Mkakati wa Mwigulu kuua CHADEMA Iramba

Mkakati wa Mwigulu kuua CHADEMA Iramba

Yusuph Jr

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2014
Posts
217
Reaction score
49
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya chama cha mapinduzi wilayani Iramba,zinabainisha kuwa,kuna mkakati mkubwa sana unaoratibiwa na mbunge wa Iramba ndugu Mwigulu Nchemba,wa kuhakikisha CHADEMA inapotea kwenye ulingo wa kisiasa wilayani Iramba.

Mkakati huo ambao tayari umefichuliwa na mmoja wa kiongozi mwandamizi wa CCM Iramba,baada ya kukerwa na mbinu hiyo haramu isiyo na maslahi kwa wananchi,unawahusisha baadhi ya viongozi wa CHADEMA Iramba wenye njaa kali,na ambao wamekuwa wakipinga maamuzi ya cc ya kuwavua nyadhifa zao,dk. Kitila na ZZK.

Kazi ya kwanza ni kuhakikisha ofisi za CHADEMA za wilaya zilizoko katikati ya mji wa kiomboi zinafungwa.

Pili ni kuwatumia viongozi wenye mrengo wa TEAM USALITI,kuanzisha mgogoro wa kiungozi,mmoja wa viongozi hao ni mwenyekiti wa kata ya Ndago.

Mtonyaji wetu toka ndani ya CCM anasema mwenyekiti huyu wa ndago amekuwa akilinda chama kwa kuwafukuza Zitto na Kitila,na amekuwa kinara wa migogoro wilayani Iramba.Viongozi hao wanalipwa fedha na Mwigulu.

source: Uchunguzi binafsi.
 
Mwigulu, baada ya ukombozi ni mmojawapo wa watakao kamatwa mapema ili kujibu mashitaka mbalimbali ya uvunjaji wa haki za wanadamu na mauaji. Inashangaza mtu anayepingana na wakati, ataumia mwenyewe. Haiwezekani ukarudisha enzi ya chama kimoja sasa. Mtu anayejiita msomi lakini ni mbumbumbu ktk maswala ya kisiasa huyu nina mashaka na usomi wake. Haoni Marekani, Uingeleza kuna siasa za vyama vingi, umeona wapi mtu anachuki dhidi ya chama cha upinzani hata kutema mate bungeni? Huyu mtu mwisho wake ni mbaya sababu ya kutanguliza tumbo lake kwanza.
 
mtoa mada anayo hoja unajua ukisha sema haya mambo huku jamvini na huko field yakatokea,ujue kuwa ndio hata shituka na kubadili mbinu,tunashukuru kwa taarifa endelea kufanya uchunguzi na kutujuza zaidi na zaidi
 
huko ni kutapatapa tuuu, ZZK amefkaje iramba ama imebaki anayekosoa n team usaliti? huko n kuishiwa sera. Polen sana kama mnadhan ninyi n malaika!!!!
 
ni suala la wakati,ukifika huwa hakuna namna,ataangaika sana!

Eti alienda kutubu haya ngoja tuone kama alitubu kweli au ni geresha.Kwa ujumla ni vigumu kutubu na kuacha dhambi ukiwa kwenye chama cha akina Mwigulu kwani shetani amejaa kwenye hicho chama kila kona.
 
huko ni kutapatapa tuuu, ZZK amefkaje iramba ama imebaki anayekosoa n team usaliti? huko n kuishiwa sera. Polen sana kama mnadhan ninyi n malaika!!!!

Wewe ni wa Kusamehewa bure maana hujui maana. ASIYEJUA MAANA HAAMBIWI MAANA.
 
mtoa mada anayo hoja unajua ukisha sema haya mambo huku jamvini na huko field yakatokea,ujue kuwa ndio hata shituka na kubadili mbinu,tunashukuru kwa taarifa endelea kufanya uchunguzi na kutujuza zaidi na zaidi

Asante,nipo hapa iramba kuhakikisha kunakuwa na ushindani wa kisiasa.Mbinu zao zote tutazing'amua.
 
huko ni kutapatapa tuuu, ZZK amefkaje iramba ama imebaki anayekosoa n team usaliti? huko n kuishiwa sera. Polen sana kama mnadhan ninyi n malaika!!!!

Huwezi kujua wewe kibaraka,muda si mrefu kila njama itafichuka.
 
Eti alienda kutubu haya ngoja tuone kama alitubu kweli au ni geresha.Kwa ujumla ni vigumu kutubu na kuacha dhambi ukiwa kwenye chama cha akina Mwigulu kwani shetani amejaa kwenye hicho chama kila kona.

Haikuwa toba ya kweli.
 
Jamani Mwigulu ni mtu safi sik hizi.kwanza yuko bize kutafuta pesa za kuendesha serikali.sasa hiyo mipango afanye muda gani?Kaka mwigulu achana nao
 
Jamani Mwigulu ni mtu safi sik hizi.kwanza yuko bize kutafuta pesa za kuendesha serikali.sasa hiyo mipango afanye muda gani?Kaka mwigulu achana nao

mh! Unajitahidi sana kujipendekeza kwa mwigulu,,unataka akufanye nini?? Au ashakwambia anapenda watu wanao jipendekeza kwake??
 
Jamani Mwigulu ni mtu safi sik hizi.kwanza yuko bize kutafuta pesa za kuendesha serikali.sasa hiyo mipango afanye muda gani?Kaka mwigulu achana nao

Sio lazima afanye kwa direct,anatumia vibaraka kama wewe.
 
mh! Unajitahidi sana kujipendekeza kwa mwigulu,,unataka akufanye nini?? Au ashakwambia anapenda watu wanao jipendekeza kwake??

Watu wa aina hii ni janga,kazi yao ni kuramba miguu ya mabwana zao.
 
Kama ni kweli analichafua tu kanisa la TB Joshua.
 
Acheni wivu wa kike mti wenye matunda haukosi kupigwa mawe,mwigulu Mungu akusaidie uendelee kusonga mbele ccm tunakutegemea sana.
 
Back
Top Bottom