DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mjumbe Ngome wa Jumuiya ya Wazee Mkoa wa Micheweni Pemba, Faki Ali Juma kutoka Maziwa ya Ngome amesema atamshawishi Mgombea wa Urais wa Chama Cha ACT WAZALENDO Othman Masoud Othman atie kura yake ya NDIO kwa Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na maendeleo ambayo ameyafanya kwani kila kitu kimedhihirika kuwa yeye ndio Rais wa Zanzibar.
Faki amesema kwa sasa nchi ina ulinzi na usalama na hivyo hakuna sababu ya watu kutomtilia kura za NDIO, Dkt Hussein Mwinyi “Mheshimiwa Rais ninachokwambia usitetereke wote wameshajua kuwa wewe ni Rais wa Zanzibar wote ACT WAZALENDO wanajua, wasifiche ukweli na hakuna chochote kitakachotokea ulinzi upon a tutachagua kwa salama kabisa” amesema Faki.
Faki ambaye alipandishwa jukwaani kutoa maelezo na kisha kukabidhiwa fulana ya CCM akiwa na baadhi ya vijana ambao wanaelezwa kutoka Chama Cha ACT WAZALENDO na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao baadae walilishwa kiapo cha utii wa chama hicho kabla ya kukabidhiwa fulana za chama hicho uwanjani hapo.
Katika uwanja uliofanyika mkutano Gombani ya Kale wananchi wengi walifurika kusikiliza hutuba mbali mbali za viongozi, Faki alisema kumekuwepo na maendeleo kadhaa kwa visiwa vya Unguja na Pemba huku akitaja miundombinu ya barabara, umeme, maji ujenzi wa vituo vya afya na shule mbali mbali vinatosha kumfanya Rais aliyepo madarakani kuendeleza kuongoza tena kwa kipindi cha miaka mengine mitano.