Mkaa VS Gesi

Watanzania wengi bado wanaishi maisha ya kupanga tena nyumba zile za chumba kimoja kimoja bila kuwa na private kitchen, sasa akinunua gesi ataliweka wapi, uani anakopikia au chumbani? Naamini wengi wanatamani gesi lkn mazingira hayaruhusu, majiko ya kushea wanaibiana mkaa, mafuta mpaka vifuu vya nazi, leo ununue jiko la gesi uliweke uani kwenye public kitchen utaishia tu kugombana na watu. Halafu mwingine kupata elf. 2000 ya mkaa ni rahisi sana kuliko kumwambia atoe 48,000 ya mkupuo kununua gesi
 
Hoja ya msingi hii...ulinganifuu huu basi mzani umekaa mahali pake
 
Ni kweli lakini inategemea na mazingira.

Kwa hali halisi ya sasa mkaa wa sh 1000/= haumalizi siku? Huo mtu akijibana sana kabisa ni mkaa wa 1000/= (sijajua maeneo ulipo bei za mkaa zipoje)
 
Ni kweli kabisa mkuu. Suala la utamu wa chakula ni utaalamu wa mpishi tu.

Mfano: kipindi tunaanza maisha na wife tulikua tunatumia mkaa na ndio alikua mpingaji mkuu wa wali wa gesi. Ila kwa sasa kashazoea gesi anatoa vitu vya maana mzee
Wali wa rice cooker ndo wakidwanzi.
Wali wa kupikiwa na gas unahitaji utaalamu sana kupikwa na unakiwa mtamu kama kawaida, ila ukikosea ndo unatoa boko.
 
Wewe umekuja na hoja nyingine sasa...hoja ya ladha....umetoka kwenye hoja ya unafuu kiuchumi ukahamia kwenye ladha nzuri nishati ipi inatoa ladha nzuri ya chakula,rudi kwenye hoja
Kwa unafuu wa uchumi mkaa unatosha ukitumia jiko bunifu gunia la elfu 80 utadumu nalo miezi 6 kama una familia kama hauna ni mwaka 1 na unapika haina yoyote ya chakula bila kujari ugumu wa chakula hicho kuiva
 
Nimekuelewa hapo kwenye kulipia gas 48elfu kwa mkupuo ni tofauti kweli na ili ya kununua 2000 hapo ni kweli,familia nyingi kuna ugumu kumudu nishati ya gas hasa kwa hii factor...

Nini kifanyike sasa ,cha kufanya:intakiwa wasambazaji wa gas waweze kuwa na mitungi ya size ili kila mwananchi aweze kumudu gharama,ipatikane hata kamtungi ka elf5 to satisfy kila class,kama kweli tunataka kuachana na mambo ya mkaa kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…