Mkakati wa Team Lowassa huu hapa

Mkakati wa Team Lowassa huu hapa

12STONE

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
1,190
Reaction score
409
Kwa sasa team Lowassa haisumbuliwi tena na watu aina ya Membe walipofikia wanamudu kazi yao ya kuhakikisha Mtu wao anashinda kwa kishindo cha sunammi ndani na nje ya chama

Imebainika kutoka kwa wasiri wa ndani ya team Lowassa kuwa hata hao akina MWIGULU CHEMBA na LAZARO NYALANDU hao vijana waaminifu kupita maelezo kwa Mh.EDWARD NGOYAI LOWASSA.

Usishangae kuwaona vijana hao ni kama kila mtu yuko lwake na hana habari na EDDO,Kumbe ni damu damu na mzee wa MAAMUZI MAGUMU.

Dakika,masaa,siku na miezi inayoyoma kuelekea uchaguzi wa ndani CCM utajaona wengi wakisema "KUANZIA LEO MIMI NAMUUNGA MKONO MH.SAANA EDWARD N.LOWASSA.Hio itafanyika dakika za mwisho kabla siku za uchaguzi huo kufanyika ndani ya chama tawala.

MOSI,
Lengo ni kuvunja nguvu za Mkuu wa Kaya asiweze kupindisha maamuzi na kuteua mtu mwingine.

MBILI,
Imekusudiwa kutokea wakati huo ili kama kuna masalio ya WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO wajichokee na kukata tamaa zaidi hasa kwa kuona ushawishi,nguvu na uungwaji mkono wa LAIGWANAN haviwezi kuzuiliwa na awaye yote iwe kwa UTEUZI ama UCHAGUZI ndani NEC CCM.

Sio hivyo tu hata baada ya uchaguzi mkuu ujao inaonyesha LAIGWANAN amejipanga vizuri zaidi kuliko KADA awaye yote wa CCM.Nimedokezwa yuko tayari kufanya kaxi na watu makini,wachapa kazi wasiocheka na Nyani huku shamba la Mahindi linaisha na kubakiwa na Mabua matupu.

Mipango ya inavuka mipaka ya vyama na kuweka mbele maslahi ya TAIFA letu.Huyu mtu niJASIRI SANA, alisikika mmoja wa wana TEAM LOWASSA akisema.

Msije mkashangaa hata hao watu wazuri walioko UPINZANI NAO WAKAWEKWA kwenye baadhi ya Nafasi za Uongozi ili kujenga TAIFA hili kwenye Ustawi wa

KIUCHUMI
KIAFYA
KIELIMU
Akilenga kila MWANANCHI lazima afaidi ama ale mema ya Nchi yake mwenyewe.

Tumeshuhudia wabunge MIA NA HAMSINI (150)CCM, Waliojitokeza wazi wazi bila kificho na kusema KWA RAIS AJAYE LOWASSA NDIYO CHAGUO SAHIHI NA HALALI ndani na nje ya CCM.

Hayo mliyoyaona kama ni Mvua basi hio ni manyunyu/rasharasha tu,Sunammi inakuja Vigogo wengi kila Wizara na Idara wanamuunga mkono LOWASSA.

HAKUNA SIKU HATA MOJA LAIGWAN E.N.LOWASSA ATAKWAMISHWA,AMEJIPANGA IPASAVYO.

Hapo nimewapa kionjo tu.

NGOMA INOGILE.
 
Sifa za Mafisadi huwa wanaonekana unstoppable mpaka siku ya uteuzi, maana wanatumia pesa na binadamu wa hulka ya kula pesa na kuona aibu kumwambia kwa macho na mdomo kuwa hatutakupa kura, subiri uone matokeo EL atadondoka. Simple understanding kama unawapa watu fedha lazima kwanza wapokee harafu wakusifie, hapo ni kwa manufaa yao sio yako
 
Do! Niliwahi kusema juu ya habari hizi kuelekea uchaguzi ya kwamba mwaka huu watz tulio HAI tutashuhudia mengi na ambayo vijana wangu inabidi waweke kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu. Maana mambo yanayotokea mwaka huu ni makubwa kulingana na chaguzi zooote zilizopita.
 
Do! Niliwahi kusema juu ya habari hizi kuelekea uchaguzi ya kwamba mwaka huu watz tulio HAI tutashuhudia mengi na ambayo vijana wangu inabidi waweke kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu. Maana mambo yanayotokea mwaka huu ni makubwa kulingana na chaguzi zooote zilizopita.

Ma Presdent is Lowassa napita
 
Kila kitu kinaweza kununulika kwa pesa ukiwa na pesa unaweza fanya utakalo, kwa nguvu ya pesa Lowasa ni mtu mzuri ila tutajuta
 
Kweli kabisa mkuu, angalia nguvu pesa hapo kwa picha hilo jiji linalojengwa huko uharabuni. Maji yanahamishwa hapo.




Kila kitu kinaweza kununulika kwa pesa ukiwa na pesa unaweza fanya utakalo, kwa nguvu ya pesa Lowasa ni mtu mzuri ila tutajuta
 

Attachments

  • 1428515326784.jpg
    1428515326784.jpg
    7.6 KB · Views: 7,930
Vipi ule mpango wa watu elfu kumi kwenda monduli kumshawishi umefikia wapi?
 
Mmmmmmh Mimi najua huyu jamaa ni mzuri ila hawa jamaa watakubali apenye?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom