RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Mazungumzo ya kutafuta amani nchini Burundi yanayoendelea jijini arusha chini ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu benjamini Mkapa leo yameingia katika siku ya tatu na ofisi ya msuluhishi huyo imetoa ufafanuzi wa malalamiko ya baadhi ya wanaharakati ya kutoalikwa kwa baadhi ya wadau muhimu katika mgogoro huo inayoonyesha kuwa wote walialikwa lakini wengine hawakuweza kufika.
Taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa wadau wote muhimu vikiwemo vyama vya upinzani,taasisi za dini,na wanaharakati vimealikwa na baadhi vilithibitisha kushiriki na vingine havikutoa majibu yoyote.
Aidha taarifa hiyo imeanisha baadhi ya vyama vilivyoalikwa na ambavyo vimeweza kushiriki kuwa ni pamoja na CNDD/FDD Sahwanya Frodebu na Rodebu/Copa pamoja na marais wastaafu wa Burundi Sylvestre Ntibantunganya na Domitien Ndayizeye na pia mwanasiasa maarufu nchini Burundi Agathon Ruasa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo vyama vilivyoalikwa na kushindwa kushiriki ni pamoja na chama cha MSD na kwa upande wa viongozi ni pamoja na Rais mstaafu wa Burundi Pier Buyoya na kwamba jitihada za kutafuta sababu za kushindwa kushiriki zinaendelea.
Hadi sasa tayari wajumbe wawakilishi wapatao 83 wa makundi yenye maslahi katika mgogoro huo wamefika Arusha na wanaendelea na majadiliano.
Alipokuwa anafungua mjadala wa mazungumzo hayo mh Rais mstaafu Mkapa aliwaeleza wajumbe wanaoshiriki kuwa wadau wote muhimu wa mgogoro huo wamealikwa.
Chanzo: ITV