Mkakati wa maandamano ya kupinga kusomwa kwa mara ya pili kwa muswada wa kuunda katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkakati wa maandamano ya kupinga kusomwa kwa mara ya pili kwa muswada wa kuunda katiba mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana_mapinduzi, Nov 17, 2011.

 1. M

  Mwana_mapinduzi Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Watanzania Wany'onge,

  Nina masikitiko makubwa kwa hayo ambayo yanatendwa na walioshikilia dola. Kusomwa kwa mara ya pili kwa mswada na kushindwa kuwasikiliza walio wengi (Watanzania) kwa kusingizio cha kuwakilishwa na Wabunge wao, ni usaliti tosha. Kama walivyoongea wadau wengi kuhusu mlolongo wa mamlaka ambayo amepewa Rais na hivyo kushindwa kuwawajibisha rafiki zake aliowateua kufisadi mali zetu ni jambo lisilovumilika.

  Kwa yeyote anayetaka kukukata mkono au kukupofosha ili mradi tu ushindwe kuishi kwa raha na kufurahia siku chache ambazo Mola amekupa, inabidi kumwajibisha. Njia pekee ya kuwawajibisha ni kutumia NGUVU YA UMMA. Tujifunze kutoka Tunisia, Misri, Libya na Sasa Syria. KIFUPI, TUKIAMUA, TUNAWEZA KUJIKOMBOA NA UDHALIMU HUU WOTE UNAOENDELEA TANZANIA KWA SASA. NJIA PEKEE NI KUINGIA MTAANI.

  'NASEMA TUKIAMUA TUNAWEZA'. Kwa mujibu wa Taarifa za Kiintelejinsia ya Mkuu wa Polisi TZ bwana Mwema, alisema Polisi mmoja anahudumia watu zaidi ya 3000. Naamini hawatuwezi. Jambo la msingi ni kuwa na mkakati imara itakapofika siku kuingia barabarani.

  Kwa Taarifa ambazo zimetufikia leo hii, baadhi ya Askari wa Jeshi katika nchi ya Syria wameasi na kushambulia kituo cha Upelelezi cha Jeshi la nchi hiyo. Si muda mwingi, Nguvu ya Umma itakomboa nchi ya Syria.

  Kunyimwa kwa fursa ya kuwa na katiba yetu, ni mwanzo mzuri wa kuanza kazi ngumu ya ukombozi wa nchi yetu. Kila Mtanzania atambua kuwa, jukumu la kuikomboa nchi hii ni la kila mmoja wetu. Usidhani kukaa pembeni kwako huta athirika na lolote litakalo tokea wakati Saa ya Ukombozi itakapofika. Ukikaa pembeni utambue kuwa utakuwa ni mmoja wa Wasaliti ambao tulipigania nchi wote na sasa wanatunyonya. Kujitenga na vuguvugu hizi utambue kuwa wewe ni msaliti. Saa ya kuunda baraza la mpito i-karibu. Hima tushirikiane.

  Polisi ni watu kama sisi na ni ndugu zetu kama ilivyo kwa askari jeshi na JKT. Tukiamua Tunaweza. Raia 15 Askari Mmoja. Tukiamua Tunaweza.

  Mkakati wa Maandamano
  1. Endapo polisi watajaribu kuwatawanya, msigeuke nyuma, au kurudi nyuma. Ukigeuka nyuma, mnawapa fursa ya kuwashambulia na kuwafanya lolote.
  2. Waandamanaji wa Mstari wa Mbele, sharti washikane Mikono ili kudumisha Umoja. Waandamani wa Mstari wa Nyuma Watachukua Jukumu la Kuwalinda Wale walio-mstari wa Mbele. Hata silaha, lakini hata mawe yanaweza kutumika kujihami endapo polisi wataamua kutumia mabomu ya machozi au risasi za moto.
  3. Kila Polisi anayejipendekeza kwa kuwasogelea waandamanaji ni Kumkamata Kama Mateka. Kukamatwa kwa polisi kuendelee hata sehemu nyingine, wakiwemo wale Usalama barabarani. Mwishoni, mkakati uwe wa kuwakamata polisi wote wanaovaa kiraia, na yeyote anayefahamika kuwa ni polisi na kuwadhibiti.
  4. Polisi wote wanapenda kutoa amri nao watakuwa katika mkakati wa kukamatwa na waandamaji kwa sababu ni vibaraka wa Watawala.
  5. Kama mjumbe mmoja avyopendekeza, Maandamano yatafanyika kila mahali na sehemu zote zenye mikusanyiko mikubwa mfano, Ubungo, Mwenge, Manzese, Buguruni, Magomeni, Kinondoni, Sinza, Tandale, Kimara, TAbora, Temeke; yaani kila palipo na watu, mikusanyiko itafanyika.
  6. Waandamanaji watakuwa ni watu wa rika zote, wakubwa na wadogo kwa sababu, kila mmoja anaathirika na unyanyasaji na wizi la raslimali zetu kutokana na katibu mbovu.

  Mwisho, mikakati ni mingi na wenzangu mtaendelea kutueleza mingine.

  Naamini Polisi na Jeshi Wataunga mkono harakati hizi za kuikomboa nchi yetu kutoka kwa Mabwenyenye.

  Mwanamapinduzi wa Kweli.
   
 2. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Sauti ya umma ni sauti ya Mungu. Wao watatujia kwa mabomu na risasi, Lakini sis tutawakabili kwa nguzo ya moto! Watanzania tuungane, saa ya ukombozi ii mlangoni. Tusiogope tutashinda.
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Tatizo sio mikakati. Tatizo ni lile lile la watanganyika kila siku la unafiki. Nachelea kusema hamuwezi kabisaaaaaaa kwani hata uhuru wa nchi yenu mlipewa ofisini.

  Hivyo hamna sirka hizo msidanganyane.
   
 4. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu ivi wazenj mnajitenga lini kwenye makucha yetu? yaani bado mna mawazo ya kuvunja muungano au mmeahirisha?
   
 5. T

  Tetere Enjiwa JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kuna pahala nilisoma kuwa mapinduzi yenu yalifanywa na kuongozwa jamaa kutoka uganda ila kwa uerevu wa Nyerere ndio akahakikisha karume anawatawala, isingekuwa mwalimu rais wenu wa kwanza angekua mganda, sasa jiulize mwenyewe mnafiki nani hapa? Na Nyerere kwa kumtumia karume huyohuyo akakutawaleni.
   
 6. T

  Tetere Enjiwa JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0  Ndugu yangu mbona unataka kuwaingiza waTz kwenye janga kubwa kabisa, huu ushauri wako ni wakipuuzi kabisa. Halafu unawachonganisha polisi na raia kwa nini? Mimi ni wale wanaoamini kuwa polisi wanatumwa tu kutekeleza mpango mkakati ambao umepangwa na wanamkakati kama wewe. Sasa nataka polisi na waanajeshi wa watafute hao wenye mikakati kama yako ya kuliangamiza taifa hili, kwani hao ndio wenye matatizo, wanatumiwa vibaya na watawala wetu kwa maslahi yao binafsi na wao wanataka kuwatumia polisi na wanajeshi wetu vibaya.

   
 7. CHIETH

  CHIETH Senior Member

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado nafasi ipo ya mazungumzo. Usiwapeleke watanzania huko, maana tunaweza tukaongea na tukaafikiana japo CCM wanaonekana sasa hivi wanachukia sana cdm. This is the last resort that needs mobilisation and sacrifices. So please wait a little longer.
   
Loading...