Mjue mnyama NUNGUNUNGU

Mpauko

R.I.P
Jan 19, 2019
2,323
3,353
Nungnungu(Porcupines) au nungu ni ni mnyama mgugunaji mwenye ngozi yenye miiba iliyochongoka wanayotumia kujilinda na maadui,Ila sio kwa kuilusha miiba hiyo.

Ana manyoya magumu ya kahawia na meupe kichwani na shingoni, lakini miiba yake yenye ncha za rangi ya manjano ndiyo humtambulisha zaidi.

kutoka mahali pamoja na kuufunika mwili wake. Kila mwiba umezungukwa na mitaro-mitaro na umejipinda mahali ambapo umeshikamana na ngozi na kufanyiza pembe-mraba.

Mwiba huanza kuwa mwembamba na kujipinda unapokaribia kushikana na ngozi. Ndiyo sababu nungunungu hawezi kuchomwa na miiba yake hata akianguka kutoka mahali palipoinuk,Ama kweli, nungunungu ameumbwa kwa njia ya ajabu!

Ni vigumu sana kuweza kumuona kwa vile anaishi kwa mashaka sana,kwani aonekanapo hushambuliwa na kuuawa kwa ajili ya kutengenezea dawa na kitoweo,wakati mwingine hukamatwa na kufugwa.

Anaposhtuliwa, nungunungu hujikinga kwa kujikunja kama mpira,Misuli yake yenye nguvu hukaza ngozi yake yenye miiba na kuufunika mwili mzima,Ngozi hiyo yenye miiba hufunika kichwa, mkia, miguu, na sehemu zake za chini na anaweza kujikunja hivyo kwa muda mrefu.

Nungunungu huona njaa wakati wa jioni. Chakula chake cha jioni huwa wadudu na minyoo, lakini wakati mwingine anaweza kula panya, chura, mjusi, au hata njugu na matunda ya beri.

nungunungu hana maadui wengi mwituni,mbali na mbweha na melesi, Melesi(chui)aweza kubambua ngozi ya nungunungu kwa kucha zake zenye nguvu bila kuumizwa na miiba.

Nimewahi kuona ngozi ya nungunungu mara kadhaa,Huenda ngozi hiyo ikawa imebaki baada ya melesi kumla nungunungu mzima.

Kwa upande mwingine, mbweha hawezi kustahimili miiba ya nungunungu lakini anaweza kujaribu kumbiringisha hadi majini,

ambapo nungunungu hulazimika kujikunjua la sivyo atakufa maji,Kwa kuwa nungunungu ni mwogeleaji hodari, huenda akafikia mawe au kuingia ndani ya mashimo yaliyo kando ya mto kabla mbweha hajamnyakua na kumfanya kuwa kitoweo chake.

Nungunungu huanza kujamiiana katikati ya miezi ya Mei na Julai, na wanarudia kufanya hivyo kwa mara ya pili katika kipindi hichohicho.

Baada ya majuma manane hadi tisa, watoto watatu au wanne huzaliwa wakiwa na uzito unaopungua gramu 30, Watoto hao huwa hawaoni wala kusikia wanapozaliwa, hivyo wanaweza kushambuliwa kwa urahisi katika majuma mawili ya kwanza.

Kisha miiba humea mahali palipokuwa na manyoya laini. Baadaye wanaweza kujikunja kabisa,Kabla ya kupata uwezo huo, wao huruka juu mara moja na kutoa mlio mkali wa kuchakatachakata wanaposhtuliwa, Jambo hilo huwatisha maadui zao wengi.

Majira ya baridi kali yeye hutumia muda mwingi akiwa amelala,ana tezi maalum inayomsaidia kusawazisha joto la mwili wake,majira haya yeye hula kwa nadra sana hivyo hutumia mafuta ya ziada anayohifadhi mwilini mwake.

Ukijaribu kumfuga nungunungu, yeye hupanda ukutani, au kwenye bomba la maji na kuponyoka kwani anapenda kulisha katika eneo kubwa.

Ndiyo sababu, si rahisi kumfuga au kumfanya awe mnyama kipenzi, Ni vizuri zaidi kwamba hafugwi kwa kuwa yeye hubeba viroboto wengi sana kwanza utavitoaje?????

images(27).jpeg
images(26).jpeg
images(24).jpeg
 
Attachments

  • Screenshot_2019-08-06-01-33-43.png
    Screenshot_2019-08-06-01-33-43.png
    211.9 KB · Views: 19
Lengo ilikuwa kuupload baby nungunungu....nimerekebisha.

Pia nungunungu huwa hafyatui miiba.

Cc SteveMollel
 
View attachment 1173340View attachment 1173341View attachment 1173342
 
Back
Top Bottom