Mkapa ampiku Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa ampiku Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Sep 20, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkapa ampiku Kikwete
  • Utawala wake wauzidi wa Kikwete kiuchumi

  na Sauli Giliard  PAMOJA na kukabiliwa na tuhuma mbalimbali za ubadhirifu, huku baadhi ya watu wakitaka Rais mstaafu Benjamin Mkapa, aondolewe kinga ya kutoshitakiwa ili apandishwe mahakamani kwa kutumia madaraka yake vibaya, kiongozi huyo mstaafu amezidi kupata umaarufu kutokana na kazi aliyoifanya katika utawala wake.
  Mkapa kwa kipindi kirefu amekuwa kimya licha ya kukabiliwa na tuhuma hizo ambazo wakati fulani zilitikisa Bunge na kuzusha mgawanyiko mkubwa miongoni mwa wabunge ambao baadhi yao walikuwa wakimtetea asihusishwe na ufisadi wengine wakitaka awajibishwe.
  Taarifa kuhusu mfumuko wa bei na masuala ya uchumi iliyotolewa na Idara ya Takwimu ya Taifa (NBS) wiki hii, ilionyesha kuwa taifa hivi sasa limo katika wakati mgumu kiuchumi, ambapo mfumuko wa bei umefikia asilimia 12.1.
  Kiwango hicho cha tarakimu mbili (double digits) ni kikubwa zaidi kulinganisha na tarakimu moja iliyodumu kwa miaka 10 chini ya utawala wa Mkapa, ambaye inaaminika alikuwa kiongozi bora katika kusimamia masuala ya uchumi.
  Kiongozi huyo mstaafu ambaye inadaiwa pia alikuwa akitumia ubabe (udikteta) uliokuwa ukilalamikiwa na baadhi ya watu katika utekelezaji wa mambo nyeti yenye kugusa ustawi wa nchi, hivi sasa amejizolea umaarufu kutokana na uamuzi huo yanaoonekana kuwa mhimili mzuri wa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya taifa.
  Awamu ya Tatu inaonekana kuwa bora zaidi kiuchumi kulinganisha na Awamu ya Nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete, ambaye anakabiliwa na wakati mgumu wa kuirudisha nchi katika uchumi imara na kuzuia mfumuko wa bei.
  Kauli ya Rais Kikwete kuwa Mkapa alimkabidhi nchi ikiwa katika hali nzuri kiuchumi, inazidi kushibisha uimara wa awamu ya Mkapa katika sekta ya uchumi, lakini pia inampa wakati mgumu Rais Kikwete kutimiza ahadi yake ya kuendeleza juhudi hizo kwa lengo la kuwaletea maisha bora Watanzania kama kaulimbiu yake ya “Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana”, wakati akiwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu mwaka 2005.
  Katika ripoti ya utafiti iliyotolewa mwaka jana na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Redet), ilibainisha kuwa kiutendaji Mkapa alifanikiwa zaidi kuliko utawala wa Rais Kikwete.
  Wanataaluma hao walibainisha kuwa Mkapa aliweza kudhibiti mfumuko wa bei na kupunguza malalamiko ya wananchi dhidi ya serikali yake, tofauti na serikali ya sasa ambayo inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwamo ya kuongezeka kwa mfumuko wa bei unaosababisha hali ngumu ya maisha kwa ujumla.
  Mkapa ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa kimya dhidi ya tuhuma zinazoelekezwa kwake, ikiwamo ya familia yake kumiliki mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, ambao unadaiwa ulimilikishwa kwa hila na bei ya kutupa.
  Kiongozi huyo pia amekuwa akishutumiwa kuwa hakuwa akitoa uhuru kwa vyombo vya habari pamoja na kutumia vyombo vya dola kuwazima wapinzani.
  Wakati shutuma hizo zikiendelea kuligawa taifa juu ya hatua za kuchukuliwa dhidi ya kiongozi mstaafu huyo, Rais Kikwete alibainisha kuwa si busara kuendelea kumuandama, bali anapaswa aachwe apumzike, kwa kuwa aliifanyia nchi mambo makubwa na kulijengea taifa heshima.
  Joto la kutaka kuwajibishwa kwa kiongozi huyo lilizidi kushika kasi pale serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kulitangazia Bunge la Bajeti mwaka huu kuwa imeamua kuurudisha mgodi huo katika mikono yake, kwa lengo la kumtafuta mwekezaji mwingine kuuendeleza.
  Kauli ya Pinda ilionekana kupingwa vikali na baadhi ya wabunge, kwa madai kuwa serikali haipaswi kuwalea viongozi wasio na uadilifu, kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaendeleza kizazi cha ufisadi.
  Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe (CCM), aliweka bayana kuwa kiongozi huyo mstaafu hapaswi kutetewa bungeni, na yeyote mwenye nia ya kufanya hivyo ni vema akaenda mahakamani.
  Ulinganisho wa baadhi ya wachambuzi wa masuala ya uchumi kuhusu utawala wa awamu hizo mbili, yanazidi kumuweka Mkapa katika utendaji bora zaidi, ambapo katika utawala wake kulikuwa na matukio 18 ya watu kudai uwajibikaji kwa maandamano na migomo, wakati kwa kipindi cha miaka miwili ya mwanzo ya uongozi wa Rais Kikwete, yametokea matukio 34.
  Hata hivyo, Dk. Bernadette Killian, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Shule ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano (SJMC) ya UDSM na mtafiti wa Redet, aliwahi kubashiri kuwa, huenda kipindi cha miaka miwili (ukiwamo mwaka huu), mengi yakajitokeza zaidi kutokana na mabadiliko ya harakaharaka yaliyojionyesha kwa kipindi cha mwanzo, ambacho Rais Kikwete alikuwa ametawala.
  “Na kwa vile kuna kipindi kilichobaki cha takriban miaka miwili na nusu hadi hapo 2010, huenda matukio hayo yakaongezeka zaidi,” alisema Dk. Killian.
  Licha ya wataalamu wa nchi tajiri kutoa matumaini ya kuwapo dalili za uchumi wa dunia kurudi katika hali yake ya kawaida kutokana na hatua zilizochukuliwa huku bei ya mafuta katika soko ikiwa imetulia kwa kiasi nchini, mfumuko unazidi kukua kwa kasi, kwani kumbukumbu zinaonyesha, Julai, mwaka huu, mfumuko ulifikia asilimia 10.9.
  Pamoja na NBS kutoa sababu za msingi za mfumko huo ambao umepanda kwa asilimia 1.2, ikilinganishwa na mwezi Julai, ikiwamo ongezeko la gharama za chakula, bado wachambuzi wa mambo wameonyesha kuwa kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya maisha bora inaonekana kuwa ni doa kwake na imepunguza idadi ya watu waliokuwa na imani naye.
  Mbali na chakula, NBS ilibainisha kwamba, kwa wastani, mfumuko wa bei kwa mwaka jana ulikuwa ni asilimia 10.3, sawa na asilimia 6.7.
  Mambo mengine kwa mujibu wa NBS ambayo pamoja na chakula yamechangia mfumuko huo kufikia kiwango kilichoshtua, ni gharama za mafuta ya taa, dizeli na nauli.
  “Kuongezeka kwa mfumuko kulichangiwa zaidi na kupanda kwa bei ya vyakula kutoka asilimia 16.9 kwa mwaka ulioishia Julai na kufikia asilimia 18.9 Agosti, 2009,” ilisomeka tovuti ya NBS.
  Baadhi ya watu waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili wameonyesha kutohusisha hali ya sasa ya uchumi wa nchi na ule wa dunia, bali moja kwa moja wanalinganisha ufanisi wa Rais Kikwete katika kuunyanyua uchumi na ule wa Rais mstaafu Mkapa.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ni miongoni mwa wanasiasa wachache ambaye kwa muda mrefu amekuwa akimsifia Mkapa kwa jitihada zake za kudhibiti mfumuko wa bei na kukuza uchumi, tofauti na utawala wa sasa ambao kwa kiasi kikubwa umeyumba kiuchumi huku maisha ya wananchi yakizidi kuwa magumu siku hadi siku.
  Baada ya kuona hali ya uchumi haiendi vema, mwaka juzi, Profesa Lipumba, alipokutana na lililokuwa Jukwaa la Wahariri, alimtaka Rais Kikwete kuitisha mjadala wa kitaifa ukiwahusisha wadau muhimu wa maendeleo nchini ili kupata mustakabali mzuri kwa uchumi wa nchi.
  Mwaka 2007, takriban miaka miwili baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani, Uchunguzi wa Bajeti ya Kaya (UBK) ulibainisha kwamba umaskini umepungua kidogo kutoka asilimia 35.7 mwaka 2001 hadi asilimia 33.3 kwa mwaka huo.
  Mmoja wa wachambuzi wa mambo ya uchumi ambaye hakutaka jina lake litokee gazetini, alieleza kuwa ni dhahiri uchumi umezorota kwa kiasi kikubwa na kutolea mfano bei ya bidhaa zilizokuwa zinauzwa mwaka 2005, kupanda bei maradufu.
  Akitolea mfano, mchambuzi huyo alisema, mwaka 2005, soda ilikuwa ni sh 300 hadi sh 350, na sasa imepanda na kufika sh 400 hadi sh 600, sawa na maji ya kunywa, huku mchele, unga na maharage vikipaa kwa kasi ya kutisha.
  Licha ya kukiri hali ya sasa ya uchumi, alibainisha kuwa, kuna tatizo kubwa la kiuongozi katika Awamu ya Nne na linatakiwa kufanyiwa kazi kubwa ili kulinusuru taifa katika mparaganyiko huu wa uchumi.
  Hata hivyo, wiki hii Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Emmanuel ole Naiko, alipokuwa akizindua ripoti ya Uwekezaji Duniani katika Ofisi za Umoja wa Mataifa, jijini Dar es Salaam, alisema kuna baadhi ya maamuzi yaliyokubaliwa mwaka 1999 na sasa baadhi ya idara za serikali zimepuuzia na athari zake zimekwishaanza kuonekana.
  Ole Naiko alisema, kutowajibika huko kwa baadhi ya idara za serikali kumewakwaza wawekezaji wa kigeni na kusababisha mtaji utokao nje kupungua. Moja ya idara za serikali zinazoleta kikwazo ni pamoja na Mamlaka ya Mapato (TRA), ambayo imetajwa kuwa inalalamikiwa na wawekezaji kwa kiasi kikubwa, ikifuatiwa na sera za ushuru wa forodha na sheria mbaya za uwekezaji katika sekta ya utalii.


  [​IMG]
  juu[​IMG]
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  hilo halihitaji tahasisi kulijua, maisha yako ya kawaida ya kila cku yanakuonyesha hilo, hali ni ngumu mno huko kwa wenye kulala hoi
   
 3. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  WENYE KULALA HOI? waache wateketee kivyao kwani wameyataka wao wenyewe kwa kuvishwa vi-T Shirt vya njano[​IMG]
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ni kwa nini EPA, Meremeta, Tangold, n.k. hatukuzijua wakati wa mkapa??? Pamoja na matatizo ya JK, lakini uhuru wa habari umekua na umetuwezesha kujua mabaya ya Mmakonde nkapa.
   
 5. a

  alibaba Senior Member

  #5
  Sep 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huo ndio ukweli Magezi hizi stori ndefu za awamu ya tatu,na ubora wake ndio tulizomtuma Njomba Nkapa atuletee na ndio mana tulimlipa vizuri. Jamaa akageuka Kibaka hata kumwita Jambazi naona nitampa Hadhi, bado mnakaa na kumsifusifu,mara ngapi iwekwe wazi kuwa MWIZI ni MWIZI tu!!! na astahili yake ni KEKO end of story.
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu unachosema ni kweli. Lakini tukijiuliza what does uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa vyombo vya habari mean to mwananchi wa mjini na kijijini ambaye hata radio hana, gazeti hawezi kununua, leave alone internet, na ambaye hata habari yenyewe hawezi kuidigest ili iweze kumsaidia kufanya uamuzi wa makinni? Mmakonde alifanya mabaya ambayo sasa kutokana na uhuru wa vyombo vya habari tunayajua, lakini has it helped us anything? Mbona hata mahakamani kwenyewe hajafikishwa na hata dalili yenyewe hakuna? Mkuu amesema wazi kuwa wezi wa hela za EPA ni wajanja na hawakamatiki, what does knowing it mean, au uhuru huu unatumika ili kuwavurugia mambo watu fulani kisiasa?
  Cha maana kwetu ni kipi? uhuru wa vyombo vya habari vingi ambayo kazi yake kubwa ni kutumiana salamu kupiga muziki 24/7, udaku na mambo ya ngono na kashfa chafuchafu, magazeti mengine ambayo kazi yake kubwa ni kubomoa jamii yetu kuliko kujenga? Au ni kutokuwa na uhuru lakini kuwa na serikali makini inayodhibiti mfumuko wa Bei, kulinda thamani ya sarafu na kumfanya kila mtanzania anaufaike na jasho lake.

  Mkuu issue hii tunatakiwa kuiangalia kwa ujumla wake na sio kuangalia kipengele kimoja tu, tuangalie mambo yote kwa ujumla, then ndio tu judge! I stand to be corrected and criticised!
   
 7. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Bado naona kuwa Mkapa alifanya vizuri sana katika uchumi, tofauti sana na Kikwete
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wachangiaji kwamba kweli mmakonde alifanya vizuri kwenye uchumi kwa kubinafsisha mashirika hata ambayo yalikuwa yanendeshwa kwa faida mfano TBL, NBC, ATC, kuingiza netgroup solutions tena FFU n.k.

  kwa upande wa JK, mimi nafikiri amejaribu kuendeleza miradi mingi iliyoachwa na mmakonde ikiwa ndo inaanza mfano barabara zote zinazoendelea kujengwa mikataba ilisainiwa wakati wa mmakonde, na jukumu la JK ktk hili ni kuhakikisha miradi hii inakamilika. JK wengi wetu tunamuona ni mdhaifu kwa sababu tu haja funga jela gwiji yeyote wa rushwa na kufuta mikataba ya madini kama alivyo ahidi, lakini hatuwezi kusema kwamba hajafanya chochote kabisa. Kweli ana udhaifu ktk uteuzi wa watendaji lakini hata mkapa alikuwa na matatizo hayo isipokuwa kwa uteuzi wa magufuli tu.

  Jambo la msingi tuelewe kwamba athari za grand corruption huonekana baada ya miaka kama 3 hadi 5. Ukiangalia failure ya TANESCO-IPTL, THA, ATCL, n.k. ni baada ya mikataba iliyoingiwa ktk awamu ya tatu na pili, wengi tulitegemea JK aingie na kuvunja mikataba na hata kuwafunga gerezani baadhi ya wahusika, hili kweli kashindwa kwa sababu ya ugumu unaohusisha mikataba ya kimataifa lakini pia na urafiki baina yake na baadhi ya wahusika.

  Nimalizie kwa kusema JK hajauza mali nyingi za nchi kama mmakonde, ukiachilia Buzwagi na Richmond, TICTS mkataba ulisainiwa kifisadi na mkapa kabla hajaondoka na tusimhukumu Jk kwa hili na kuuvunja ni gharama pia, ingawa kama rais unaweza kuuvunja tu.
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Mkuu, huenda ni vile BADO hatujajua, na tungejua huenda tungekuwa tunamwangalia kivingine. Yake huenda yakajulikana baada ya 2015!

  Sasa basi, ni maajabu ya namna yake kuwa uchumi ulikuwa wakati wa Mkapa na hapo hapo anashutumiwa kwa kuiiba nchi.
  Muungwana hapa hatuoni kitu zaidi ya tabasamu, na hatujui kama tunaibiwa au la. katika hili bora mmakonde kama mnavomwita hapa.
   
 10. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na nyinyi wote mliotoa mawazo hapo juu kuwa Mmakonde alifanya vizuri
   
 11. green29

  green29 JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 35
  JK alikuwa ni waziri wa kutumainiwa wakati wote wa miaka 10 ya Mkap! Ni ngumu sana kumnyooshea kidole Njomba bila kumtovuga Mkwere. Alibaba fungua macho, Kikwete alikuwepo mezani na mkapa wakati wakijenga nchi pamoja. Kama kuna kitu kiliibiwa wakati huo basi na yeye alikuwepo kwenye mgao. kama walikuwa safi basi wote ni malaika.

  Karibu kila nchi duniani ina wezi na ina watu wanaojenga nchi kwenye utawala. Tatizo ni pale wanaojenga ni wachache ukulinganisha na wanaoiba. Uchumi unaweza kukua iwapo bidii ya kujenga itazidi ile ya kuiba. Kama uchumi wa TZ unakufa unafikiri nini kinaendelea?
   
 12. M

  Magezi JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Lakini jamani ni ktk awamu ya mmakonde tuliishia kupewa statistics za uchumi kukua huku mwananchi wa kawaida akizidi kuwa maskini na shilingi ikizidi kuporomoka. Mimi nacho mlaumu mkwere ni serikali yake kutokuwa na priorities za maana, angalia walivyo shupalia issue ya vitambulisho vya uraia wakati pesa hiyo ingeweza kuingizwa ktk elimu tukahakikisha kwamba waliofaulu wote advanced/FTC wanadhaminiwa kusoma chuo kikuu.
   
 13. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tatizo kubwa sana la mzee mkubwa anakosa ujasiri wa dhabiti katika kusimamia mambo muhumu sana katika ujenzi wa Taifa
   
 14. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Linapofika suala la utendaji huwezi kumlinganisha Mkapa na Kikwete au Lowasa na Kikwete, kwasababu Kikwete hawezi ni kiongozi asiyemtendaji. Ila unapozungumzia wizi lol Mkapa noma.
   
 15. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkapa kweli kwa utendaji ni hodari sana na pia huyu jamaa alitumia muda mwingi sana katika kusoma
   
 16. H

  Haki JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2009
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe acha hizo kampeni za CCM. Mnaona uchaguzi unakuja mnaanza kusifia viongozi wa CCM; kwamba awamu ya tatu ni bora kuliko ya nne. Akimaliza JK mtasema awamu ya nne ni bora kuliko ya tano. Hizi ni kampeni za CCM; ambazo zishapitwa na wakati. Nyie mnajua kabisa kwamba CCM, hakuna walichofanya tangu walipoanza kuongoza nchi baada ya uhuru (2009-1961)= 48 years. Niambie hiyo miaka 48 iliyopita CCM wamefanya nini? zaidi ya UFISADI.
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Si katika uchumi tu, ni katika maeneo mengi sana. Haya tunayoyasikia hii sasa kuhusu Mkapa wala hayatokani na kingize zaidi ya kutama kumwonyesha kwa mabaya ili wananchi wasiyaone mabaya ya utawala uliopo.
   
 18. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Mnyonge mnyongeni, tatizo la hii analysis ni kwamba ingesubiri kwanza Kikwete amalize na yeye miaka 10, ndio kwanza yupo wa nne, ingawa sio siri kwamba dalili ziko wazi tunakoelekea sio kwema!

  Respect.

  FMEs!
   
 19. a

  alibaba Senior Member

  #19
  Sep 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mwamuzi wa haki ni Mahakama mweke Njomba Nkapa kizimbani nae atasema kama alishirikiana na Nkwele, Mmachai au Ndigo? Au na Fisadi Kadhalika. end of story.
   
 20. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sasa Tatizo ni watu au yeye mwenyewe mzee mzima juu ya mambo ya uchumi then jaribu kulingalisha taaluma zao Jk ni Economist but Mkapa ni Mwandishi
   
Loading...