Mjue Mangi Mandara wa Moshi

Mainus

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
295
238
Kaskazini mwa nchi yetu upo mlima maarufu sana wa Kilimanjaro. Chini ya milki ya mlima huo aliishi Mangi maarufu sana aliyeitwa Mandara ambapo jina lake la pili ni Rindi.

Mandara alianza kuwa Mangi wa Moshi mwaka 1855.Alikuwa Chongo hata hivyo aliweza kufanya kazi zake kiufanisi zaidi.Sambamba na hilo alikuwa na halmashauri ya wazee ,Tama(Hakimu), na Wachili(Akida) ambao walimsaidia katika majukumu mbalimbali.

Pamoja na hayo Mandara alisifika sana kwa umakini wake ,kwani hakuweza kusaini mikataba bandia ya wageni katika utawala wake.

Tutamkumbuka sana Mangi Mandara wa Moshi.
 
historia inaandikwa vipande namna hii?kachimbe data ulete historia acha utani meku.
 
Wachagga bhana.
Kila kitu kuungaunga tu...mtu haujui historia
ya mtu...unaamua kuileta kwa kuungaunga tu ili muonekane ni baabkubwa.
 
Ni Mandari kuna vitukuu vyake tulipiga nao shule

Sio Mandari, ni Mandara kama mleta uzi alivyoandika. Anapewa heshima huku Marangu mpaka leo. Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro (KINAPA) imekipa jina la MANDARA kituo cha kwanza kulala watalii wanaopitia njia ya Marangu. Kituo hicho kinaitwa Mandara hut.
 
Stry ipo ipo tu.
Alikuwa mangi wa Moshi sehem gani. Moshi pakubwa.

Kwanza, ni lazima kujua tofauti kati Moshi na Kilimanjaro. Moshi ni halmashauri na manispaa. Marangu ni sehemu ya Moshi Vijijini ambapo Mangi huyo alihudumu kiuongozi enzi za uhai wake
 
Hii ni historia kwa ufupi kwamba tusubiri inakuja nyingine au ndio full story na mzigo umeishia hapo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom