Mkapa: Lowassa was right! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa: Lowassa was right!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sam, Jul 13, 2006.

 1. S

  Sam JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2006
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkapa explains rescinding of City Water contract

  CORRESPONDENT
  Arumeru

  FORMER president Benjamin Mkapa has defended the dissolution of a contract between the government and City Water, saying the company failed to improve the delivery of potable water in Dar es Salaam.

  Mr. Mkapa told participants in the 17th General Meeting of the Evangelical Lutheran Church in Tanzania (ELCT) here yesterday, that even donors withheld funds after seeing City Water was not honouring the contract.

  The erstwhile president, who was presenting a paper on: Privatization and Good Neighbourliness at Tumaini University College at Makumira, said after cancellation of the contract donors resumed funding the sector.

  He explained that the then Minister for Water and Livestock Development, Mr. Edward Lowassa, took the decision to rescind the contract after realizing that they were doing shoddy work.

  ’’It happened that after dissolution of the contract and informing the donor community and the World Bank about the decision, money started pouring in for improving water supply,’’ said Mr. Mkapa.

  He told the participants that he fully supported the current government on its move to review some contracts which looked askew, saying that will raise national income.

  The former president defended privatization, explaining that it was necessary to lessen a burden on the government of supporting ailing parastatal companies.

  Touching on religious institutions, Mr. Mkapa exhorted them to be exemplary in preaching unity and civility, themes which will help in promoting peace and love in Tanzania.

  Investors in the City Water project have now taken their disagreement with the government to the International Centre for the Settlement of Investment Disputes (ICSID) for arbitration.
  [/b]
   
 2. S

  Sam JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2006
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkapa: Benki ya Dunia ilibariki City Water kutimuliwa
  Asema mikataba Tanesco na ATC haikuwa na tathmini halisi
  Na Omari Shaaban, Arumeru
  RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amesema Benki ya Dunia iliridhia uamuzi wa serikali kuvunja mkataba na kampuni ya City Water.
  Ameeleza kuwa serikali ya awamu ya tatu ilivunja mkataba na City Water, baada ya kampuni hiyo kushindwa kutekeleza makubaliano iliyowekeana na serikali ya kuboresha upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es Salaam.
  Rais mstaafu amefafanua kwamba wafadhili, ikiwemo Benki ya Dunia, waliokuwa wakiipatia fedha serikali katika kuboresha upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es Salaam, waligoma kuchangia baada ya kuona City Water haitekelezi makubaliano yake na serikali.
  Aliyasema hayo jana wakati akiwasilisha mada kuhusu ubinafsishaji na ujirani mwema, kwenye mkutano mkuu wa 17, wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini, Makumira, wilayani Arumeru.
  Akifafanua zaidi kuhusu City Water, kutokana na maswali ya wajumbe wa mkutano huo, Mkapa alisema kuwa baada ya kugundulika kwamba kampuni hiyo inakwenda kinyume na utaratibu, ilibidi Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo wakati huo, Edward Lowassa, kuingilia kati na kuzungumza nao.
  Mkapa alisema kuwa licha ya kueleweshwa zaidi na zaidi na Waziri Lowassa, ilionekana hakukuwa na maelewano mazuri na kilichofanyika ni kuvunja mkataba.
  "Na kweli baada ya kuvunja mkataba huo, na kuwaarifu wafadhili pamoja na Benki ya Dunia, fedha zikaanza kuingia tena kwa ajili ya kuendelea na utaratibu huo," alisema Rais mstaafu.
  Akizungumzia mashirika mengine kama Shirika la Ndege Tanzania (ATC) na Tanesco, Mkapa alisema serikali iliingia mikataba bila kuwa na tathmini halisi ya faida ambayo ingepata kwenye mashirika hayo.
  Alisema kuwa anaungana na serikali ya awamu ya nne katika kuhakikisha mikataba mbalimbali ambayo serikali iliingia, iwe ya mafanikio na si ya ubabaishaji.
  Kuhusu sera ya ubinafsishaji, alikumbusha kwamba lengo ni kupunguza mzigo wa serikali kuhimili shughuli za mashirika ya umma ambayo aghalabu huendeshwa kwa hasara.
  "Ubinafsishaji si itikadi ya kisiasa.ndani ya nchi yetu sijasikia chama chochote cha upinzani kwa CCM, kikipinga ubinafsishaji kisiasa.ni kwamba wanaeleza tuhuma zao na kutoridhishwa kwao kwa taratibu za ubinafsishaji, lakini hoja za ubinafsishaji ni nzito na hazipingiki," alisema Mkapa.
  Akizungumzia taasisi za kidini, alitaka ziwe vielelezo tosha vya umoja na uadilifu na ziwe mfano wa mema kwa jamii, ili kuendeleza amani na upendo katika jamii ya Tanzania.
  Katika miaka kumi ya uongozi wake, alisema, KKKT iliunga mkono juhudi za serikali za kuboresha maisha ya Watanzania na kuimarisha umoja na amani ya nchi.
  Rais Mkapa aliwataka wajumbe wa mkutano mkuu huo kuhakikisha wanaendeleza utaratibu wa kuchagua viongozi ambao watawaongoza kwa amani na upendo na kuliimarisha zaidi kanisa hilo.
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2007
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  At 11.30am on June 1 2005, three British expatriates were detained by the police in Tanzania. Cliff Stone, Michael Livermore and Roger Harrington were the senior managers at City Water, a consortium responsible for managing Dar es Salaam's water supply. After being held for several hours, the men were served with notices describing them as "undesirable immigrants" and told to leave the country.

  More
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2007
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huyu si alisema amestaafu siasa! kulikoni tena?
   
 5. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hata mimi nimeshangaa, kumbe tuendelee kumbana mpaka atuambie kwani alituibia mali zetu?
   
 6. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2007
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Huu ni ushahidi tosha kuwa huyu jamaa ni mangungo kwelikweli. Mliokuwa mnataka ushahidi, haya mangungo mwenyewe ameshakiri hapo. Kilitime kazi kwako.
   
 7. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mbona unaanza kuweweseka? Hakitoki kitu hapa!
   
 8. S

  Semanao JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2007
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 208
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Yaani ni kichekesho kabisa wakati mikataba yeye ndo alikuwa mkuu wa kaya na kuruhusu wale city water waingie mkataba. Watu walipiga kelele na hii mikataba yao mibovu lakini hakusikia, sasa baada ya kuliingizia Taifa hasara na kuwafaidisha mafisadi wenzake kama MKONO anaanza kutekea upuuzi. MKONO kwa kuvunja ule mkataba, analipwa pesa nyingi eti anatetea serikali--huu ni ujinga kabisa. I support MWANAMALUNDi kuwa huyu ndo MANGUNGO kumbe alikuwa bado hajafa.
   
 9. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2007
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tarehe za post ya sam ni 13th July 2006, 07:30 PM...!!
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,894
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Kuna haja ya kufanya kampeni kumnyamazisha huyu. Ni kumwambia kwamba kama hataki kujibi tuhuma dhidi yake ya yale aliyoyafanya akiwa Ikulu, basi Watanzania hawataki kusikia toka kwake, kae kimya kabisa.
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2007
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Vipi una matatizo ya macho?
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Oct 26, 2007
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Vipi una matatizo ya akili?
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Oct 27, 2007
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Yebo yebo,
  Hivi Mkapa alijiuzuru lini haswa hizi Siasa kiasi kwamba tumechelewa kupata majibu toka kwake..
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2007
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0


  Mkuu wangu Masatu, na Mkuu FDR,

  Tuliwaambieni kuwa huyu ni msanii aliyeenda shule, waliomnyima tuzo ile MO sio wajinga wanajua mambo yake yote,

  Juzi alipoambiwa kujibu tuhuma za wizi kasema hataki siasa, hebu niambie mkuu alichosema hapo juu si ile ile siasa aliyosema hataki?

  Labda sielewi maana ya neno usanii!
   
 15. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #15
  Oct 27, 2007
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  ..hii ndio namna sawa ya kuwatumia vongozi wastaafu wetu ambao pia ni wanazuoni...kama mkapa ,dr salim ,warioba,mzee mwinyi na wengine...wawe wanapewa mialiko ya kutoa mihadhara mara kwa mara kwenye vyuo vyetu vikuu....vyuo vingi ulaya hufanya hivyo hata mara nyingine LIVE VIDEO LECTURES ambapo viuongozi wengi hualikwa...last year COL.MUAMMAR GHADAFI Alitoa live video conferece kutoka libya kwa london school of economics..

  hii itasaidia kuwapanua vijana kifkira na kuwezesha vizazi vijavyo kusahihisha makosa ya leo na kudumisha mema yaliyopo.
   
 16. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hawataki hiyo, kwanini wafanye kazi ngumu wakati wanaweza kuchota pesa za taifa bila matatizo?

  Kuna wanasiasa wengi wasomi ambao wamestaafu lakini hawataki kabisa kurudi kushika chaki, wengine wanasema eti ni aibu.

  Ni prof. Mwandosya tu ambaye alipochoka mambo ya wanasiasa akaamua kurudi kufundisha mlimani, wengine wako radhi wawe walanguzi kuliko kuwaambia warudi vyuoni.
   
 17. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2007
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Du umenimaliza,Mbavu sina mkuu, sasa kilitime afanye nini tena??? Kilitime na Mkapa wapi na wapi???
   
 18. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2007
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  phillemon mikael
  JF Senior Expert Member

  ----------------------------------------------------------------

  "..hii ndio namna sawa ya kuwatumia vongozi wastaafu wetu ambao pia ni wanazuoni...kama mkapa"  Heshima mbele mkuu, kumtumia vizuri ni pamoja na kumuomba azungumzie abuse of power za the sitting presidents, na legal/political ramifications zake kwa taifa, hasa la kwetu, Tanzania!
   
 19. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2007
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..lile jibu halikuwa la kisanii pekee,bali pia la kijeuri!

  ..nani asiyemjua chinga kuwa ni jeuri! yaani pale anasema[in other words].."msinifuatefuate sitaongelea au kujibu maswali hayo"..
   
 20. S

  Sam JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2007
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Jamani
  Hii post ni ya zamani sana kabla hajasema kuwa amestaafu siasa. Watu mnaandika kana kwamba amesema hayo mambo baada ya kusema amestaafu siasa. Ni mjadara mzuri ukiondoa hiyo kasoro ndogo.
   
Loading...