Mjue kiumbe aina ya Sisimizi

Mjue kiumbe aina ya Sisimizi

Huwa napenda wanvyoongozana wakiwa wanatambaa kwa mstari huku wakipishana wala hawakosei.

MUNGU AISEE.
 
Huwa napenda wanvyoongozana wakiwa wanatambaa kwa mstari huku wakipishana wala hawakosei.

MUNGU AISEE.
Nadhani hao ni siafu Sisimizi hawana hiyo Style
 
Unusa hata harufu zilizo ndani ya kuta za zege? Maana utaacha mchuzi mezani ndani ya nyumba yenye kuta za zege lakini hawachukui dakika nyingi kufika kwenye huo mchuzi.
hahahaha
 
Sisimizi ni kiumbe cha ajabu sana hapa duniani.

Sisimizi hupenda sana kutembea kwenye makundi makundi.

Sisimizi hutokea fasta sana ukiacha chakula / uchafu sehemu fulani. Hata ukiwa ghorofa ya 10 hapa Bongo, mwaga tu mchuzi kidogo au asali, ndani ya muda mfupi sana utaona sisimizi hao hapo.

Sisimizi huvutwa na kitu haraka sana. Sijajuaga sisimizi hutokea wapi haraka haraka ukishamwaga chakula au uchafu mahali.

Swali :

Sisimizi wanaishigi mazingira gani kiasi cha kwamba hutokea haraka sana fasta…

Sent using Jamii Forums mobile app


Tunakaa ndani ya kuta za nyumba zenu tukisubiri mtumwagie ridhiki yetu. Umeshamwaga tayari niwaite wenzangu tuje kuzoa?
 
Sisimizi ni Mdudu mwenye hisia Kali sana,
Ni Mdudu mwenye bidii na ni hodari...
Hakati tamaa kama walivyo viumbe wengine,
Analolipanga sisimizi haliwezi kurudi nyuma..
Anapoamua kufanya jambo analifanya, akiona linamshinda anaita wenzake, wenzake wakija kama linawashinda wanaomba msaada kwa Ukoo mwengine. Kama na hao pia hawatoshi. Wanaweka kambi hapo hapo na kuanza kuzaliana ili wawe wengi ili watimize malengo yako

Wana moyo wa kusaidiana kuliko viumbe wowote duniani..
Hawaogopi.. Akikasirika kitakachokusaidia ni kumsagasaga kutokana na udogo wake..

Sisimizi ni wakwanza kupata taarifa ya mizoga au vitu vitamu vilivyopo karibu ya eneo lake au hata umbali kidogo kwasababu ya udogo wake kwahiyo hata kile tunachokiona ni kidogo kwetu, kwake ni kikubwa na hata mzoga wa panya ni mdogo kwetu lakini kwake ni mkubwa na atapata taarifa mapema sana na ataufata popote ulipo atafika kwa wakati kwasababi hupita njia iliyonyooka kwa maana hakuna sehemu atakayoshindwa kupita.

SISIMIZI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisimizi wanaishi kwenye jumuia.
Sisimizi wanamgawanyo wa kazi.
Sisimizi wanauwezo wakubeba vitu vyenye uzito mara 50 ya uzito wao,
Sisimizi wanafuga
Sisimizi wanalima.
Sisimizi wanahifadhi chakula ghalani kwaajili ya matumizi ya baadaye.
Sisimizi wanapigana vita.
Makazi ya sisimizi vere complex and sophisticated

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom