MKAPA- CHUKI, WIVU, FITNA, UDUNI na uvivu wa kufikiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MKAPA- CHUKI, WIVU, FITNA, UDUNI na uvivu wa kufikiri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bongolander, Feb 1, 2009.

 1. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ndugu wana JF
  Toka rais wetu alipomaliza muda wake kuna manno mengi ambayo amekuwa akiyasema kuhusu shutuma zinazoelekezwa kwake au kwa viongozi waliokuwa kwenye serikali yake. Alipokuwa kule Ntwara aliwahi kusema yanayosemwa na vyombo vya habari ni uongo, ni wivu tu umewajaa. Hivi karibuni hako Iringa ameruda maneno kama hayo na mengi ambayo amekuwa akiyasema kuwa hakuna baya alilofanya ila ni wivu tu ambao unatokana na uvivu wetu wa kufikiri.
  Kama kuna anayejua msingi wa maneno ya Mkapa WIVU, CHUKI, FITNA na ujinga wa kufikiri? Kwanini hakuyashughulikia alipokuwa madarakani na sasa kulalamika kila siku kuhusu wivu, wivu wivu. Au haya yameibuka baada ya JK kuingia madarakani?? Ni nani hasa anayemuonea wivu na kwa nini amuonee wivu, na kwa nini yeye Ben aonewe wivu na sio JK, au Mbowe au Bakhressa??? Kila nikifikiri sielewi maana hasa ya Mzee Mkapa, na kila nikijaribu kuondoa uvivu wa kufikiri naishia njia panda.
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  .....Hapo ndio utajibiwa ni uvivu wako wa kufikiri kama watanzania wengi tunavyoambiwa na BWM tu wavivu sana kufikiria,nafikiria JK pekee anaweza jibu swali hili la wivu kwa BenM
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Guilty conscious
   
 4. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Toka lini viongozi wetu wanajua wanachokisema?

  Wengi wao wamelala usingizi mzito lakini kwasababu sasa hivi media imeanza kutoa maovu yao, ndio wanaanza kuja na sababu zisizo na kichwa wala miguu.

  Angalia wanavyotupiana mpira wakati kuna issue. Hakuna anayejiamini kushika nafasi yake na kuelezea kilichotokea. Utasikia kuwa tunamsubiri raisi au waziri mkuu utafikiri wao ni MABOGA huko kwenye kazi zao.
   
 5. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu wenzangu Waswahili wasemaa; Mfa maji heshi kutapatapa au Mfa maji hushika maji, sasa weka kwenye imejineshen zako kwamba ndio unazama unachokiona ni maji kilichokuzunguka ni maji na uajaribu kuyashika na kuyaomba yakusaidie usende chini yaani usizame, si sheshe hilo???? Sheshe hilo ndilo linalomkabili B W Mkapa, ikiwa sisi ni wavivu wa kufikiri , hakika yeye ni mwepsi wa kufikiri na kujua kuwa Amechambia Mgomba Amebaki na Mavi yake. Mkapa kanasa kwenye ndoana wenye uzoefu wa kuvua mnafahamu apewe mshipi afurukute nao akichoka anavutwa kilaini. kwa mneno ya mjini kama kumsukuma mlevi.Lets hold the fishing line and dont let Mkapa off the HOOK.
   
 6. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Maneno hayo ya Mkapa ni ya kawaida kwa viongozi wetu wa CCM katika Tanzania. Mkapa anaona haya kukubali kwamba ni mwizi. Pia anaona haya kukubali kwamba alikiuka na kuivunja katiba alipokuwa pale Ikulu, lakini siku ya kifo cha nyani miti yote huteleza. Mkapa anajaribu kushika mti huu na ule lakini wakati wa kutiwa hatiani yeye na kundi lake utafika.

  Mnakumbuka hata katika suala la EPA lilipoanza jinsi CCM walivyokuwa mstari wa mbele kusema kwamba ni uwongo hakuna wizi huo?.

  Ushahidi wa wizi na uchafu wa Mkapa uko wazi hilo halina ubishi, ni bora angekuwa mstaarabu kama waziri mkuu Pinda. Mkapa akubali kosa lake, arudishe mali alizoiiba huenda Watanzania tungefikiria kumsamehe lakini vinginevyo kila asemalo ni sawa na kutia petrol katika moto unaowaka.
   
 7. share

  share JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,293
  Likes Received: 2,277
  Trophy Points: 280
  Watanzania wameweka wazi tuhuma dhidi ya Mkapa na kuzichambua kwa kina. Imefikia mahali sasa tunatarajia hoja hii iibuke bungeni ili Mkapa aondolewe kinga. Wengine wameenda mbali na kudai kuwa Mkapa hana kinga kwa makosa aliyoyafanya binafsi kama Mkapa. Wenye mlengo huu wa mawazo wanajipanga kufungua kesi dhidi ya Mkapa wakati wowote. Mkapa hajawahi (hata siku moja!) kujibu hoja hizo. Amebaki tu kutoa vigezo rahisi vya WIVU - hoja mufilisi. Nani hapa mvivu wa kufikiri! Mkapa au Watanzania? Akae kimya, anazidi kuamsha kwa kasi hasira za kumshughulikia kwa uvivu wake wa kufikiri.
   
 8. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  JUJUMAN last phrase yako imenifurahisha sanaaa ''Lets hold the fishing line and dont let Mkapa off the HOOK'' Ha ha ha utterly, he will notget out of the hook...
   
 9. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama viongoz wetu wangekuwa kama pinda au warioba baadhi ya matatizo yetu yangekuwa yamepungua. pinda kaona kakosea kaomba samahan. warioba katuhumiwa kulikoroga pahala akatoa maelezo ambayo yanaonesha yeye kama yeye hakulikoroga pahala (kitu kama hicho)

  sasa aliyekuwa rais wetu ambaye hana CHUKI, WIVU, FITNA na wala asiye na UDUNI na uvivu wa kufikiri anaambiwa wew ulipokuwa rais ulifanya hiki na hiki na kile ambacho hakikustahili na yeye anajibu nyie mnaosema hivyo mna CHUKI binafsi, WIVU, FITNA na UDUNI na uvivu wa kufikiri

  wao. ni kweli? mi binafs nasoma kwenye vyombo vya habar mapungufu yake yale. hata suala la warioba na mwananchi gold nalo nalisoma kwenye vyombo vya habar na hata maelezo aliyotoa niliyaona kwenye vyombo vya habar.

  lakin warioba katoa maelezo ambayo yanaonyesha angalau hakuharibu kias hicho. aliyekuwa presidaa bwm anakomaa kudai vyombo vya habar na wanaomshutumu kuwa wana CHUKI binafsi, WIVU, FITNA na UDUNI na uvivu wa kufikiri.

  mbona mwenzie warioba kaongea? au ndo yaleyale ya mkubwa au rais hakosei? kwamba rais anakuwa kama mungu? au malaika?

  asikuongopee mtu msomaji wa JF, hii afrika imefika hapa ilipo kwasababu ya viongoz wake wabovu ambao anyway wanapatkana kutoka miongon mwetu
  wasipokuwa na ubovu wa kupenda kujichukulia kila wakitamanicho watakuwa na ubovu wakutojua matatizo ya jamii zao na jins ya kuyakabili au vyote

  au afuate njia ya pinda - aombe samahan. lakin hii iambatane na kurudisha alichochukua isivyostahili

  afanye kama warioba. jamii inakutuhumu nawe unaijibu. mwenye ushahid aulete. kiongoz lazima uwe hivyo ukiwa madarakan au ukitoka. sasa huyu presidaa mstaaf mbona kimya? alikuwa clean kwel? mbona anauficha uclean? watu tumezoea kuficha uchafu

  akishtumiwa na akakaa kimya mtz wa kawaida kama mim nimweleweje? mim sio sampuli ya watz waoona ni halali kiongoz kujichukulia chochote atakacho etc
   
 10. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mtamsoma siku atakapoiacha dunia wakuu ila kwa sasa wengi wetu ni sikio la kufa halisikii dawa
   
 11. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Vipi Balali hukumsikia alivyoongea na waandishi wa habari kuhusu moyo wake ulivyo mweupe? Mzee wa vijisenti je? JK aliyetwambia ili mtera ijae inahitaji Elnino 3 au kwamba Richmond haikuiingizia serikali hasara yoyote kwani hawakulipwa ktu. RA HUKUMSIKIA AKISEMA YEYE SI FISADI, Karamagi, EL si wote wanadai ni watu safi? Warioba je?

  Sasa kwa nini tushangae hii ya Mkapa kama yeye anaamini ni safi aruhusu kwa hiyari yake kinga iondolewe apelekwe mahakamani akishanekana safi anarudishiwa kinga yake.

  Mwanawasa amewahi kujiuzulu alivyokua makamu wa raisi ili kupisha uchunguzi uliomtuhumu kujihusisha na biashara ya amadawa ya kulevya.
   
 12. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Mkuu uzuri ni kwamba yeyehakanushi yote yanayosemwa dhidi yake isipokuwa anapiga vijembe, kushutumu wivu, fitna, udini na siasa za chuki. Ana uwezo mkubwa tu wa kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kusema mimi sio fisadi, sikujiuzia Kiwira, sikufanya biashara nikiwa ikulu, na sikuua watu zanzibar. Na aseme n nani anayemuonea wivu, kwa nini, na kwa kipi alichonacho ambacho wengine wasiionacho wanamuonea wivu. Na aseme kama hayo yameanza wakati wa utawala wa JK. Itakuwa vizuri sana akituwekea msingi kama huo, maana JK nae naweza kufanya biashara na kuja na jibu kama la Mkapa ni wivu, chuki, udini na fitna.
   
 13. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #13
  Feb 4, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Sounds great!

  People are keeping on blaming Mkapa, we have new preds, cabinet, we have mahakama, DPP, na jela!

  Kwa maana nyingine anasema, mbona hamumkamati??? who has problem here??

  Is it not for political gains of the current government to use Mkapa's name , just to hide dirty things that are going on now??? Oh yes, if are cleans, why dirty Mkapa is freeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!
   
Loading...