Chama cha Mapinduzi Arusha leo kimepata pigo kubwa baada ya Francis Ole Okayo kujitoa ndani ya chama hicho na kujiunga na Chadema.
Katika mkutano wa ndani unaoendelea muda huu jimboni Longido Okayo amekabidhi rasmi kadi yake kwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa.
Mjumbe huyo wa Halmashauri kuu mkoa wa Arusha kati ya 2007-2012 ambaye ana nguvu kubwa jimboni Longido amesema CCM imeshakufa na kinachosubiriwa ni mazishi yake tu Oktoba mwaka huu.
Baadaye jioni mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema anatarajiwa kuwasili kwa chopa mjini Longido kuongoza mkutano mkubwa wa hadhara wa kumpokea rasmi Francis Ole Okayo CHADEMA.