Mkalimani aliyetafsiri visivyo matamshi ya mtalii afikishwa mahakamani Tanzania

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
_94630012_28e2bf2e-be04-4807-84b9-922cfc7a9bf0.jpg
Mkalimani mmoja nchini Tanzania, ambaye alikamatwa kwa kutoa kanda ya video ambayo alikuwa akitafsiri visivyo matamshi ya mtalii, amefikishwa mahakamani leo.

Mkalimani huyo alikamatwa wiki iliyopita kufuatia agizo la wizara ya utalii Mh Prof Maghembe, Simon Sirikwa alifikishwa katika mahakama ya Musoma Kaskazini Magharibu mwa Tanzania kwa kile mamlaka zinasema kuwa kuichafulia jina nchi.

Akiongea na BBC kamanda wa eneo la Mara Jaffer Mohammed, anasema kuwa uchunguzi umeonyesha kuwa kanda ya Video ya Simon, inakiuka sheria ya uhalifu wa mitandao.

BBC SWAHILI
 
Alidhani hatapatikana, hii ni aibu sana kwa nchi yetu. mtu hujui kiingereza halafu unapotosha
 
Huyo alifanya makusudi kama comedian muangalieni kwenye akaunti ya facebook jina Saimon sirikwa mtajua jaribu Saimon utaona uharo wake kututia aibu nchi, huwezi kuleta utani katika vyanzo vya makusanyo ya serikali au atakua ametumwa nini??! wenzetu jirani tangu juzi wametake tourism Marketing strategies weakness kwenye Tanzania tourism service daah huyu bwana mfano kama ni mauzo ya hisa ameyashusha ghafla
 
Back
Top Bottom