Mkakati wa CHADEMA kuiangusha CCM!

Mkakati wa CHADEMA kuiangusha CCM!

Endeleeni na mkakati wenu 2020 ni kipigo cha mbwa koko
 
Hivi cdm bila wapiga kura IPO?, Mimi kinachonitisha ni kuwa wanahama na wapiga kura. Aah nimesahau , kwa hiyo ikitokea baba akasema nimechoka sigombei hivi wananchi wataenda wapi?
 
Wanaccm wengi wanafurahia wapinzani kuhamia ccm na kupewa nyadhifa mbalimbali huku hawajui mkakati Wa cdm ni kupandikiza mamluki wao kila kona ndani ya ccm, soon Bomu linalipuka, viva cdm rip ccm
Nawaza kwa sauti kubwa naona kuna point flani, but inaweza isiwe ni mkakati wa CDM direct but indirect .

Siku ikijafika wakianza kukkimbia kutoka huko CCM ndio mwisho wa CCM utakuwa .

Mleta mada your right to some extent
 
Wanaccm wengi wanafurahia wapinzani kuhamia ccm na kupewa nyadhifa mbalimbali huku hawajui mkakati Wa cdm ni kupandikiza mamluki wao kila kona ndani ya ccm, soon Bomu linalipuka, viva cdm rip ccm

Hujaenda "in deep" kuichambua hoja yako.....lakini hata mimi hili nilikuwa najaribu kulitafakari sana....

Honestly, binafsi naweza sema kuna chembe ya ukweli flani wa karibu ama zaidi ya 75%.....

Mimi sikubali wala siamini kabisa kwamba style hii ya uongozi wa Bwana Pombe Magufuli eti ndiyo kuua vyama shindani dhidi chama kinachoongoza serikali - CCM....

Anasahau kabisa kuwa ktk vita kum - under estimate adui yako huwa ni kosa linalogharimu kuliko maelezo!!

Kwa sbb, mbinu hii anayoitumia kujaribu kujenga "single party surpremacy" ktk nchi ambayo mifumo ya kisheria na kikatiba inatambua uwepo wa "mult - party democracy", ni njia iliyo nje ya zama hizi za maendeleo ya dunia ya kisayansi na kiteknolojia na ofcoz ni 100% kuandaa "chaos" katika nchi!!

Katika zama hizi, onesha uongozi wako kwa kutenda kweli na uoneshe matokeo (results/outputs) yanaoonekana na macho ya kila mtu, kushikika na mikono ya kila mtu bila kutumia ulaghai wa kipropaganda za kulazimisha watu waone kisichoonekana, washike kisichoshikika huku ukiwawatisha wakukubali, wakupende na kukuamini kwa mtutu wa bunduki......impossible....haijawahi kutokea popote duniani kwa njia hii anayotumia Magufuli!!

Na kwa sbb hii, asidhanie kamwe kabisa kuwa eti kwa sbb ya ubabe wake wa kuvi "mis-use" vyombo vya dola kwa lengo la kumsaidia kutekeleza mipango yake ya kisirisiri kinyume cha katiba na sheria za nchi ili abaki yeye peke yake kutawala inakubalika na kwamba wasiompenda na hususani wapinzani wake wao wamelala tu na hawabuni mbinu zozote kumshibiti na kisha kumtupa nje.....

Hawajalala kamwe na "absolutely" hawamwogopi.

Tatizo la Bwana Pombe nadhani hatambui kuwa binadamu "is a unique creature" kwamba wewe unapokuwa unafikiri hivi, mwenzako anafikiri vile tofauti na wewe tena pengine akiwa 100miles ahead of your strategies!!

Rejea hadithi ya Goliath na kijana mdogo Daudi katika Biblia takatifu ya Kikristo. Who expected kuwa kijana mdogo Daudi asiye na jeshi wala silaha za kivita za kisasa angeweza kuwalaza chali askari hodari na mapindikizi ya watu ya jeshi la Wafilisti wenye silaha za kisasa, mbinu za kijeshi za kisasa na vifaa vya kisasa??

Hebu watawala jifunzeni somo hili muhimu.....

Na kumbukeni kama binadamu walibuni namna ya kujaribu kumpindua Mungu Yehova kwa kumfuata hukohuko mbinguni kwa njia ya mnara wa Babeli, sembuse wewe Magufuli na CCM yako mlio binadamu wenzao???

The best way ya kuwa - impress watu ili mwisho wa siku usije kufa kwa stress huku umekenua meno na kutoa macho nje, ni kutenda yaliyo haki kisha maliza miaka yako mitano ama kumi kisha ustaafu kwa amani yako ukamalizie uzee wako kwa kula pensheni yako kijijini kwako Chato ukiwa na roho safi!!

Else, Karma itawatafuna tu wewe na wenzako!!

Na tukumbuke kuwa paka (nyau) mnyativu na mwenda pole ndiye haswa akamataye panya kwa ufanisi kuliko yule anayefukuza kwa kubamiza masafulia.....!!

Na akumbuke tu kuwa, uongozi siku zote ni dhamana ya muda tu na ktk level yake mdhamini wake mkuu ni Mungu mwenyewe muumba.....

Mungu huwa hamvumilii kiongozi (mfalme) anayeongoza kibabe kwa kutumia "miungu yake" akitesa wana wa Mungu huku akiwa amemwacha Mungu halisi....

Hacheleweshi, huwaondoa kwa aibu watawala wa namna hii!!
 
Last edited:
Wanaccm wengi wanafurahia wapinzani kuhamia ccm na kupewa nyadhifa mbalimbali huku hawajui mkakati Wa cdm ni kupandikiza mamluki wao kila kona ndani ya ccm, soon Bomu linalipuka, viva cdm rip ccm
Hivi unaifahamu CCM au unaisikia
 
Kuiua ccm ya baba yetu Jiwe ni rahisi sana, msifie uatapewa nusu ya heshima
 
Umesahau 2015, E. Lowasa alipo jiunga kwenu na ghafla mkampa aipeperushe bendera ya UKAWA???

Kama mchezo wenyewe ndo huo basi CCM wameshinda kwa kua ujio wa viongozi walio kua mawaziri wastaafu Lowasa na Sumaye walikuja kimkakati na leo hii wote meparaganyika hamueleweki mnasimamia nini.

CHADEMA iliyo jinasibu kutetea wananchi dhidi ya serikali dhalimu ya CCM awamu zilizopita ikiwa imegubikwa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji, utendaji mbavu wa watumishi wa serikali, kuzorota kwa huduma za afya, maji n.k

Sasa awamu hii imejipambanua kwa kuleta maendeleo mashinani japo kwa sasa tupo katika kipindi cha mpito ambapo serikali imejikita kuimarisha mazingira mazuri ya uchumi endelevu kwa kujenga miundo mbinu mbali mbali mfano reli, viwanja vya ndege na barabara.

kumbukeni kua mpinzani sio kupinga kila hoja hatakama zinamanufaa kwa taifa. Bali ni kupinga hoja panapo stahili na kuleta mawazo yako mbadala ili kuweza kilifikia lengo husika.

Ni hayo tu wanajamvi JF.
 
Wanaccm wengi wanafurahia wapinzani kuhamia ccm na kupewa nyadhifa mbalimbali huku hawajui mkakati Wa cdm ni kupandikiza mamluki wao kila kona ndani ya ccm, soon Bomu linalipuka, viva cdm rip ccm
Wakati mimi naona CDM imejaa wana CCM ambao hawafikiri hata mara mbili wanapoitwa nyumbani (CCM).
 
Vijana wa ufipa mnakaribia kuchanganyikiwa
 
Back
Top Bottom