Abdull Kazi
JF-Expert Member
- Dec 29, 2012
- 344
- 306
Muda mfupi baada ya vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi Ukawa kumkaribisha rasmi, waziri mkuu aliyejiuzulu,Edward Lowasa, mkakati kabambe wa kuimaliza CCM umebainika
Watu walio karibu na Lowasa wanaeleza kuwa njia ya kwanza ni kwa wagombea 80 wa CCM wanaomuunga mkono kuhakikisha wanapitishwa katika majimbo kuwa wagombea wa Chama hicho.
Watu hao wakishajihakikishia kuwa wateule wa CCM hatua inayofuata ni kuchukua fomu za Tume ya uchaguzi na kuzijaza kupitia CCM kisha fomu hizo watakaa nazo mpaka saa moja kabla ya muda wa Mwisho wa kurudisha kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi
Wakati muda ukiwa unayoyoma wagombea hao kwa pamoja watatangaza kujitoa katika kinyang'anyiro hicho kupitia CCM na kutangaza kujiunga na vyama vinavyounda UKAWA wakati huo watakuwa tayari wameshachukuliwa fomu za kuwania majimbo hayo hayo kwa tiketi ya vyama walivyojiunga navyo
Hatua hiyo itahitimishwa kwa wagombea wa vyama vilivyo katika UKAWA kwa sasa kuwaachia nafasi wale waliotoka CCM hasa katika maeneo ambayo upinzani hauna nguvu
Katika hatua ya Kwanza CCM itakuwa haina wagombea katika majimbo 80 na hili litakuwa ni pigo lao la kwanza kwani wagombea wanaounda ukawa watapita bila kizuizi kikubwa
Nitaendelea kuwaletea mkakati huo kadiri utakavyokuwa unapatikana.