Mjue Mchezaji mpira Jean Pierre Adams ambae bado yupo kwenye COMA kwa takribani miaka 38

wilson kaiser senior

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
397
1,000
BADO AMELALA.

FB_IMG_1592584555137.jpg

Wakati tunaendelea kufurahia kuzinduka kwa mchezaji wa Ajax ABDELHAK NOURI baada kuwa kwenye Coma kwa takribani miaka miwili akiwa amepoteza fahamu, tukumbuke pia kuna mchezaji mwingine 'Bado amelala'. Anaitwa Jean-Pierre Adams, nyota wa zamani wa PSG na timu ya taifa ya Ufaransa, aliyebarikiwa ngozi adhimu yenye rangi ya thamani kama umuonavyo pichani. Hajui atazinduka lini maana ni miaka 38 sasa amepoteza fahamu asijue nini kinaendelea duniani. Inauma sana!!

Hivyo basi: wadau wa soka ulimwenguni, tukiwemo waafrika hasa wa nchini Senegal mahali alipozaliwa, kwa pamoja tuungane katika kumuomba mwenyezi Mungu ampe afya njema Adams, ili aweze kuzinduka kutoka kwenye Coma na kuungana tena na familia yake aliyoiacha tangu 1982.

Inshallah Adams atafumbua tena na kukuta mambo mengi yamebadilika kwanza atakuta timu yake ya Ufaransa imetwaa kombe la dunia mara mbili. Pia atakuta watoto wake nao wana watoto hivyo ataitwa babu. Pia atamkuta mkewe kabadilika, maana alimuacha akiwa binti lakini sasa ni bibi mwenye zaidi ya miaka 60.

Yote kwa yote, tuendelee kumuomba Mungu ampe uzima Adams, pamoja na kumpa moyo wa ujasiri mke wake, Bernadette, amekuwa akimhudumia tangu 1982 akikataa Adams kufanyiwa 'euthanization' (assisted suicide) akiamini kuwa ipo siku atapona. Huu ni upendo wa hali ya juu! Anastahili sifa na pongezi na Mungu ambariki.

Amina🙏🏿
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
12,758
2,000
Aiseee toka nimekuwa jf hakuna mada ambayo akili yangu inasoma negative kuiamini kama hii!!. Miaka 38 kwenye coma! Mke akatae madaktari washindwe kufanya Yao.

Naona tunalazimishana kuwa sayari ya mars wakati bado tupo duniani hapahapa aliposhushwa shetwain..!
 

Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
8,204
2,000
Aiseee toka nimekuwa jf hakuna mada ambayo akili yangu inasoma negative kuiamini kama hii!!..
Miaka 38 kwenye coma! Mke akatae madaktari washindwe kufanya Yao..
Naona tunalazimishana kuwa sayari ya mars wakati bado tupo duniani hapahapa aliposhushwa shetwain..!
Mkuu ni kweli nenda YouTube andika Hilo Jina utapata taarifa zake
 

wilson kaiser senior

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
397
1,000
kama hii mada inaukweli. .basi huyo mungu mnaye muabudu atakuwa ni katili sana
Usiseme hivyo na jutia kauli yako. Mungu anafanya kazi yake kwa namna mbali mbali, anakupa shibe wewe mwingine anampatia njaa. Anakuja kifo wewe ananipa uhai Mimi. Aliyekuinua wewe ndie atakae nishusha Mimi.

Yote haya ni kudhirisha ukuu wake, ndie muweza wa yote na ndie muamuzi ya yote. Ndio maana hatupaswi kulaumu Bali yatupasa tushukuru kwa kila jambo.

Kufanya hivyo au kuruhusu yote hayo ni kwamba tumtegemee yeye tu.
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
7,080
2,000
Mbona umetumia lugha ya kibaguzi kwenye michezo? Na hao waliomwajiri wangefanya hivyo sijui kama angechezea timu ya ulaya.
 

hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
38,558
2,000
Usiseme hivyo na jutia kauli yako. Mungu anafanya kazi yake kwa namna mbali mbali, anakupa shibe wewe mwingine anampatia njaa. Anakuja kifo wewe ananipa uhai Mimi. Aliyekuinua wewe ndie atakae nishusha Mimi. Yote haya ni kudhirisha ukuu wake, ndie muweza wa yote na ndie muamuzi ya yote. Ndio maana hatupaswi kulaumu Bali yatupasa tushukuru kwa kila jambo.
Kufanya hivyo au kuruhusu yote hayo ni kwamba tumtegemee yeye tu.
nijutie kauli yangu nini acha ujinga. .hivi nyinyi wafia dini mbona mnapenda sana kutishana tishana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom