Uzi huu unanikumbusha mbali hasa naposikia neno Cannibalism, in fact 90% ya viumbe wa baharini na kwenye maji kiujumla ndio wana hii tabia ya Cannibalism , yaani tabia ya kuweza kula kipande cha mwili au mwili wote wa kiumbe mwenzako wa aina yako.
Kwa binadamu, inadhaniwa kuwa wachawi ndio wana hizi tabia za kula watu, na kwa maelezo ya mwandishi ni kuwa ELIZABETH BATHORY alikuwa anafanya ibada za kichawi.Hivyo ni ushahidi tosha kuwa tabia za wachawi ni kula watu.
Naomba kuuliza hivi UCHAWI na UKATILI ni nadharia mbili zanazoenda kwa pamoja? Maana nasikia wachawi wengi huwa wana roho ngumu za kikatili. Je hakuna wachawi wenye moyo wa huruma. Naomba majibu wakuu.
Nawasilisha
Asante kwa kuuliza swali mkuu. Nitajaribu kujibu kwa uelewa wangu. Na nitakapoishia naomba mwenye kuelewa ataendeleza.
1. Kwa kuanza ni kweli Cannibalism ipo tena kwa kiasi kikubwa. Achilia mbali viumbe ambao wao ni Carnivorous in nature kama Chui, Simba, Mbwa na wengine. Upande Wa marine organisms ni kweli kuwa samaki wanazo traits za Cannibalism mfano: Wanabiolojia wanadai kuwa samaki aina ya Sangara amechangia kupotea kwa species za samaki zaidi ya elfu moja ndani ya ziwa Victoria. Hii Ina maana ya kuwa Sangara amekula species zingine sio kwamba ni ukatili lakini adaptation ya Sangara sio Ziwa Victoria Bali ni Ziwa Turkana.
Turudi kwenye lengo nitajibu kwenye pande mbili swali lako mkuu.
2.1. Uchawi na Ukatili vinaweza kuwa pamoja au dhana zenye kushabiana, kwa maana hii; dunia Imepata kushuhudia mambo na matukio mbalimbali ya kutisha mfano; watu kupoteza viungo vyao kwenye mazingira ya ajabu ajabu. Hii inapelekea moja kwa moja Wachawi kupewa cheo au sifa nyingine ya Ukatili. Tukichukua mfano rahisi Wa huyu bi mdada Elizabeth licha ya kuwa na jina tanu sana lakini matendo yake yamemfanya hata wale waliokuwa wanafanya kazi ndani ya jumba lake la kifahari kuona ni kama mchawi tu, sababu ni mtu gani mwenye ujasiri Wa kumkata kichwa Binti na kukitumia kichwa hicho kama sehemu ya kuweka mshumaa? Je ni nani mwenye roho ngumu mpaka kumtoboa mtu tumbo na kukinga damu na kuna kuinywa? Haya matendo yalitosha kumpa haki ya kuitwa mchawi.
2.2. Uchawi una philosophy yake na umegawanyika kwenye makundi mawili makuu. Kuna uchawi wa kudhuru au kuua na uchawi Wa dawa. Makundi haya ni maarufu sana kwa majina ya Black Magic pamoja na White Magic.
2.2.1. Tuanze na Black Magic au Uchawi Wa Kudhuru. Huu ni uchawi wenye nia zenye kuua mnyama au mtu kama sio kumdhuru, inahusisha kufanyika kwa matambiko yenye nguvu sana ambayo kuzuiwa ni mpaka kafara zitolewe. Hapo ndo kuna Kafara za wanyama na Human Sacrifice. Kundi hili ndo linaonekana sana kama wakatili kutokana na ukweli kama philosophy yao imekaa kwenye kudhuru au kuua tu na sio kuponya. Kwenye kesi hii Bi Elizabeth tunaona ni kama mmoja Wa Black Magicians tu kutokana matendo yake.
2.2.2. White Magic au White Magicians; hiki ni kundi la kipekee lenye kutokutambuliwa na dunia kwa kina. Hawa ni wale waongofu katika uchawi yaani wanatumia uchawi kwa nia ya kuponya au kutibu tu, wala sio kujeruhi wala kuua mnyama na hata binadamu. Kundi hii ni safi kwani halina historia chafu kama ya upande Wa kwanza kule (Black Magicians) kwani hawa naweza kusema wamebebwa na philosophy yao ya uchawi kuwa upande Wa kutibu tu. Ni nadra sana kuona White Magicians wanafanya Ukatili labda tu kama akitoka kuwa White Magician au Mchawi msafi na kwenda kuwa Black Magician au mchawi Mchafu. Na wanakuwa ni hatari kuliko hata Wazoefu Wa black magic kwani huyu anakuwa anajua dawa nyingi na namna ya kutengeneza ndumba (spell)
NB: Kwa wenye elimu ya Majini na mapepo (Demonologists) wanadai Ukatili katika uchawi utokea tu pale ambapo dhamira itakuwa ni tofauti na Kutibu au kuponya.
Hivyo ni kweli wachawi ni wakatili lakini sio Wachawi wote ni wakatili. Inategemea na Dhamira husika ya ndumba (spells) zao.
I hope nimekujibu mkuu.......