Mkakati wa Team Lowassa huu hapa

Lowassa kama ilivyoada kwa viongozi wa CCM kijinadi. Lowassa amewabiti wenzake, ndio maana wana jaribu kumchafua.
Hata hao wakina makamba wananunua watu. Ni vitu vya kawaida kwa siasa za Tanzania.
Ile ni kwamba pamoja na matarajio ya wengi kuwa kashfa ya Richmond ingemtoa nishai, imewashangaza ni kwa jinsi anavyoibuka na kuwazidi wao, wanataka kujiaminisha kama watu safi kuliko Lowassa wakati wote wametokea chama kimoja hichohicho. I think mwenye jeuri ya kujiona yuko safi angefaa atoke upinzani na sio CCM. Kwani mwisho wa siku CCM ni walewale na wamoja.
Nakumbuka kuna Waliowahi kuhama wakaenda CCJ, mwisho wa siku wakarudi CCM.
Kuna watu wanalalamika eti lowassa haongei bungeni. Aongee nini wakati yeye ni serikali?
Kawaulizeni watu wake wa monduli
Ndio watatoa jibu la kuhusu mbunge wao lowassa.
Lowassa aliwahi kusema "ukimya wangu umenisaidia sana. .mungu amenipa hekima."

Kumbe ni kweli kimya kingi kinamshindo mkuu.
Mfalme Solomon alikuwa na hekima sana. Na sasa lowasa anayo hiyo hekima.
 
Jadili na mengine haya yanachosha

Wewe ni Mtanzania makini kweli mwenye kuipenda Nchi na kujua yanayoendelea kwenye siasa zetu?

Au mwenzetu wewe U Mnyarwanda
Hata kama huipendi Kambi A ama Kambi B unapaswa unapaswa kujua kwa undani nini kinaendelea upande A angalau unaweza kuambua mbinu za kukusaidia kuuimarisha upande B.

Endapo unachoka na kuzikinai siasa mapema hivi basi utachelewa kila kitu.
 
Ukitaka ujue Lowasa anaungwa mkono kiasi gani kila ukikutana na mtu, iwe msomi, mfanyabiashara, askari n.k hebu muulize swali hili "Unadhani ni Mtu gani anafaa kuwa rais kwa Tanzania tuliyo nayo? mimi nimeanza ila sitaki kuongea hapa nisije kuwaumiza moyo wale wanaona Almasi wakasema "NIKOKOTO"
 
Ni wewe tu ndio umebaki na mawazo ya kupandikizwa,wengi tunasema NDIYO kwa LOWASSA.

Ni wewe tu na wenzako mnaotumiwa na Lowasa. Watanzania wenye akili tunajua team ya Lowasa imejaa Wezi, na tunawakataa kwa nguvu zetu zote na kwa akili zetu zote. Nguvu ya Mungu itatuepusha na kikombe hiki.
 
Ni wewe tu na wenzako mnaotumiwa na Lowasa. Watanzania wenye akili tunajua team ya Lowasa imejaa Wezi, na tunawakataa kwa nguvu zetu zote na kwa akili zetu zote. Nguvu ya Mungu itatuepusha na kikombe hiki.

Nina Ujasiri sana ninapoeleza ukweli juu ya LOWASSA kuliko Makada wengine woote walijitokeza kutaka urais ndani ya ccm.

Tuambie Lowassa aliiba nini na wapi
Acheni chuki zenu ni dhahiri WENGI HAMKUTEGEMEWA KAMA EDDO ATAKUWA NA NGUVU za kisiasa tena,
mlifanya makusudi kumtelekeza na kumchafua lakini ni Ajabu anafanya vizuri kwenye siasa,JINA LOWASSA KWA MIKAKATI ALIYONAYO NA TEAM YAKE MTAMPENDA TU NA KULAZIMIKA KUSEMA NDIYO KWA EDWARD N.LOWASSA MWAKA HUU.
 
ccm wanaogopa kumfukuza lowasa au mwizi yeyote kwa ccm ni ngumu mana 99.9%ni mafisadi

Walio ndani ya CCM yenye mamlaka na maamuzi,yawezekana wanasababu tofauti wala si ufisadi.Lakini hao CCM maamuzi wanataka sisi tulio nje tuamini kuwa Lowassa ni fisadi.Nasi kwa kutojua tunaitikia kwa jazba.Na ukienda mbele ukauliza au ukahoji kama ni mwizi kwa nini msimpeleke kwa Pilato?Hapo utasikia wakijikanyaga ohhh muda ukifika tutamvua gamba.Tunadanganywa kwa hila.
 
Hata kikwete mlimpamba hivohivo leo hii tunasaga meno kwa uongozi wake mbovu..
Hii ndo tanzania nchi inayoongoza kwa ujinga..
 
Kachukue posho yako

HAPO UMEPOTEZA DIRA KABISAAA!!!

Mmezoea siasa za kizushi,kinafiki,kiujanjaujanja, uongo na za kununuliwa.
Mimi sio miongoni mwa hao mliowazoea,Ni mwandishi huru asiye na mipaka ya vyama vyenu vya siasa.
 
HAPO UMEPOTEZA DIRA KABISAAA!!!

Mmezoea siasa za kizushi,kinafiki,kiujanjaujanja, uongo na za kununuliwa.
Mimi sio miongoni mwa hao mliowazoea,Ni mwandishi huru asiye na mipaka ya vyama vyenu vya siasa.

Wewe ni kipochi manyoyaa
 

akili ya njaa haishindwi kitu.
Njaa mbaya sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…