Hata hii lugha ya Kiswahili ina jina lingine.Wengine wanatumia majina mengine
Pluto sio sayari mkuuMercury - Zebaki
Venus - Zuhura
Earth - Dunia
Mars - Mihiri
Jupiter - Sumbura
Saturn - Saratani
Uranus - Zohari
Neptune - Kausi
Pluto - Utaridi
BAKITA wana mamlaka ya kuamua kila sayari itumie jina gani katika lugha ya Kiswahili.Tatizo ni kwamba kuna majina mengi mno, tena jina moja linatumika kwa sayari tofauti.
Kwahiyo mnataka kutushirikisha wananchi ili tuyapigie kura majina ya sayari ili mchukue yatakayo shinda ?Tuko nao. Ndiyo maana tunatoa hii mada kwa umma ilituelewane kwa pamoja.
Lugha ni matumizi, na maneno yana mazoea ya kutumiwa. Kwa hiyo tutaweza kuelewa mazoea ya kutumia majina hayo, na kama kuna matumizi ambayo hatuyaelewi na kama kunamisingi ya matumizi ya maneno hayo, tutatumia michango hiyo kuwashauri BAKITA.Kwahiyo mnataka kutushirikisha wananchi ili tuyapigie kura majina ya sayari ili mchukue yatakayo shinda ?
Mi nadhani jukumu lenu ni pamoja na kuyachagua majina sahihi ya kibantu ili yatumike kuziita hizo sayari.
Na vigezo vya kuyaita vinaweza kuwa vya kitaalamu, kwa mfano mnaweza kuchukua kwa kichagua majina katika Lahaja au mizizi ya kibantu, badala ya kuchukua majina yenye matamshi (sauti) za kiarabu.
Jambo hili naona linahitaji utafiti wa kitaalamu zaidi na sio maoni ya watu.
Kuna utamaduni wa WaSwahili waliokuwa mabaharia na walishatumia majina ya sayari 5 zinazoonekana angani usiku kwa macho kavu. Walitumia nyota mbali mbali pamoja na kudinyota na fungunyota kupata mielekeo wakiwa katika uwazi wa bahari, mbali na nchi kavu. Huo ni msingi mkubwa wa kuzingatia katika kuamua majina ya sayari na nyota.Kwahiyo mnataka kutushirikisha wananchi ili tuyapigie kura majina ya sayari ili mchukue yatakayo shinda ?
Mi nadhani jukumu lenu ni pamoja na kuyachagua majina sahihi ya kibantu ili yatumike kuziita hizo sayari.
Na vigezo vya kuyaita vinaweza kuwa vya kitaalamu, kwa mfano mnaweza kuchukua kwa kichagua majina katika Lahaja au mizizi ya kibantu, badala ya kuchukua majina yenye matamshi (sauti) za kiarabu.
Jambo hili naona linahitaji utafiti wa kitaalamu zaidi na sio maoni ya watu.
Asante sana kwa shairi tamu. Inaonesha umuhimu wa kuelewana majina ya sayari.Malkia wa yamini ya Benin, wekundu wa Zebaki
Kwako najiamini,sintohama nitabaki
Mrembo mwendo Zuhura, mpole usofura
Na kwa kudura una sura umefungasha mpaka chura
Wote wa dunia, wanakuhudumia
Wewe hariri bunia, wao busati la gunia
Mahiri vita Mhiri, si jamvi la mshihiri
Mama wanisitiri, kiroho na kimwili
Roho unasumbua, Dar mpaka Bujumbura
Nikupe bamvua kama za miezi ya Sambura
Kwa kani ziso fanani, sina budi kughani
Nikuvike pete kama za kwenye Saratani
Wewe tunu johari, nikupige zumari
Na utulivu wako kama sura ya Zohari
Bi Tausi, nyara kama Kausi
Ubaridi wa Utaridi wewe mwisho wa kamusi.
Mercury - Zebaki
Venus - Zuhura
Earth - Dunia
Mars - Mihiri
Jupiter - Sumbura
Saturn - Saratani
Uranus - Zohari
Neptune - Kausi
Pluto - Utarid
Asante sana kwa shairi tamu. Inaonesha umuhimu wa kuelewana majina ya sayari.
Wewe umenikumbusha mbali hivi vitu tulivisoma primary enzi hizo ila nilisahau, ahsante kunikumbusha.Mercury - Zebaki
Venus - Zuhura
Earth - Dunia
Mars - Mihiri
Jupiter - Sumbura
Saturn - Saratani
Uranus - Zohari
Neptune - Kausi
Pluto - Utaridi
Nakumbuka kusikiliza hadithi za kipindi cha "Mama na Mwana" miaka ya themanini ya mwanzo.Kuna utamaduni wa WaSwahili waliokuwa mabaharia na walishatumia majina ya sayari 5 zinazoonekana angani usiku kwa macho kavu. Walitumia nyota mbali mbali pamoja na kudinyota na fungunyota kupata mielekeo wakiwa katika uwazi wa bahari, mbali na nchi kavu. Huo ni msingi mkubwa wa kuzingatia katika kuamua majina ya sayari na nyota.