Mjue mwanzilishi wa hoja dhaifu ya 5G kusababisha Covid-19 kabla haijakamatwa na "wakamata-fusra wa nadharia njama"

Dr Mathew Togolani Mndeme

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
201
808
Jua kilichotokea kwa ufupi kisha ujisomee kiambatanisho na link iliyoko mwishoni
  1. Hoja dhaifu kwamba Covid-19 imesababishwa na teknolojia ya 5G Ilianzishwa na Daktari mmoja wa Ubelgiji anayeitwa Kris Van Kerckhoven.
  2. Alifanyiwa mahojiano na kazeti la kidachi la Het Laatste Nieuws tarehe 22 January 2020 wakati Covid-19 ilikua haijaanza kusambaa nje ya China.
  3. Katika maelezo yake akasema anahisi Covid-19 inasababishwa na 5G, lakini hakua na maelezo yoyote ya kwa nini anahisi hivyo.
  4. Mahojiano haya yalichapishwa kwenye gazeti la Ubelgiji lakini makala hiyo ikafutwa (online) baada ya kuonekana hakuna ushahidi wa alichosema.
  5. Tatizo wakati wanafuta makala online, ilikua imeshachapishwa na imeshasomwa na watu kadhaa. Ndani ya muda mfupi ikawa imeshasambaa katika nchi zinazoongea kidachi.
  6. Wakamata fursa wa nadharia njama (Conspiracy Theorists) ambao nao walikua na hofu na ugonjwa huu kama ilivyo kwa kila mtu, wakaikamata hiyo hoja na kuanza kuitengenezea maelezo ya kuungaunga, uongo, na uzushi kwa kigezo cha kujua sayansi.
  7. Kwa bahati mbaya sana, nadharia njama hii ikawafikia "watumishi" na wao wakaisambaza kama "hoja na mafunuo ya kiroho" hivyo ikaanza kutembea kwa kasi miongoni mwa makundi ya kiimani.
  8. Kama ujuavyo, wengi wetu hatuhoji mambo yanayoongelewa kiimani na baadhi yao wametukaririsha kutoshuku wanayosema hasa kwa kuwa wamefanikiwa kutukamata akili zetu. Tumejikuta tunawaogopa na kuwasikiliza hata kuliko "tunayemwamini na neno lake".
  9. Mwisho wa siku, uongo umeshapikwa vya kutosha sasa umekua ukweli unatotumika madhabahuni na hata kutumika kushauri kuhusu kinga.

    Tazama kiambatanisho cha mahojiano yenye kauli ya kwanza kuhusu 5G na Covid19 (imeandikwa kwa lugha ya Kidachi)

  10. 1586488168594.png
  11. Fungua link (How the 5G coronavirus conspiracy theory tore through the internet) kusoma maelezo ya undani kwa kingereza ni kwa jinsi gani kauli hii ya kizembe ya huyu daktari ilivyobadilishwa kuwa nadharia njama na kuvuma ulimwenguni kwa kasi ya maambuzi ya Covid-19 hadi kutumia kwenye madhabahu za ibada na kuwa "kiki ya kitumishi".

    Niliichambua mada hii kwa kirefu siku ya juzi. Kama utapenda waweza kuisoma kwenye uzi huu: Teknolojia ya 5G na Chanzo cha Covid-19: Nadharia Njama (Conspiracy Theory) yenye maswali mengi. - JamiiForums


    Ushauri:
    Moja, Iliwahi kushauriwa kwamba "Akili za kuambiwa, tujitahidi sana kuchanganya na zetu"
    Mbili, tujitahidi sana kutafuta habari za kweli kabla ya kukubali kuaminishwa uongo hata kama unafanana sana na kweli



    MM Togolani


















 
Hua siamini sana wanachosema viongozi wa dini mbalimbali pale majnga yakitokea. Yani shida zao ni sadaka na zaka tu.
 
Shukrani sana, hki kitu kinasambaa sana watu wameaminishwa ujinga, kinahubiriwa kanisani.
 
Mwehu aliyeikamatatia huku kwetu ndio hajielewi kabisaa.Hata simu yake inaweza kuwa na 5G na hajijui.
 
Back
Top Bottom