kijana hujui unalosema unakurupuka tu........
Huhitaji akili nyingi kujua nani ni mkurupukaji kati yetu. Kama ulifuatilia kesi ile vizuri utajua kwamba kinachofanyika sasa hivi ni kuinyonga haki na dhana ya kwamba wakubwa hawastahili kwenda jela! Kama ungekuwepo pale IFM (mimi nilikuwepo) wakati wa video evidence ambayo Marando aliipinga sana (bila mafanikio) ungejua kwamba nchi hii ilipaswa kugeuka kuwa China kwa muda na kumtia adabu Mahalu. Yule muuzaji wa jengo lile alionyesha kushangazwa na Tanzania kuwa na maofisa ambao wanalazimisha kutengeneza mikataba miwili tean mmoja ambao una-inflate bei ya mauzo na huku Mahalu akikiri wazi kwamba alitaka kujipatia kitu. Na kwa nini ilielekezwa fedha hizo za malipo ziingie kwenye akaunti binafsi ya Mahalu. Fungua macho! Usiingie kwenye mkumbo wa watu ambao wana chuki binafsi na rais na kubeza hata yale ambayo yanafanyika kuwasaidia watanzania. Kwa mwenendo huu hakika kuna haja ya kutangaza wazi kwamba kila aliye na dhamana ya mali au rasilimali za umma sasa ajichukulie tu! Hivi mnadhani Mahalu ni malaika? Ulizeni mtaambiwa. Jiulize kwa nini imechukua miaka hataki kujitetea kama hana hatia na ana utetezi wa nguvu? Hivi tutabadilika lini na kuweka maslahi ya taifa mbele? Kama Kikwete ni mtu wa bifu basi angemwadhibu Prof. Mwandosya. Mbona wanapiga kazi pamoja tena bila matatizo? Acheni kulishwa sumu na huku mnachekelea!