Hali ya Mkandarasi YAPI MERKEZ ya Uturuki ambaye anajenga reli ya SGR si shwari hata kidogo kwa maana ameishiwa fedha na kushindwa kuwalipa Wazabuni wanaotoa huduma katika mradi huo. Wazabuni ni pamoja na wanatoa ya magari, Mashine na vifaa mbalimbali ya kujengea reli hiyo.
Hadi sasa imefikia miezi saba bila Wakandarasi hao kupata malipo yao huku Wazabuni hao wakilalamika kwamba kutokana Makadarasi hiyo kushindwa kuwalipa na wao wanashindwa kuwalipa Wafanyakazi wao ambao ni waendasha mitambo kama Escavetor, madereva wa malori, mabasi nk. Hali kadhalika Wazabuni hao pia wamedai kwamba wanashindwa kuwasilisha na kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na kutokupwa.
Wazabuni hao wameendelea kudai kwamba wamefanya juhudi mbalimbali za kukutana na Uongozi wa Yapi Merkez lakini hawajafanikiwa kutokana na uongozi huo kutoa visingizio vya COVID 19. Hata hivyo baadhi ya wazabuni wamedai wamefikisha malalamiko yao kwa Shirika la Reli nchini (TRC) lakini hadi sasa hawajapata ufumbuzi wowote wa malipo yao.
Kutokana na hali hiyo Wafanyakazi YAPI MERKEZ nao mwezi huu wa Saba watalipwa mshahara nusu.