Siku hizi watu hawaambiliki na chimbuko kubwa la matatizo ni ujuaji mwingi, kila mtu anaamini kuwa anajua, na hili jambo ni la hatari.
Wengine hawakuwapo wakati nchi hii inapata uhuru na hata wakati uhuru unapiganiwa, wao waliikuta nchi ikiwa huru.
Lakini utakuta wanasimulia mambo mengi ambayo hata hawayajui na hayana msingi wowote, alisema Mkapa.
Pamoja na wengi kuona kuwa Mzee Makapa ameanza kuchoka kifikra, kauli hii hapa juu ni ya kweli na ndiyo sababu kubwa ya kukwamisha maendeleo ya nchi ambayo pia inatoa fursa kwa wachache kutumia mwanya huo kujinufaisha, tukubali tusikubali bila kubadiliaka maendeleo ni safari ambayo bado ni ndefu sana kwa Tanzania.