Mkapa arusha kombora; Awashutumu viongozi wa dini, Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa arusha kombora; Awashutumu viongozi wa dini, Serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 20, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMATANO, SEPTEMBA 19, 2012 08:49 NA DEBORA SANJA, DODOMA

  *Awashutumu viongozi wa dini, Serikali
  *Asema viongozi wastaafu hawathaminiwi
  RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, ameibuka na kusema kuwa, hivi sasa baadhi ya viongozi wa Serikali na viongozi wa dini, wamekuwa hawawathamini na kuwajali viongozi wastaafu.

  Amesema hali hiyo imekuwa ikitafsiriwa na kuonekana kuwa, viongozi hao hawana jipya mbele ya jamii.

  Rais Mkapa alitoa kauli hiyo mjini hapa jana alipokuwa akihutubia katika ibada maalumu ya kumbukumbu ya miaka 40 ya uaskofu wa Askofu Mstaafu Mathias Isuja wa Jimbo Katoliki Dodoma.

  Mkapa alisema, kuna dhana iliyojengeka, kuwa viongozi waliostaafu wanakuwa hawana jipya na hawathaminiwi tena kutokana na kustaafu kwao kwa mujibu wa sheria.

  “Hivi sasa imezuka tabia kwa baadhi ya viongozi wa nchi na makanisa kuona kuwa mtu akistaafu basi anakosa hekima.

  “Mtu akistaafu anaonekana kuwa ni mufilisi tu asiye na kitu na nataka mfahamu kuwa, kustaafu siyo kuchoka na wala michango ya wastaafu siyo mibovu bali inatakiwa kuangaliwa,’’ alisema Rais mstaafu Mkapa.

  Aidha, alisema nchi imekuwa ikikumbwa na matatizo kutokana na ubishi na ujuaji wa wananchi hali inayosababisha nchi isipige hatua ipasavyo katika maendeleo.

  “Siku hizi watu hawaambiliki na chimbuko kubwa la matatizo ni ujuaji mwingi, kila mtu anaamini kuwa anajua, na hili jambo ni la hatari.

  “Wengine hawakuwapo wakati nchi hii inapata uhuru na hata wakati uhuru unapiganiwa, wao waliikuta nchi ikiwa huru.

  “Lakini utakuta wanasimulia mambo mengi ambayo hata hawayajui na hayana msingi wowote,” alisema Mkapa.

  Aliwataka pia viongozi kujenga tabia ya kujifunza bila kuchoka na kwamba viongozi lazima wawe mfano kwa kupenda kusoma.

  Akimzungumzia Askofu Isuja, Mkapa alisema Isuja alikuwa ni kiunganishi cha wananchi wa Dodoma pamoja na Tanzania, kwani alipenda kufanya kazi zake kwa uwazi na ukweli wakati wote. Mimi namfananisha Askofu Isuja na mtumishi mwema katika shamba la bwana,” alisema.

  Kwa upande wake, Askofu Isuja aliwashukuru maaskofu wote, mapadre, watawa, waumini wa Kanisa Katoliki wakiwamo wa Jimbo la Dodoma na Serikali kwa kipindi chote walichompa ushirikiano wakati akitumikia Jimbo la Dodoma.

  Askofu Isuja pia alihimiza amani nchini na kuwataka Watanzania kuwa na upendo bila kujali ubaguzi wowote miongoni mwao.

  Mbali na viongozi hao, katika ibada hiyo alikuwapo pia Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kardinali Pengo ambaye ndiye aliyeongoza ibada.

  Walikuwapo pia viongozi mbalimbali wa Kanisa Katoliki nchini, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.

   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mkapa anataka wamjali kwa lipi? Siye yeye aliyefuga na kukuza ufisadi na kusaidia kumweka Kikwete mamlakani?
  Sasa kama hujaacha legacy nzuri tukuthamini kwa lipi?
   
 3. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,647
  Likes Received: 5,237
  Trophy Points: 280
  Jamaa kadiri siku zinavyokimbia kuelekea 2015 ndo'anavyozidi kuchangayikiwa na kutokwa "POVU".
  Kwa hiyo alitaka walioipatia nchi uhuru ndo'waopekee wazungumzie kuhusu uhuru, sasa nini maana ya kua na historia? Na anataka watakaosimulia hiyo histora wawe wakina nani?
  Mbona linapokuja swalia la MGODI KIWILA NA MCHUCHUMA, hatoi hayo maneno yake....!
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,404
  Likes Received: 81,431
  Trophy Points: 280
  Huyu fisadi Mkapa alipokuwa madarakani aliwathamini wastaafu au alikuwa busy kuwaibia Watanzania? Mbona alishindwa kuwalipa wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

   
 5. Foum Jnr

  Foum Jnr JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 272
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  maneno yake yanaonyesha mambo asiokubaliana nayo yeye:-
  a) Kuupinga uhuru wa wananchi wa kushiriki katika maamuzi yanayowahusu. Unaposema kila mtu mjuaji unaashiria masuala ya ujuzi ni ya elite maalum, wengine hawana maana. kauli potufu and undemocratic kama ulivyokuwa utawala wake wa wataalamu wengi waliowazuia wananchi kujua ili kuiifisidi nchi kwa muongozo wa matumbo yao.

  b) Kama kutowajali pensioners, yeye kachangia pa kubwa katika kupuuza malalamiko ya pensioners hata wale wa EAC iliyovunjwa, jee aliwasaidia nini alipokuwa madarakani? Kama ni kwa viongozi waliomtangulia basi na ajiulize yeye mwenyewe perception yake kwa mzee mwinyi wakati ule, ajitathmini zaidi hii culture ieanza wapi kama si kwake?

  c) sioni kama ana-lecture ya kuwapa watanzania kwa sasa, credibility yake sio nzuri kutokana na history ya utawala wake, nilishangaa juzi Mh Sumae akikemea jeshi la polisi kwa kumuua Mwagosi wakakti alipokuwa yeye mtawala na wenzake watu zaidi ya kumi waliuliwa na jeshi la polisi baada ya ku-protest election result, hizi ndio legacy zao ambazo wametuachia watanzania kama mfumo wa kutawaliwa, sasa unalalalamika nini?

  Wakati wa kuhadaa wananchi umepitwa, watulie tu wakalime vijijini na kuwa neutral ili kujenga heshima zao upya.
   
 6. b

  bagwell Senior Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hana lolote yeye ndio aliekua kinara wa kutowajali wastaafu na badala yake alihalalisha rushwa kua maji ya kunywa...ati wamjali kwa lipi wamjali?
   
 7. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkapa ameishiwa point maana yeye alikuwa rais ndie aliyetupatia huu ulengelenge tulio nao na udhaifu unaotusumbua na kututumbukiza kwenye janga la umaskini kiasi kama hiki. alijua kabisa ndio maana ni bora kutumia uongozi huku ikijua siku moja utakuwa mitaani kama yeye leo hayuko kwenye system leo hii anaona madudu lakini alipokuwa kwenye system hakuona hayo yote.
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Katika watu wa kunyonga na kutupa baharini ni Mkapa na aliyekuwa AG wake, Chenge. Mikataba yote MIBOVU, sheria ya sasa ya TAKUKURU na ujinga wa kujiuzia nyumba za serikali kaufanya Mkapa. Leo hii anasimama kwenye mimbari ya makanisa anataka aombwe ushauri upi? Kapata akili mpya wapi?
   
 9. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hatuna haja ya kuwakumbuka viongozi mafisadi na wezi, waliotuletea hasara katika nchi yetu. Ajiulize mbona Nyerere anakumbukwa na alikuwa anaheshimiwa? hana jipya! Kauza nchi huyu na kuuza madini na mikataba ya ajabu ambayo sana ilaleta shida!
   
 10. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni marais wetu kuwa wenyeviti wa vyama vyao, wanapokuwa madarakani wanasimamia vyote, serikali ikigaribu hakuna wa kumraumu, sasa leo atakuja na jipya lipi watu wakamsikiliza? hana mvuto kama Late Mwl Nyerere, kichwa kilikuwa kizuri na alikuwa na ushawishi kubwa sana, alitete hoja zake viziri na zikakubarika
   
 11. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,731
  Likes Received: 1,443
  Trophy Points: 280
  They should EARN the respect they want.

  Otherwise let their kids and family just give the normal and traditional and social respects. But if he want the respect of the public, Mkapa and all leaders are herein categorically advised to work for it.

  Unless Bw. Mkapa analalamikia watu wake wa karibu kutomjali na kumheshimu. Kama ndivyo basi tutamshauri JK aunde tume kuchunguza na pia Bunge liunde Kamati ili kupitia mapendekezo ya hiyo Tume kabla ya uwasilishaji wa siri kwa Mkapa.
   
 12. D

  Deo JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,190
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Akumbuke aliyowafanyia wale wazee wetu wastaafu wa jumuia ya Afrika mashariki.

  Michango gani yeye anayo? Wizi, ufisadi au kusema uongo kuwa fulani si mwanafamilia?

  Kaa na aibu yako mzee, usiamshe hasira za watu
   
 13. N

  Njaare JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Ha ha haaaaaa! Huyu Mzee kasahau ule msemo wa "Fainali uzeeni".

  Akumbuke pia pia kuwa mwalimu Nyerere alitufundisha kuwa Heshma ya mtu itokane na huduma yake kwa jamii. Kama huduma yako haikuwa muafaka watu watakuheshimu ukiwa madarakani kwa sababu umeshika mpini. Ukiachia madaraka utaonekana kama takataka.

  Ushauri wa bure kwa walioshikilia madaraka nikuwa wakumbuke kuwa fainali ni uzeeni. Kama ulikuwa huna busara ukiwa kazini hatutategemea uwe na hekima ukistaafu.
   
 14. K

  Kibagata JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 773
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Mwizi tu huyo.
   
 15. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hatumpi nafasi asituletee tene uabe wake wa kimacjinga, ukiona mtu anajialika kwenye sherehe ujue kaishiwa
   
 16. A

  Ame JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Nadhani roho aliyobeba huyu binadamu na mimi ni contrary kama yeye ana holly basi mm nipo opposite ya roho aliyowanayo. Kila mara nikimsikiliza ananikwaza kabisa...yeye ndiye mjuaji kama aliweza kuita raia wenzake wanwivu wa kike what kind of person is he? Kama yeye alishindwa kuheshimu raia nani atamheshimu yeye? Kila action ina reaction yeye anapata reaction ya action zake.
   
 17. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Siku hizi watu hawaambiliki na chimbuko kubwa la matatizo ni ujuaji mwingi, kila mtu anaamini kuwa anajua, na hili jambo ni la hatari.

  "Wengine hawakuwapo wakati nchi hii inapata uhuru na hata wakati uhuru unapiganiwa, wao waliikuta nchi ikiwa huru.

  "Lakini utakuta wanasimulia mambo mengi ambayo hata hawayajui na hayana msingi wowote," alisema Mkapa.

  Pamoja na wengi kuona kuwa Mzee Makapa ameanza kuchoka kifikra, kauli hii hapa juu ni ya kweli na ndiyo sababu kubwa ya kukwamisha maendeleo ya nchi ambayo pia inatoa fursa kwa wachache kutumia mwanya huo kujinufaisha, tukubali tusikubali bila kubadiliaka maendeleo ni safari ambayo bado ni ndefu sana kwa Tanzania.
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Ndo maana huwa hapendi kuongea hasa na vyombo vya habari kwa hofu ya kuwa "misquoted", inawezekana hata jambo lenyewe halikuwa kama lilivyoletwa hapa!!!!
   
 19. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkapa hana moral authority ya kuwaasa watanzania jambo lolote. Dhambi yake ya kugawa bure mashirika ya umma kwa kisingizio cha ubinafsishaji bado hatujasahau. Mikataba mibovu iliyoingiwa wakati wa utawala wake kwenye sekta ya madini bado ni maumivu makali kwa watanzania. Na pia asifikiri kuwa sisi hatujui kuwa yeye ndie muasisi wa upigaji mkubwa (ufisadi) na kupitia kwake pesa za EPA zilikwapuliwa kusaidia CCM 2005. Mkapa hana budi kwa sasa kukaa kimya na kupumzika na ashukuru JK kaamua 'kumuacha apumzike'.
   
 20. b

  bahatil mselle Member

  #20
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hana jipya huyo. Laana ya ufisadi aliofanya mauaji ya Wapemba katika utawala wake imeanza kumtafuna na ameanza kuchanganyikiwa. Tutasikia mengi zaidi kadiri atakavyozidi kuchanganyikiwa.
  AKUMBUKE MALIPO NI HAPAHAPA DUNIANI.
   
Loading...