Mkanganyiko wa Majukumu ya Mkuu wa Mkoa Vs Meya

mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
3,051
3,255
Binafsi ningependa kufahamu kipaka ya majukumu kati ya watu hawa wawili ,Naona kama Vile RC kuna muda anafanya majukumu ambayo si ya kwake .

Kwa anayejua utaratibu Rasmi atusaidie ,kuna kaharufu cha kuoneshana nani Zaidi Kati Ya RC na Mayor wa Jiji Dar .

Kwa anayefahamu atutolee mkanganyiko huu . .
 
Ukijua majukumu ya mkuu wa wilaya na mayor wa wilaya basi ushajua kwa mkoa, hakuna anayeingilia majukumu ya mwenzake kwani kabla ya kuwa viongozi lazima wale viapo na kupewa majukumu yao yote hivyo hakuna muingiliano wa majukumu.

Kwenye ubabe ni jambo la kawaida kwani mmoja amechaguliwa kwenye mchujo wa wengi ila mwingine ameteuliwa kwa matakwa ya mtu mmoja tu...kuna anayeitwa raisi wa mkoa ambaye ni RC ila mwingine ni mtekelezaji na mfuatiliaji wa mambo ya halmashauri...

Kwa sasa inawapa ugumu na kusema ubabe sababu RC ni CCM na mayor ni UKAWA ila mbona miaka yote imekuwepo hii system na haijawahi leta shida au sababu kilikuwa chama kimoja...
 
Mayor ndiye anayebeba sauti za wananchi kwa ujumla wao kwasababu anatokana na madiwani ambao huchaguliwa na watu,pia yeye ndiye m/kiti (spika) wa vikao vya halmashauri ya jiji,na kikao hiki kinauwezo wa kupiga kura ya kumkataa RC au Mkurugenzi wa jiji.

Kwa upande wa RC,yeye ni m/kiti wa kamati ya ulinzi na usalama,huteuliwa na Rais(hachaguliwi na raia),ni mwakilishi wa Rais katika mkoa,ana nguvu kisheria kumweka ndani mtu hadi saa 48.ILA HAWEZI KUMFUTA KAZI AU KUMKATAA MEYA.
 
Tatzo ukiwa ni ulemsemo WA maskini akipata HV huyu meya ndowakwanza hapa d.s.m au meya kazi zake hazijulikani?
 
Mayor ndiye anayebeba sauti za wananchi kwa ujumla wao kwasababu anatokana na madiwani ambao huchaguliwa na watu,pia yeye ndiye m/kiti (spika) wa vikao vya halmashauri ya jiji,na kikao hiki kinauwezo wa kupiga kura ya kumkataa RC au Mkurugenzi wa jiji.

Kwa upande wa RC,yeye ni m/kiti wa kamati ya ulinzi na usalama,huteuliwa na Rais(hachaguliwi na raia),ni mwakilishi wa Rais katika mkoa,ana nguvu kisheria kumweka ndani mtu hadi saa 48.ILA HAWEZI KUMFUTA KAZI AU KUMKATAA MEYA.
ni sahihi mkuuuu umeniwahi mkuu.......
 
Meya amkatae r,c alieteuliwa na rais hvyo nivichekesho nyny
mkuu kikao cha almashauri ya jiji kinauwezo wa kupiga kura kumkataa RC kma hafanyi kaz vizuri(au mbabaishaji kma makonda),...kwa kuwa mw/kiti ndo hivyo bas kla kitu kipo plain
 
Mayor ndiye anayebeba sauti za wananchi kwa ujumla wao kwasababu anatokana na madiwani ambao huchaguliwa na watu,pia yeye ndiye m/kiti (spika) wa vikao vya halmashauri ya jiji,na kikao hiki kinauwezo wa kupiga kura ya kumkataa RC au Mkurugenzi wa jiji.

Kwa upande wa RC,yeye ni m/kiti wa kamati ya ulinzi na usalama,huteuliwa na Rais(hachaguliwi na raia),ni mwakilishi wa Rais katika mkoa,ana nguvu kisheria kumweka ndani mtu hadi saa 48.ILA HAWEZI KUMFUTA KAZI AU KUMKATAA MEYA.
Mkuu hujamjibu mleta mada bado, hapa ulichofanya ni kuonyesha Mkuu wa Mkoa ni nani, Meya ni nani. Ila yeye anatakakujua majukumu yao aone hakuna mwingiliano?
 
Ni hivi,kuna mkuu wa mkoa,katibu tawala (RAS) na mkurugenzi wa jiji...hawa ni sehemu ya utawala kwa ujumla wake na wote ni wateule wa Rais.RC yeye vilevile anaangalia usalama wa mko wote.Upande wa pili kuna MEYA ambaye anaongoza halmashauri ya jiji...kazi yao kubwa ni kufanya check and balance ya utawala,kujadili na kupitisha/kutopitisha bajeti ya jiji.Kwa kifupi ni kwamba MKUU WA MKOA,RAS na MKURUGENZI WA JIJI wanasimamiwa na HALMASHAURI YA JIJI CHINI YA MEYA.
 
Back
Top Bottom