CHA The GREAT
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 651
- 854
Wandugu, nimesoma kuhusu muswada wa mfuko mpya wa jamii kama ilivyoripotiwa na gazeti la Mwananchionline hapo jana tarehe 23/11/2017.
Nina mashaka na kilichoripotiwa, aidha aliyeripoti kuna vitu ameviacha na kama hakuna kitu alichokiacha, basi muswada huo una mapungufu, dosari na mikanganyiko.
Moja ya yaliyomo kwenye muswada huo ni kwamba kutakuwa na fao la kukosa ajira, lakini haielezwi ni nani mwenye sifa zipi apate fao hilo la kukosa ajira, kadhalika haielezwi au haioneshwi ukokotoaji wake ukoje. Itakumbukwa, suala la fao la kukosa ajira limesemwa mara tatu ama nne. Mara moja (Rais Magufuli—siku ya wafanyakazi Mei Mosi, 2017) mara ya pili (Jenista Mhagama—12, Mei, 2017 kama ilivyoripotiwa na Mwananchionline: Fao la kujitoa lafutwa rasmi) mara ya tatu (Anthony Mavunde--).
Kuna kipengele pia kinasema (kwa mujibuwa gazeti la Mwananchionline) kwamba..... Endapo mwanachama hakuacha mtoto wala mke, inapendekezwa: “Wazazi wake walipewe haki zote za mtoto wao.” Je, mwanachama huyo kama hana wazazi pia hela zake zinakwenda wapi?.
Kadhalika kuna kipengele kinasema kwamba....”Muswada unapendekeza wanachama kuwa na uwezo wa kuchukua mkopo wa nyumba kwa dhaman ya michango yao waliyonayo kwenye mfuko huu mpya”. Je, ndiyo kusema hata mtu mwenye milioni mbili atapewa mkopo wa nyumba.
Kama hiyo haitoshi, kuna kipengele kinasema kwamba…… mwanachama yeyote atastahili mafao endapo atakuwa amechangia walau miaka 15 au jum-la ya miezi 180. Je, ndiyo kusema waliofanya kazi mwaka mmoja miwili mitatu ama mitano hawastahili kupata mafao na hela zao zimeenda kama sadaka.