Mkapa alikuwa na mafaili ya wengi wasio wasafi CCM na Serikalini, Mzee Mangula simama imara kwenye kuchuja wagombea

Kwa akili yako,angeweza kudhuliwa bila wahusika kupata go ahead?

Waliomuwekea Mangula sumu wamewahi kukamatwa?

Kama hawajakamatwa,jiulize ni kweli wameshindwa kupatikana au kuna jambo nyuma yake?
Tatizo la nchi hii ni CCM na polisi. Polisi wamekuwa tawi ndani ya CCM mpaka imefikia kuona CCM ni watakatifu na wakifanya makosa yanatakaswa kwa ngyvu zote. Ila wapinzani hata wakikaa wawili tu mahali ni uchochezi. Sheria zote zinazotungwa na Bunge ni kwaajili ya kuilinda CCM dhidi ya upinzani. Yanakaribia kuisha
 
Alishakiri kwenye kitabu chake kuwa alikosea wataalamu aliowapa kazi walinmumislead .Mkapa alipompa kazi kibaka Daudi Balali Kama mshauri wake wa uchumi na mkewe Balali ndio waliharibu kumshauri kuanzia ubinafsishaji holela,kuuza Mali za umma kuanzia mashirika Hadi nyumba za serikali na za mashirika ya umma nk
Kumbe ndiyo maana Magu hacheki na nyani,ukimmisslead tu anakulamba kichwa
 
Kama mnafahamu mafisadi CCM kwanini wasichukuliwe hatua za ki sheria? Kuwahukumu watoto wao wasipate nafasi za uongozi ndani ya chama kwa makosa ya wazazi wao si sahihi.
 
Kwa akili yako,angeweza kudhuliwa bila wahusika kupata go ahead?

Waliomuwekea Mangula sumu wamewahi kukamatwa?

Kama hawajakamatwa,jiulize ni kweli wameshindwa kupatikana au kuna jambo nyuma yake?
Wakikamatwa hao waliomuwekea sumu Mzee Mangula aibu ni ya CCM yote.
 
Hata makamu wa Raisi Mama Suluhu Kashtuka na Spika Mstaafu mama Makinda kaonyesha Kushtuka
Nimechukua kwa uzito mkubwa maneno yako "I smell a rat". Wengi tumenusa harufu ya Panya huyo, ni dhahiri hata utoaji taarifa ya kifo hiki unatia shaka. Wengine watasema miaka 82 mlitaka asife? Mbona kuna wenye 90 hawajafa? I smell a Rat.
 
Kumbe ndiyo maana Magu hacheki na nyani,ukimmisslead tu anakulamba kichwa
Ndio kajifunza kwa MKapa .Wengi walikuwa wakimlaumu Magufuli kuwa ndie aliuza nyumba za serikali akiwa waziri kitu ambacho sio kweli kilichofanyika ni genge la washauri vibaka wa Raisi Mkapa akina Daudi Balali na mkewe ambao mkapa aliwaamini sana kama washauri wake wa uchumi waka mu mislead vibaya mno kwenye hayo ya kuuza mashirika na mali za umma na kuzibinafsisha

Ndio maana Magufuli mkali kama pilipili kwa wasaidizi wake au anaowateua.Ukim mislead akajua utamkoma
 
Alishakiri kwenye kitabu chake kuwa alikosea wataalamu aliowapa kazi walinmumislead .Mkapa alipompa kazi kibaka Daudi Balali Kama mshauri wake wa uchumi na mkewe Balali ndio waliharibu kumshauri kuanzia ubinafsishaji holela,kuuza Mali za umma kuanzia mashirika Hadi nyumba za serikali na za mashirika ya umma nk

Hapo kwenye red ongeza nyama tafadhari!
 
Kwani Mangula ni PCCB? Mnawajua watu wachafu badala ya kuwapeleka mahakamani sheria ichukue mkondo wake, mmebaki kutaka kupambana nao kwa siasa uchwara. Polisi na vyombo vya usalama mmebaki kuwatumia kwenda kupambana na kina Lisu kama magaidi, huku watu wachafu mkiacha wadhibitiwe na wazee!

Halafu unakuta rais wa nchi anatumia madaraka yake kubaka box la kura ili wanaccm ndio watangazwe washindi. Kashindwa kudhibiti rushwa ndani ya chama chake, saa hii anajiandaa kuweka bunge la chama kimoja, kinachoshindikana kupata nafasi za uwakilishi kwa rushwa za wazi. Shubamiit
 
Ndio kajifunza kwa MKapa .Wengi walikuwa wakimlaumu Magufuli kuwa ndie aliuza nyumba za serikali akiwa waziri kitu ambacho sio kweli kilichofanyika ni genge la washauri vibaka wa Raisi Mkapa akina Daudi Balali na mkewe ambao mkapa aliwaamini sana kama washauri wake wa uchumi waka mu mislead vibaya mno kwenye hayo ya kuuza mashirika na mali za umma na kuzibinafsisha

Ndio maana Magufuli mkali kama pilipili kwa wasaidizi wake au anaowateua.Ukim mislead akajua utamkoma

Ni mkali au ana jazba? Kama kweli ni mkali tungeona kwa uchache kabisa watia nia wa ccm 1,000 wakipandishwa mahakamani, na wangalau 200 wangekuwa magereza hivi sasa. Watu wenye jazba hutumia madaraka yao kuwakomoa wale wasiowapenda, kisha wapambe wao hutengeneza propaganda kuwa huo ndio ukali. Kama kweli ni mkali na sio mtu anayekomoa wasiomsujudia, kwenye hii rushwa ya aibu waliyofanya wanaccm kwenye hizi kura za maoni, ndio tungeona hatua stahiki.
 
Back
Top Bottom