Mkapa: Kuna mtu kanizomea?

Wandugu, nimefurahi sasa kuosoma post zenu zilizonikonga moyo, ukiacha ya Devil Novo, oops! De Novo....wote mmenena sawa!

Jamaa anaona noma huyo. Mr Clean IN, Mr. Dirtiest OUT..ole wake mchonga ange survive kama Mandela, angemkoma. Alimlaghai Nyerere akabebwa, wengine wakipigwa marungu ati wanataka kwenda ikulu kufanya nini....nakumbuka mzee wa Kiraracha alionekana kwamba anataka kwenda kufanya biashara humo. Duh! kumbe Nyerere alidanganyika!
 
but he is better kuliko wa sasa
BEING BETTER DOES NOT TAKE AWAY YOUR PROBLEMS.............. yale ya kiwira anatakiwa ajizomee mwenyewe............. uzuri ni kuwa nafsi za binadamu huwa zina kawaida ya kujishitaki pindi mtu anapofanya visivyo..............
 


Hicho sio kibali cha kutuibia wala sio kigezo cha kutukana wananchi wake ati wawivu wa kufikiri, wana wivu wa kike. Alipewa kazi hiyo afanikishe sio afanikishe na kisha kuiba. Hujui baya moja hufuta mema yote?
 
Kweli Miafrika ndivyo tulivyo, Kumbe anajua alichofanya ndo maana baada ya kukutana na wananchi na kuona hawajamzomea akajua kuwa leo siku imekuwa nzuri na kujisifia. Wenzetu UK juzi kati hapa wamemuweka Tony Blair kiti moto kuhusu vita vya Iraq, sisi tunawachekea tu hawa mabaradhuli, lkn ipo siku wataumbuka tuu hawa
 
alifanya kazi inayoonekana, hakika, na alifanya wizi wa kufuru kuliko yoyote katika HISTORIA YA IKULU ya magogoni.
kuna ufujaji alioufanya moja kwa moja kama Rais, kuna uliofanywa na wasaidizi wake, kuna ule alioruhusu ufanyike.
kifupi alitafuna asilimia kubwa ya alichokijenga, aina ya udokozi alioufanya ndio huo uliomfanya akae chimbo kwa miaka karibu mitatu sasa anaanza kuja na vikejeri, wamvue kinga akajisafishe mahakamani...
 
DHAHABU ZILIZOKAMATWA NA MREMA PALE NJIA PANDA YA ULAYA............. lamada hoteli walijiuzia shilintg ngapi........??? mgodi wa kiwira walijiuzia kiasi gani.............?????????? INAWEZEKANA ALIZIKUSANYA LAKINI AKAJIKABIDHIZA ZOTEEEEE
 
Mwisho wa Yote itabaki kuwa ni ubatili tuu na kijilisha upepo chini ya jua.

No matter how much mkapa amejilimbikizia mali but baraka haziendani na wingi wa mali mtu alizonazo! kwa mfano nasikia watoto wake ni fyatu + bangi tupu. Je akifa Mkapa hizo mali atamwachia nani?

Mkewe ndo hivyo tena tunajua ni fisadi # 2.
 
Pumzika baba, uliyowatendea waTanzania ni mengi na makubwa kwa wale wenye kuangalia mambo kwa mapana!

Sisi tunaopiga mdomo wengine hatujaifanyia chochote Tanzania zaidi ya kulalala kila kukicha!
 
- Unaona si nilisema huko nyuma kwamba kuwazomea ni silaha nzito sana tuliyonayo wananchi, hawapendi kuzomewa wanapenda kutukuzwa tu, sasa dawa ni kuyazomea tu, si huyu anasema mwenyewe fears zake kwamba anaogopa kuzomewa, sasa zomea tuu mpaka lirudishe Kiwira,

- Halafu lituambie siri ya kufungua benki yake baada ya kuwa Rais wa 10 years only tena Tanzania wakati Mwalimu miaka 25 hakufngua hata kiosk cha soda!

Respect.


FMEs!
 
Pumzika baba, uliyowatendea waTanzania ni mengi na makubwa kwa wale wenye kuangalia mambo kwa mapana!

Sisi tunaopiga mdomo wengine hatujaifanyia chochote Tanzania zaidi ya kulalala kila kukicha!
UNAJUWA MTU ANAWEZA AKAKUIBIA 10M NA UNAPOOMBA MSAADA AKAKUCHANGIA 3M TENA ZAIDI YA WENGINE......... kwa asiyefikiri ataona kasaidiwa sana na huyo mtu kumbe kimsingi anasahau kuwa effectively kaibiwa 7M............ mwaeeeeeeee we acha tuwatukuze wezi.........
 
Pumzika baba, uliyowatendea waTanzania ni mengi na makubwa kwa wale wenye kuangalia mambo kwa mapana!

Sisi tunaopiga mdomo wengine hatujaifanyia chochote Tanzania zaidi ya kulalala kila kukicha!

Hakika yalikuwa mengi na mapana:
Sisi wapigadomo kamwe hatutaweza kufanya kama hayo juu, kamwe!!!
Mkuu Kasheshe, kama kuna mapana zaidi unaweza kuongezea kwenye orodha hiyo...
 
Hakika yalikuwa mengi na mapana:


Sisi wapigadomo kamwe hatutaweza kufanya kama hayo juu, kamwe!!! Kama kuna mapana zaidi unaweza kuongezea kwenye orodha hiyo...
Huyo KASHESHE anaweza akaongeza mengine.........
 
Unajua nashangaa sana, unaposema mtu kafanya vibaya je unalinganisha na nini? Wengine mnaseama alizalisha na kuchukua vile vile, je wanaochukua bila kuzalisha hao tuwaitaje?
Ukitaka ujua uzuri na utendaji wa serekali zote za awamu nne, usimzungumzie tu Mkapa. Wewe toa data za awamu moja baada ya nyingine hapo ndipo tutaona kumbe Mkapa hakufanya kitu. Hili swala lakuongea tu bila ulinganishi ni aibu kwa wasomi. Ili kujua kama mtu amefanya vizuri unatakiwa uangalie vitu vifuatavyo
Umlinganieshe yeye na wenzake katika idara zote, kama haiwezekani uwe na standard za kulinganisha. Huwezi kusema ubatili. Pia jiulize wewe umelifanyia nini taifa lako?
Ili tuondoe ubishi, mnaosema mkapa aliboronga tuambieni ni nani aliyefanya vizuri na ni kwenye maendeo gani yenye tija

Mwacheni ampumzike
 

Mazuri aliyoyafanya yapo na ameyafanya kwa wajibu wake aliotuapia umma wa watanzania!

Kinachoongelewa hapa ni madudu alilyoyafanya! na ukifanya mazuri na wewe huyo huyo ukafanya madudu ; madudu yatafunika mazuri yote! Watu watakumbuka madudu!

Usimtetee
 
Nakubaliana nawe Kamanda. Kuzomea saaana ndio dawa yao. Nashangazwa na wanaosema amefanya mengi makubwa katika kipindi chake hivyo aachwe apumzike. Huo ni unafiki mkubwa. Alipoomba kazi hiyo kwa kuzunguka nchi nzima si ndiyo aliyoahidi kufanya nasi tukampa ajira (kura)? hivi angesema kuwa nyongeza ya kazi hiyo ntakayofanya nitawaibia na kuuza rasilimali zenu kwa bei ya kutupa nani angempa ajira hiyo (Uraisi)?
Tusipotoshane, BM ametusaliti big time.
 
C'mon, why we beating around the bush? Simply name 5 in contrast to above Bubu's list so we can all figure their order of magnitude to this nation's pride or rather plight!!
 
Umesahau kwamba yeye huyu bwana ni mR Clean? Amechagua kwenda Kilolo kijijini kwa makusudi, unajuaje, labda wanyalukolo kule wanadhani bado nkapa anatawala?

BWM huwa anapenda kuzungumza akiwa vijijini; mnakumbuka hata mara ya kwanza kujaribu kujibu tuhuma alizumgumza akiwa kijijini kwao Lupaso!! Watu wa vijijini wana busara ya woga na kama haamini ajaribu kuhutubia Kawe wilaya ya Kinondoni tuone kama atapokelewa kwa kishindo!!
 
Kasubiri mijadala imefungwa bungeni ndo kajitokeza na watz tumesahau uchafu wake
Inchi hii bila kuchi....na HAITABADILIKA!!!!!!!
 

Huyu mzee ajinyamazie maana anazidi kutonesha vidonda alivyowasababishia watanzania wakati wa uongozi wake.
Mi naona ni bora aendelee na matangazo yake ya HIV anayotangaza kwenye TV.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…