Mkandarasi amchefua Waziri Mbarawa mkoani Njombe, aagiza kuwekwa kizuizini

kilagalila

JF-Expert Member
Nov 8, 2018
320
154
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa ameagiza kuwekwa kizuizini Msimamizi wa Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Igando Kijombe unaotekelezwa na kampuni ya STC JV YELL LMT Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Erick Mlema kwa kushindwa kukamilisha mradi kwa wakati.

Waziri Mbarawa amesema mpaka sasa mradi umefikia asilimia 17 pekee huku wananchi wakilalamikia kero ya upatikanaji wa maji wilayani humo.

Mradi wa Igando-Kijombe unatajwa kugharimu takribani bilioni 12 na ulianza rasmi mwaka 2018 mwezi wa 10 na kutakiwa kukamilika mnamo mwezi wa kumi 2019 na kulazimika kuongezewa muda Mkandarasi huyo mpaka mwezi wa 4 2020.

“Katika mkoa wenye changamoto kubwa za miradi ya maji ni Njombe, kuna mradi huu ambao unafika asilimia 17 hata tukimuongezea muda hamalizi,kuna mradi Makambako umefika asilimia 2 na ni mradi wa bilioni 6 hakuna kitu”alisema Waziri Mbarawa

Mbarawa amesema kutokana na hali hiyo,miradi yote yenye shida serikali itawafuta wakandarasi na kuichukua ili kuwatekelezea wananchi na kuwasaidia kuwafikishia huduma.

Mbunge wa jimbo la Wanging’ombe Gerson Lwenge amesema mradi huo tangu kuanza kwake umekuwa na shida kubwa na kulazimika kumuomba Waziri kuanza kulifanyia uchunguzi suala la kusuasua kwa mradi huo kuanzia kwenye Wizara.

“Maradi huu toka mwanzo ulikuwa na matatizo ndio maana unakuta bei zinaleta shida,lakini la msingi tutafute kila namna inayowezekana ili wananchi wetu hawa mradi uweze kukamilika”alisema Lwenge

Baadhi ya wananchi Wilayani humo akiwemo Osca Kilamya wanasema ni shauku yao kuona mradi unaanza kufanya kazi ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji.
 
Back
Top Bottom