"ufisadi ni mfumo" hii ni sabuni ya kutoa madoa kwa Lowassa, na wakati huo huo ni matope kwa CCM na wala sio issue kwa Dr. Magufuli. Tafsiri yangu ni kwamba ukiwa msafi ndani ya CCM na kwenye serikali yake lazima utafunikwa kwa uchafu wake, na dawa yake ni kuiondoa madarakani ili kuwe na mfumo usio na 'ufisadi' ili wananchi wapate maisha bora. Sasa wananchi watachagua mtu safi aliyefunikwa na uchafu, au kuondoa uchafu na kuongozwa na mtu safi aliyefunikwa na uchafu na sasa hana uchafu uliomfunika tena.