Mkapa, Mahita, na Mauaji ya Pemba. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa, Mahita, na Mauaji ya Pemba.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JokaKuu, Jan 31, 2009.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Jan 31, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,973
  Trophy Points: 280
  wandugu,

  ..i read in the news kwamba kuna wazee wa Kipemba wameamua kumshtaki Mkapa na Omar Mahita kutokana na mauaji yaliyotokea Pemba.

  ..ninavyokumbuka Raisi Mkapa alikuwa nje ya nchi mauaji yale yalipotokea. vilevile IGP Mahita, kama sijakosea, alikuwa likizo kipindi kile na kulikuwa na Acting IGP.

  ..kuna madai kwamba mauaji yale yalifanywa na askari polisi waliotokea Tanzania Bara.

  ..ZNZ kuna vikosi vya Polisi na Mkuu wa Vikosi hivyo kwa utaratibu huwa ni Mzanzibari na huteuliwa na Raisi wa Zanzibar.

  ..Raisi wa ZNZ hupigiwa wimbo wa Taifa, mizinga, na kukagua gwaride, la vikosi vya ulinzi na usalama vilivyoko ZNZ. kwa msingi huo Raisi wa ZNZ ana mamlaka fulani na vyombo vya ulinzi na usalama vilivyoko ktk nchi yake.

  ..kutokana na muhtasari huo mfupi, ninaomba michango yenu kuhusu matukio yale ya kusikitisha yaliyotokea kisiwani Pemba.

  ..ninaomba kufahamu ni nani alikuwa akikaimu nafasi ya Raisi wa Muungano na kuhusika kwake ktk mauaji yale.

  ..nani alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Muungano, na nani alikuwa waziri incharge wa vyombo vya ulinzi ZNZ, na hao walihusika vipi?

  ..je IGP Mahita alihusika au aliyekaimu nafasi yake ndiye alikuwa mhusika mkuu?

  ..je, kamanda wa vikosi vya Polisi ZNZ alihusika au hakuhusika na mauaji haya?

  NB:

  ..kuna mtu yeyote ana makala ya ripoti ya Brig.Gen.Hashim Mbita? pia naomba kufahamu wajumbe wa kamati hiyo.
   
 2. K

  Kjnne46 Member

  #2
  Jan 31, 2009
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JokaKuu, hebu soma mchango wangu wa 29/11/08 kuh "Mkapa above the law? Allegations" , ama nenda kwenye hii link utapata majibu mengi ya maswali yako juu ya mauaji hayo ya kinyama ya Wazanzibari 27!!http://www.hrw.org/tanzania

  TANZANIA: Zanzibar Election Massacres Documented
  Human Rights Watch: April 9, 2002

  Nyongeza: Rais ndiye Amiri Jeshi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ndiye anapaswa kushitakiwa kwa Crimes against Humanity na sio hao wa chini yake (eti Mahita, Kamanda wa Kituo!), labda awataje yeye kwenye utetezi wake ili "asife peke yake".

  Kibaya zaidi kwa mauaji haya ni kuwa Rais Mkapa aliwapandisha cheo hao askari waliohusika kuwaua in cold blood unarmed civilians !! Yaani hapo ndio utamwelewa vipi wakati Human Rights Watch wanasubiri adhabu wapewe hao machinjachinja yeye Mhadhamu anawapandisha chati na kuwa-promote kazini. Cha kuhuzunisha kingine ni kwamba Local Human Rights agencies, activists au TAMWA hazikufuatilia hatima ya wadhalimu hao! Wee acha tu ...
  Ngoja tusikilize maoni ya wengine.
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Jan 31, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,973
  Trophy Points: 280
  kjnne46,

  ..nakumbuka suala la kupandishwa vyeo askari. ukweli ni kwamba walipandishwa vyeo kabla ya mauaji yale.

  ..Raisi anapopandisha watumishi vyeo hutamkwa na siku vyeo hivyo vipya vitakapoanza kutumika. magazeti yaliandika kiushabiki suala hilo.

  ..unachoweza kukilaani ni kitendo cha Raisi kutowachukulia hatua za kinidhamu makamanda na askari walioshiriki ktk mauaji yale.

  ..siyo kweli kwamba Raisi peke yake ndiye anayepaswa kushtakiwa kwa crimes against humanity. kama hoja yako ingekuwa ya kweli basi kusingekuwa na mahakama ya Nuremburg kwa kuwa Hitler aliyekuwa Raisi wa Ujerumani alishafariki.

  NB:

  ..naomba kujua ushiriki wa Raisi wa JMT, Kaimu Raisi kwasababu Mkapa alikuwa nje, Raisi wa ZNZ, waziri wa mambo ya ndani, mkuu wa polisi[aliyekaimu nafasi ya mahita], kamanda wa vikosi vya polisi ZNZ, katika mauaji yale.
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hakuna kesi katika hili, kumbuka kuwa ni hao marehemu ambao walivamia kituo cha polisi na kufanikiwa kuchukua bunduki kadhaa. Polisi katika kujihami ilibidi kufyatua risasi za moto.
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Jan 31, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,973
  Trophy Points: 280
  Kibunango,

  ..chama cha CUF kupitia msemaji wao Tambwe Hiza walidai kuna jahazi lilojaa wananchi lilizamishwa kwa kupigwa mabomu na helikopta ya polisi.

  ..leo hii Tambwe Hiza amerudi CCM na kuna madaraka amepewa huko.
   
 6. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je mauji yalitokea wapi?? Mitaani au katika eneo la kituo cha polisi?? Hili swala limefanyiwa uchunguzi naamini na utafiti pia na kilichojitokeza ni kuwa Mlinzi wa sheria kavunja sheria. hilo liko wazi ikiwa hatutoingia katika hoja za mitaani za simba na yanga. Nani awajibishwe au awajibike kwa mauji hayo ndio kinachohitaji ufumbuzi.
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na alipokuwa mbeya kwenye kampeni za uchaguzi alishatamka kuwa alishiriki kupanga njama za kumwaga damu ya wapemba kwenye machafuko hayo! Na bado polisi wanamwangalia tu
   
Loading...