labda kweli coz JEIKEI babake alikuwa kwenye system pia. MIE SIIIMOOO........!!!
   
 15. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  anatia kichefuchefu sasa huyu kikwete...
   
 16. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hivi achafuke mara ngapi? Kwani jina lake safi?
   
 17. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,477
  Likes Received: 1,441
  Trophy Points: 280
  hauziki
   
 18. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  mhhhh
   
 19. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wale wazee wana nguvu sana!! KAma kawatosa, itamghalimu!! Mark my words.
   
 20. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,186
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mwisho wa ccm ni 31 october, 2010. Familia yake ndo imebaki kumbebea mikoba make kila mtu kamkimbia. Kamuulize Sumaye.
   
Loading...