Mjue ndg Charles Ekelege | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjue ndg Charles Ekelege

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Njowepo, Apr 20, 2012.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  [h=3]Board Memberships and Affiliations[/h]


  [h=3]Education[/h]
  [h=6]B.Sc , Electrical Engineering[/h] University of Dar es Salaam
  Mwenye info zaidi aziweke apa maana huyu ndiye anayetulisha Blue Band feki,pitisha fake tyres etc.
  We need to know who is this person messing up with our life and health!
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Muonekano mwingine व Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege wakati wa kikao hicho
  [​IMG]
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege (kushoto) akiwa hoi wakati Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC), Deo Filikunjombe (kulia), akimshutumu kwa utendaji wake mbovu, uliojaa utapeli ambao Kamati hiyo iliugundua katika ziara nje ya Nchi ya kukagua kampuni za ukaguzi wa magari yanayoingizwa nchini. Filikunjombe alikuwa anazungumza hayo katika kikao cha kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (POAC) na PAC cha kujadili utendaji wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dar es Salaam
  [​IMG]
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege akizungumza na wanahabari baada ya sakata hilo, hata hivyo hakutaka kufafanua jambo lolote , hivyo kuamua kuondoka na kuwaambia kuwa wanahabari atakutana nao leo kuelezea kwa kina.
  [​IMG]

  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC), Deo Filikunjombe (kulia), akimshutumu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Charles Ekelege (picha ya juu) kwa utendaji wake mbovu, uliojaa utapeli ambao Kamati hiyo iliugundua katika ziara nje ya Nchi ya kukagua kampuni za ukaguzi wa magari yanayoingizwa nchini. Filikunjombe alikuwa anazungumza hayo katika kikao cha kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (POAC) na PAC cha kujadili utendaji wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dar es Salaam
  [​IMG]
  Mbunge Lugora akielezea jinsi alivyoaksilishwa na ubabaishaji wa Ekelega, na kuamua kumrushia konde ambalo lilidakwa na Filikunjombe wakiwa Ughaibuni baada kamati kupewa sumu feki ya kampuni ya nje inayokagua magari yanayoingizwa nchini
  [​IMG]
  Mbunge wa Viti Maalum, Esther Bulaya (CCM), akielezea jinsi alivyotapeliwa na wakala wa ukaguzi wa magari
  [​IMG]

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko,Joyce Mapunjo (katikati), akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC), Deo Filikunjombe (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (POAC), John Cheyo baada ya kamati hizo kumtajia uozo wa ukaguzi wa magari unaofanywa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na kampuni feki za nje ya Nchi,jana wakati wa vikao vya Kamati za Bunge, Dar EsSalaam.Picha na Mdau Richard Mwaikenda
  --
  KAMATI ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC) imemlipua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Nchini (TBS), Charles Ekelege baada ya kubaini kuwa shirika hilo lina ofisi hewa za ukaguzi wa magari nje ya nchi.

  Imesema kutokana na hali hiyo fedha za ukaguzi zinazotolewa na wanunuzi wa magari, zinaishia mikononi wa wajanja huku ikisisitiza kuwa itaanika madudu mengine ya TBS katika kikao cha Bunge kinachoanza wiki ijayo na kwamba hali hiyo ndio chanzo cha kujazana kwa magari mabovu nchini. Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Hesabu za Serikali, (PAC), Makamu Mwenyekiti POAC, Deo Filikunjombe alisema waligundua madudu hayo baada ya kamati yake kutembelea vituo vya ukaguzi wa magari nchini Singapore na mjini Hong Kong, China.

  Wakati Filikunjombe akieleza hayo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Joyce Mapunjo, Ekelege alionekana kuishiwa nguvu na kupata mshangao. Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali, John Cheyo alisema a walilazimika kuwaita wajumbe wa POAC katika kikao hicho kwa kuwa suala hilo ni nyeti. “Tulikwenda Hong Kong na Singapore na tumegundua kwamba TBS ni wababaishaji, huwezi kuamini anachokifanya Mkurugenzi (Ekelege) huko nje”,
  “Ninasema haya bila woga wowote na hata nikiwekewa sumu, wajumbe wengine wa kamati yangu watasema,” alisema. Alisema walipotembelea Hong Kong, waligundua kuwa ukaguzi wa magari haufanyiki na kwamba fedha zinazotolewa na wanunuzi zinaliwa na wajanja.

  Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa kamati,Ekelege aliwapeleka katika ofisi hewa ambayo baadaye waligundua kuwa haikuwa ya ukaguzi wa magari. “Katibu (Mapunjo) ili ulinde heshima yako usimbebe Ekelege, tumekwenda Hong Kong na akatupeleka katika ofisi feki na tulipombana akasema kuwa aliomba kwa muda kuitumia ofisi hiyo,” alisema Filikunjombe. Alisema kampuni inayotumiwa na TBS kukagua magari nje ya nchi inapasaw ieleweke huku akifafanua kuwa wakati wakiwa Hong Kong, walinunua cheti feki cha TBS mtaani. “Huyu Ekelege si mkweli, ukaguzi wa magari haufanyiki sisi tumekwenda na kujionea wazi, ndio maana magari mengi yakifika hapa yanakuwa mabovu na gharama za usafirishaji na ukaguzi zinakuwa kubwa,” alisema Filikunjombe.

  Kwa mujibu wa Filikunjombe baadhi ya watu waliowakuta katika kampuni hizo waliwaeleza kuwa Ekelege amekuwa akiwaeleza kwamba fedha za ukaguzi zinazopatikana wazitumie kununulia vifaa vya magari. Alisema walipokwenda Singapore pia hawakukuta kampuni ya kukagua magari na kwamba walipomuuliza Ekelege akashindwa kuwapeleka zilipo ofisi za ukaguzi wa magari. “Jamani mashirika yetu ya umma yananyonywa na wajanja wachache, fedha zinaliwa na wakati tupo huko tuliomba namba za simu na kupewa za uongo,” alisema Filikunjombe.

  Alisema kama Mapunj) anambeba Ekelege, wao kama wabunge hawatakuwa tayari kuvumilia suala hilo huku akisisitiza kuwa wana mengi ya kuzungumza kuhusu mkurugenzi huyo. “Hayo ni machache sana kuna mengi ambayo kamati tumeyagundua katika ziara yetu na tutayaanika hadharani Dodoma,” alisema Filikunjombe.

  Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugora alisema walipokuwa nchini humo alitaka kupigana waziwazi na Ekelege baada ya kugundua jinsi walivyokuwa wakidanganywa kama watoto wadogo. Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Ester Bulaya alisema a ripoti ya TBS inaonyesha kuwa ukaguzi wa magari ni Dola150 lakini ofisi hizo za ukaguzi zinataka zilipwe Dola300. “Mimi mwenyewe walitaka kunitapeli nilikuwa nataka kununua gari na wakanieleza niwatumie Dola300 wakati kawaida natakiwa kulipia Dola150, nilipowaeleza wakasema wana mtandao mkubwa na hata niende wapi siwezi kuwakamata,” alisema Bulaya.

  Mapema Cheyo aliiponda ripoti ya TBS ya mwaka 2011 na kueleza kuwa ina upungufu mkubwa.
  “Ripoti ina upungufu, kwanza haina takwimu zinazoonyesha magari mangapi yalikaguliwa na ukaguzi uliingiza fedha kiasi gani na zilizobaki ni kiasi gani” alisema Cheyo. Alisema licha ya taarifa ya CAG kueleza kuwa zoezi la ukaguzi wa magari halikufanyika ipasavyo, bado ukaguzi wa kucha bandia na nywele uliendelea kufanywa na kampuni hizo hewa.

  “Hata vitu vilivyokaguliwa na kuonekana kuwa havifai haijulikani viko wapi, haijulikani kama vimetupwa ama laa, hakuna ushahidi vilikuwa kiasi gani” alisisitiza. Alisema kuwa kutokana na hali hiyo kamati yake haitaipitisha ripoti hiyo huku akimwagiza Mapunjo kuandaa upya ripoti hiyo na kuiwasilisha mbele ya kamati yake kabla ya Februari 2 na iwe imekaguliwa na CAG.

  “Hakuna haja ya kuendelea kubishana tunaitaka wizara mpaka kufika Alhamisi ijayo (Februari 2) tupate takwimu zote na ziwe zimekaguliwa na CAG,” alisema Cheyo. Cheyo alimweleza Mapunjo kwamba kabla ya kumalizika kwa kikao cha Bunge mjini Dodoma watakutaka na Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko na Kamati ya PAC na POAC ili kulijadili kwa kina suala hilo.

  “Pia tutamweleza Spika wa Bunge ili kuona kama suala hili tunaweza kulifikisha bungeni ili wabunge watoe maoni yao,” alisema Cheyo. Ekelege anena Baada ya kikao hicho kumalizika Mwananchi lilimtafuta Ekelege ili ajibu tuhuma hizo ambapo alisema kuwa hawezi kuzungumza lolote huku akitaka atafutwe leo ofisini kwake.

  Huku akionekana kuwa na kigugumizi Ekelege alisema,“Kwa leo siwezi kusema lolote kwa kuwa sina data (vielelezo), kesho (leo) njoo ofisini kwangu nitakueleza kila kitu, ila kwa sasa siwezi kusema lolote” alisema Ekelege Kauli ya Wizara Kwa upande wake Mapunjo alisema kuwa hawezi kueleza chochote kwa kuwa hajaipata ripoti ya CAG na kusisitiza kuwa atakapoipata ripoti atatoa ufafanuzi.   
 3. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  TUTAENDELEA KULINDANA ILA MWISHOWE TUTALIA!!!:shut-mouth:
   
Loading...