WilsonKaisary
JF-Expert Member
- Apr 4, 2017
- 392
- 946
BADO AMELALA.
Wakati tunaendelea kufurahia kuzinduka kwa mchezaji wa Ajax ABDELHAK NOURI baada kuwa kwenye Coma kwa takribani miaka miwili akiwa amepoteza fahamu, tukumbuke pia kuna mchezaji mwingine 'Bado amelala'. Anaitwa Jean-Pierre Adams, nyota wa zamani wa PSG na timu ya taifa ya Ufaransa, aliyebarikiwa ngozi adhimu yenye rangi ya thamani kama umuonavyo pichani. Hajui atazinduka lini maana ni miaka 38 sasa amepoteza fahamu asijue nini kinaendelea duniani. Inauma sana!!
Hivyo basi: wadau wa soka ulimwenguni, tukiwemo waafrika hasa wa nchini Senegal mahali alipozaliwa, kwa pamoja tuungane katika kumuomba mwenyezi Mungu ampe afya njema Adams, ili aweze kuzinduka kutoka kwenye Coma na kuungana tena na familia yake aliyoiacha tangu 1982.
Inshallah Adams atafumbua tena na kukuta mambo mengi yamebadilika kwanza atakuta timu yake ya Ufaransa imetwaa kombe la dunia mara mbili. Pia atakuta watoto wake nao wana watoto hivyo ataitwa babu. Pia atamkuta mkewe kabadilika, maana alimuacha akiwa binti lakini sasa ni bibi mwenye zaidi ya miaka 60.
Yote kwa yote, tuendelee kumuomba Mungu ampe uzima Adams, pamoja na kumpa moyo wa ujasiri mke wake, Bernadette, amekuwa akimhudumia tangu 1982 akikataa Adams kufanyiwa 'euthanization' (assisted suicide) akiamini kuwa ipo siku atapona. Huu ni upendo wa hali ya juu! Anastahili sifa na pongezi na Mungu ambariki.
Amina🙏🏿