KISUTU: Tido Mhando afikishwa Mahakamani, asomewa mashtaka matano na kuachiwa kwa dhamana

Mangungu

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
2,392
3,017
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Wa shirika la Utangazaji nchini, Tido Mhando, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtka mashtaka matano.

Mhando ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Azam Media anakabiliwa na mashtaka matano ya matumizi mabaya ya madaraka na shtaka moja la kuisababishia TBC hasara ya zaidi ya sh. Milioni 887.

Kosa la Kwanza la matumizi mabaya ya madaraka anadaiwa alilitenda Juni 16 mwaka 2008 akiwa Dubai kama mtumishi wa TBC alisaini mkataba wa uendeshaji wa vipindi kati ya TBC na Channel Two Group Corporation bila kutangaza zabuni na kusababisha channel hiyo kunufaika

Kosa la Pili Pia Juni 20 mwaka 2008 akiwa Dubai kama Mkurugenzi wa TBC alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mikataba ya kiutendaji kati ya TBC na Channel Two Group bila kutangaza zabuni

Kosa la tatu, kati ya Agosti 18 na Septemba 2008 alitumia madaraka yake vibaya akiwa TBC kwa kusaini kununua kusambaza na kusimika vifaa vya kurushia matangazo kati ya TBC na Channel Two bila kutangaza zabuni ya manunuzi na kusababisha channel kupata dhamana

Kosa la nne alilitenda Novemba 16 mwaka 2008 akiwa Dubai alisaini mikataba ya uendeshaji wa miundombinu ya BTT kati ya TBC na Channel Two Group bila kutangaza zabuni na kusababisha channel hiyo kupata faida

Kosa la tano Kati ya Juni 16 na Novemba 16 mwaka 2008 akiwa Falme za Kiarabu kama Mkurugenzi wa TBC aliisababishia shirika hilo hasara ya milioni 887



Update:

Tido ameachiwa baada ya kutimiza masharti ya dhamana kwa mashitaka yanayomkabili na kesi hiyo itatajwa tena Februari 23 mwaka huu
tido2.jpg


Video ya Wakili wa Mhando akielezea kilichojiri Mahakama



Mhando alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kati ya mwaka 2006 na 2010. Awali alikuwa Mkuu wa Idara ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la BBC (1999-2006).

Kwa kipindi cha miaka mingi sana alikuwa akifanya kazi ya utangazaji wa radio. alianza Utangazaji mwaka 1969 Radio Tanzania Dar es Salaam, (RTD), baadaye akaenda Kenya, halafu Uingereza na hatimaye akarejea tena RTD inayofahamika kama TBC siku hizi.

Kwa sasa Tido Muhando ni Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media.

Habari zaidi...

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC, Tido Mhando leo amefikishwa mahakamani katika mahakama ya Hakimu mkazi jijini Dar es Salaam kwa mashtaka ya matumizi mabaya ya Madaraka.

Tido Mhando, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa shirika la Habari la Azam Media nchini Tanzania alifikishwa katika mahakama hiyo mapema leo Ijumaa, na kusomewa mashtaka yake.

Anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, wakati alipokuwa akilitumikia shirika hilo la Utangazaji la Serikali TBC, pamoja na kulitia hasara ya shilingi milioni 887 za Tanzania.

Mkurugenzi wa sasa wa TBC Dkt Ayoub Rioba ameambia BBC kwamba hawezi kuzungumzia taarifa hizo za kufikishwa mahakamani kwa Tido Mhando kwa sasa kwa kuwa “amezisikia pia katika mitandao ya kijamii.”

Mwanahabari huyo mkongwe ndani na nje ya nchi anatuhumiwa na Takukuru mbele ya hakimu mkazi mkuu wa makahama hiyo, Victoria Nongwa kwa mashtaka matano.
Wakili wa Takukuru Swai amesema Juni 16, 2008 katika maeneo ya Dubai, United Arab Emirates (UAE), Tido akiwa mwajiriwa wa TBC kama Mkurugenzi Mkuu kwa makusudi, alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa makubaliano kwa ajili ya kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 group Corporation ( BV1) bila ya kupitisha zabuni kinyume na sheria ya manunuzi na kuisababishia BVl kupata manufaa.

Shtaka la pili, Tido anadaiwa Juni 20, 2008 katika maeneo ya utekelezaji wa kazi yake alitumia madaraka vibaya kwa kusaini makubaliano (wakuu wa makubaliano) kwa utangazaji wa digital duniani kati ya TBC na BVl.

Shtaka la tatu, Agosti 11, 2008 na Septemba 2008 katika maeneo hayo, Tido anadaiwa kutumia vibaya madaraka yake kwa kusaini mkataba wa makubaliano (kuongeza wakuu wa mkataba ) kwa ununuzi, usambazaji kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuisababishia BVI kupata faida.

Shtaka la nne, Tido anadaiwa Novemba 16,2008 akiwa Dubai, United Arab Emirates alitumia vibaya madaraka yake kwa kusini mkataba wa makubaliano (kuongeza wakuu wa mkataba ) kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji (DTT broadcast infrastructure) kati ya TBC na BVI na kusababisha BVI kupata manufaa.

Katika shtaka la tano, Tido anadaiwa kati ya Juni 16 na Novemba 16, 2008 katika maeneo hayo ya United Arab Emirates aliisababishia hasara TBC ya Sh 887, 122,219.19.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Tido ambaye anatetewa na wakili Ramadhani Maleta alikana mashtaka yote.
Swai alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Hakimu Nongwa alimtaka mshtakiwa kutoa fedha taslimu mahakamani hapo Sh444 milioni ama hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Mbali na sharti hilo, pia awe na wadhamini wawili ambapo watasaini hati ya dhamana ya maneno yenye thamani ya Sh500 milioni na asitoke nje ya nchi bila ya kuwa na kibali cha mahakama.

Mshtakiwa alikamilisha masharti hayo kwa kuwasilisha hati za mali na wadhamini wawili nyakati za saa sita mchana na kuondoka.
Kesi imeahirishwa hadi Februari 23, 2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali
 
Hahaha Mil 900 zile za UNDP ama nini jipya?! aka "Mchakato majimboni"

In short mzee hayuko vizuri kabisa kwwmye management...kwa waliowahi Fanya nae kazi watashuhudia..

Sifa mnazo mmwagiaga humu wala siio kama wengi mnavyodhani...Pitieni file lake LA Mwananchi..TBC na hata sasa Azam!

Bure kabisa!

watapigwa vpapai hao...mzee Wa Tanga yule!
 
Back
Top Bottom