Mjue jasusi Paul Kagame - Sehemu ya Pili

simba songea

JF-Expert Member
Feb 8, 2016
1,498
1,211
JASUSI PAUL KAGAME ALIEITOA RWANDA KWENYE ARDHI YA DAMU

(Simba Wa Vita Alieikimbia Rwanda Kwa Mtutu na kurudi kuikomboa Kwa Mtutu).
version. 2

Naam Baada Ya Maombi mengi kuhusu muendelezo wa Jasusi Kagame, Leo nimeona niwaletee Simulizi ya kweli ya Paul Kagame. Kuhusu vita ya Kagera nitaambatanisha humu humu ili tuelewe vizuri Maana vita ya kagera ndo ilimpaisha Kagame.

Baada Ya wamisionari wa ubelgiji kumteua msomi Gregoire Kayibanda kuwa Katibu wa Askofu na Mhariri wa gazeti la kanisa akaona hapa ndipo pa kuikomboa Rwanda. Machi 24 1957 wasomi nane wa Kihutu pamoja na Gregoire Kayibanda waliandika waraka wa Kihutu wa kudai uhuru kwa ukoloni wa kibelgiji. June 1957 walianzisha chama chao cha kudai uhuru kilichoitwa PERMEHUTU. Baada ya vita ya pili ya Dunia iliibuka vuguvugu la kudai uhuru ikapelekea wakoloni kuondoka.

Mwaka 1959 Mtawala wa Kitusi aliyekuwa akiitawala Rwanda, utawala wake ulilalamikiwa sana baada ya kuwaneemesha watusi. Hii ilipelekea Wahutu kuuangusha utawala wake. Mabadiliko haya yalifuatiwa mauaji ya takribani Watusi 150,000, Walioponea chupuchupu walikimbilia nchi za jirani na Rwanda. Ni wakati huu Wazazi wa Paul Kagame walikimbilia Uganda huku yeye akiwa na miaka miwili.

July 1962 Rwanda ikapata uhuru na Gregoire Kayibanda akawa Rais, cha ajabu alitumia Uhuru wake kuwanyanyasa Watusi na kuiendesha nchi kama familia yake. Ndipo Julai 5 1973 Serikali ya Gregoire Kayibanda ilipinduliwa na Mapinduzi haya yalifanywa na wahutu yakiongozwa na meja Jenerali Juvenal Habyarimana ambaye naye ni Mhutu. Huyu Meja Jenerali Juvenal Habyarimana alimtupa jela Gregoire Kayibanda na kufariki kwa kunyimwa msosi.

Rais Juvenal Habyarimana akafuta vyama vyote vya siasa ili watu wachape kazi, Rwanda ikatulia tuli Wahutu wakampenda wakaona hapa tumepata kiongozi. Baadae Habyarimana akaharibikiwa kwa kupenda visasi akapoteza mvuto nchini watu wakamuona Kikaragosi akashuka hadhi. Mkewe akaanzisha harakati za kuwaua Watusi wote nchini ili Wahutu wale maisha. Akaanzisha kituo cha redio na majarida nchi nzima ili watu wajitokeze kuwaua watusi. Wakaanzisha na Amri kumi za kuwaua Watusi. Kwa kifupi maisha ya Rwanda yakakosa muelekeo Wa kukimbia walikimbia na wa kufa alikufa.

Kagame nae akaanzisha redio Uganda kupambana na propaganda za mke wa Rais Meja Jeneral Juvenal Habyarimana, akiamini dawa ya moto ni moto. Dhambi ya Ukabila ikamnyima Uhuru Kagame Katika Kambi ya wakimbizi akajikuta anaishi maisha ya mboga mbele ugali nyuma mazingira machafu watu wanazaliana kama kuku maisha ya ukimbizi kwake yalikuwa magumu na yalimkera. Pamoja na yote Kagame alikuwa kichwa shuleni na alipenda sana kujifunza vitu na kuwa mwanaharakati, alivutiwa zaidi na mwanaharakati Ernest Che Guevara.

Paul Kagame mwaka 1978 aliitembelea Rwanda hakuwahi kuikanyaga nchi yake toka wazaz wake waikimbie akiwa na miaka miwili tu. Paul Kagame aliitembelea nchi hii kutokana na kukosa amani ndani ya moyo wake. Alikuwa anatafuta 'kusudi' lake la maisha. Katika kipindi hiki alikuwa amempoteza baba yake mzazi na rafiki yake kipenzi Fred Rwigyema alikuwa amepotea kusikojulikana. Kwahiyo Kagame alikwenda Rwanda kwaajili ya 'Soul Searching'. Alikuwa anataka kupata hamasa rohoni mwake ili ajue kusudi la maisha yake.

Kutokana na historia ya familia yake kuwa na ushawishi kwa kiasi fulani (baba yake ana undugu wa kikoo na mfalme Kigali na mamake ana undugu wa kidamu na malkia wa mwisho wa Rwanda). Kwahiyo hizi safari za Rwanda alizifanya kwa siri kubwa ukizingatia serikali iko makini na Watusi walio nje ya Rwanda kama wakimbizi kutokana na harakati zao za kuipindua serikali mara kwa mara. Safari hii ilikuwa na maana kwa Kagame alijenga 'Connection' zilizokuja kumsaidia baadae kwenye harakati zake.

Mwaka 1979 alifanya harakati zake kwenda Rwanda mara nyingine na safari hii hakupitia Uganda alipitia Zaire(Kongo). Kwa wiki kadhaa alizokaa Kigali alitumia mda huo kuimarisha 'Connection' alizokuwa nazo na pia kusoma hali ya kisiasa na uimara wa serikali.
Safari hizi mbili ziliamsha hali kubwa mno katika nafsi yake. Aliona kwa uhalisia mateso na manyanyaso wanayopata watusi Rwanda. Akajihisi kama ana kitu rohoni ya kumaliza mateso hayo.

Aliporejea Uganda Kagame akageuka kama mwanaharakati hivi katika kambi za wakimbizi akiwahimiza vijana wenzake kujidhatiti na kuweka mipango ya kuikombo Rwanda. Wakati huo huo rafiki yake Fred Rwugyema aliyepotea pasipo mtu yeyote kujua ni wapi alipoelekea alikuwa Tanzania katika kambi ya FRONASA chini ya uongozi Yoweri Kaguta Museveni ambao walikuwa wanaweka mikakati ya kumuondoa Dikteta Nduli Idd Amin Dadah.

Habari kuhusu mwanaharakati machachali Paul Kagame zilimfikia Yoweri Kaguta Museveni ndipo akatamani awe sehemu ya 'timu' yake ndipo Fred Rwigyema aliyekuwa rafiki wa Salim saleh ambaye kaka yake Museven. Huyu fred Rwigyema aliondoka Rwanda bila kumuaga Rafiki yake Kagame kuungana na Salim Saleh kumsaidia kaka yake Museveni kumng'oa Idd Amin. Fred ndo kwanza alikuwa amerejea Tanzania kutoka Msumbiji alipopelekwa na Museveni kupata mafunzo ya pamoja na wapiganaji wa FRELIMO juu ya vita ya msituni. Alitumwa nchini Uganda kwajili ya mambo mengi mojawapo ni kumshauri Kagame kujiunga na kikundi cha mapigano cha Museveni walioko Tanzania. Kagame hana muda wa kupoteza linapokuja suala la kazi, alihisi ile safari yake ya 'Connection' Rwanda inatimia. Akaambatana na Fred hadi Tanzania.

Sasa basi kuna mahali morogoro si vema kutaja ila nje kidogo ya mji kuna 'Espionage farm' ya siri ambapo 1978 Paul Kagame na maafisa wengine wa FRONASA walikuwa 'recruited' wakipata mafunzo ya ujasusi na intelejinsia. Nipende sema kwamba Paul Kagame ni moja ya maafisa bora na hodari kuwahi kuzalishwa na Idara yetu ya usalama wa Taifa.

Kagame amewahi kutumiwa kwenye 'High Profile Mission' lakin kubwa zaidi ni ile aliiongoza kikosi cha intelejinsia ya wapiganaji wa UNLA(Uganda National Liberation Front) vita ya Kagera.
Wapiganaji wa UNLA walikuwa zaidi ya 20,000 walikuwa ni kiungo muhimu sana cha ushindi wa vita dhidi ya Kagera.
Kuna kikao cha siri sana ambacho kilifanyika Moshi kinajulikana kama 'Moshi Conference' ambacho kilihudhuliwa na watu adhimu sana mmojawapo ni Paul Kagame.

Kwa wakati huu ambapo Milton Obote aliyepinduliwa na Idd Amin alikuwa Tanzania na kikundi chake cha wapiganaji ambacho alikiita kwa kiswahilii "KIKOSI MAALUMU" ambacho makamanda wake walikuwa Tito Okello na David Oyite Ojok hawa nao pamoja na Obote mwenyewe walikuwepo mkutanoni Moshi. Kikao hiki ndo kilizaa mpango mkakati uliotumika kumshinda Amin vita ya Kagera. Kagame ndo alibebeshwa mipango ya kintelejinsia ya Jeshi vita ya Kagera

Oktoba 1978 tukaingia vitani dhidi ya majeshi ya Amini. Licha ya swahiba wake Kanali Muammar Gadaffi ambaye alituma wapiganaji 2500 na silaha nzito za kivita kwa kipindi hicho kama vifaru T-54, T-55, magari ya kivita ya kisoviet aina ya BTR,APC na Grad, MRL pamoja na ndege za kivita aina ya MiG 21 pamoja na ndege hatari za kivita(SuperSonic Bombers) aina ya T-22 Kumsaidia Amin. Ajabu licha ya majeshi ya Amin kuwa imara kiasi hichi kutokana na silaha za kivita lakini mwanzoni mwa mwaka April 1979 tukampiga Amin mpaka "Ikulu" na kumlazimu kukimbilia Libya kwa rafiki yake Gaddafi na baadae Saudi Arabia ambapo 2003 alifariki.

Baada ya Uganda kukombolea kutoka majeshi Nduli Idd Amin Dada. Mwaka 1980 Kagame alijiunga na chuo cha mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Arusha kuchukua mafunzo ya Luteni Usu (Cadet Officer) Ofisa Mwanafunzi, pamoja na mafunzo ya ukachelo.

Ikumbukwe mwaka 1986 Museveni baada ya kuwa Rais wa Uganda akamteua kagame kuwa Chief Inntelligency Millitary(Mkuu wa Usalama Wa Jeshi) na Fred Rwigyema akala shavu la Naibu waziri wa Ulinzi. Juvenal Habyarimana Baada ya kusikia uteuzi huo aliweweseka kinyama maana anaujua fika miziki ya hawa jamaa.

Mwaka 1990 Wakati Juvenal Habyarimana akiwa Marekani Fred Rwigyema aliongoza wapiganaji 4000 wa RPF kupitia mpaka wa Rwanda na Uganda kuivamia Rwanda na kufanikiwa kuwarudisha nyuma majeshi ya serikali ya Rwanda zaidi ya Km 60 ndani ya Rwanda hadi katika mji wa Gabilo. Zilichapwa kinoma ikabaki kidogo Habyarimana apinduliwe.
Wakati wapiganaji wa RPF wakiendelea na mapambano dhidi ya serikali ya Rwanda. Paul Kagame alikuwa masomoni katika mafunzo ya juu ya uongozi wa kijeshi yaani Commander and General Staff College marekani.

Wakati mapambano yakiendelea huko Rwanda na kubaki kidogo majeshi ya serikali ya Rwanda kuzidiwa, kiongozi wa RPF fred Rwigyema aliuawa kwa kupigwa Risasi kichwani akiwa kambini inasemekana ni adui aliyemuua. Kufa kwa Fred Rwigyema kulizorotesha mapambano kwa RPF morali ya vita ikashuka. Majeshi ya serikali ya Rwanda yaliwarudisha nyuma majeshi ya RPF. Wakati huo serikali ya Rwanda iliongozwa na Jenerali Habyarimana akipewa nguvu na ufaransa wanajeshi 600.

Taarifa za kuuwawa kwa Rwigyema ziliwafikia Museveni na Kagame. Ikabidi Kagame akatishe masomo yake Kansas Marekani na kurudi vitani kuongeza nguvu. Kagame Akakuta jeshi lake halina moral tena akatumia miezi mitatu kulijenga kisaikolojia na kurudi vitani huku Kagame akiwa mstari wa mbele 'front Line' kwa mapambano. Kagame aliliambia jeshi lake "Wewe ukisema unaopigana nao ni wezi nawe ukawa mwizi sasa tofauti itakuwa wapi enhee? Wakajibu "Hakuna", "Basi inafaa bora uende huko ukawe nao, wakati ukiwa hapa vitendo havifanani na vile nilivyosema"

Nchini Rwanda jeshi la serikali lilifanya mauaji ya kinyama kwa watusi. Mwaka 1993 umoja wa Afrika na marais wa maziwa makuu wakaitisha mkutano wa maridhiano pale Arusha walikubaliana kugawana madaraka lakini wapi vita ikaendelea. Octoka 5 1993 baraza la usalama la umoja wa mataifa likapitisha maamuzi 872 kuanzisha jeshi United Nations Assistance Mission To Rwanda (UNAMIR) ili kuilinda Rwanda. Pamoja na kuwepo serikali ya mpito bado mauaji yaliendelea na Habyarimana hakuonesha muelekeo wa kuzuia vurugu.

April 9 1994 Ndege ya Rais Habyarimana ikatunguliwa na abiria wote waliokuwepo ndani wakafa. Jeshi likatangaza vijana wa RPF ndo wameitungua hivyo Wahutu wote wawaue watusi kwa mapanga, mijereji na mikuki. Watu wakachinjwa wakachinjika ardhi yote ilijaa damu mito na maziwa ilijaa maiti hata pa kukanyaga hamna. Dunia nzima ikasisimka kwa mauaji yale. Ndani ya miezi mitatu watusi milioni moja walipoteza uhai hata Waziri mkuu agath mhutu aliyepinga mauaji ya watusi aliuwawa na mume wake kipenzi hata walinzi wake kumi wenye asili ya kibelgiji nao wakateketezwa. Ikaitishwa kamati ya dharura mansele Gansinzi Mhutu wenye msimamo wa kati akateuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi. Baada tu ya kuteuliwa Masinzi akakataza Wahutu kuua Watusi, wakubwa wakachukia wakataka kumuua akawakimbia. Nafasi yake ikachukuliwa na Augustine akaendeleza mauaji.

Baada vita ya muda mrefu julai 1994 RPF wakashinda vita wakafanikiwa kuingia madarakani wakaunda serikali ya Taifa na Kagame kuwa makamu wa Rais huku kizumungu akawa Rais kushughulikia mambo ya ndani ya nchi. Ili Taifa liwe salama lazima baadhi wafe ndo ilivyotokea Rwanda.

Wakati huo wauaji wote walikimbilia Zaire na kuwa tishio kwa Rwanda maana Mobutu Sseko aliwafadhili. Mobutu na Habyarimana walikuwa marafiki hata siku chache kabla ya ndege yake kutunguliwa Habyarimana alimtembelea Mobutu akakaa Zaire kwa siku mbili akila na kunywa. April 1994 Habyarimana alielekea Dar es salaam Tanzania kwenye mkutano wa wakuu wa nchi. Baada ya mkutano alianza safari kurejea Rwanda na dege lake la kibabe lenye thamani ya bilion 45 aliyopewa zawad na Ufaransa. Wakat wanatua Kigali Airport Rwanda ndege yake ilitunguliwa na watu wote waliokuwa ndani wakafa pamoja na Rais wa Burundi nae alikuwemo akafa.

Mpango wa Mobutu ulikuwa kuirudisha Rwanda mikononi mwa Wahutu ili amzike kiheshima rafiki yake. Muda wote huo alikuwa na maiti ya Habyarimana ndani hata sijui aliipataje.

Ikabidi Kagame kwa kushirikiana na Museveni kumfurusha Mobutu. Siku moja kabla ya Mobutu kutimkia Zaire Aliichoma moto maiti ya Habyarimana na kutimka na majivu, alikaa na mwili kwa miaka mitatu.

Rais Bizumungu alitofautiana na Kagame kwa kulinda wala Rushwa na wakwepa kodi. Mwaka 2000 akaamua kujiuzuru na Kagame kuwa Rais
Mpaka leo. Bizumungu akaanzisha chama chake cha siasa lakini kikafutwa mara moja kwa tuhuma za kuivuruga nchi. Bizimungu alikuja kufungwa kwa tuhuma za kuvuruga nchi na rushwa alitoka jela 2007 kwa msamaha wa Rais Kagame. Kagame aliona Bizumungu anamchelewesha kufikia dira yake ya maendeleo akaamua amfunge. Mimi nahisi kama huyu Bizumungu zingekuwa zile enzi za Kagame muda wote yupo msituni angemuulia mbali, maana jamaa hana mchezo kwenye operesheni zake.

MUHIMU: Kagame wakati anaisadia Tanzania kumuondoa Idd Amin1979 pia wakati ana msaidia Museveni kuwa Rais 1986 hakufikisha hata miaka 30. Alifanya haya yote ili awe nguli kwenye medani ya vita ili wakati ukifika aikomboe Rwanda dhidi ya Majeshi ya serikali Alikubali maisha yake yote yapotee afe ila Nchi yake iwe salama. Hili ni funzo la kweli kwetu vijana. Kupoteza kila kitu nchi iwe salama, maana binadamu tutapita ila Taifa halitapita.

NOTE: katika kujenga nchi Kagame alitafuta wataalamu wa maendeleo toka China, Singapore, na Thailand ili kuifanya Rwanda ya kisasa. Tunapoongea Mpaka sasa Rwanda hamna makazi holela wala duni. Hamna shida ya umeme.

NYONGEZA : Huyu ndo Kagame Simba wa vita asiye thubutu kuona Mtu yeyote anaitishia amani Rwanda. Haogopi mabeberu alishawahi kuwajibu mbovu wazungu baada kuona wanataka kuingilia utawala wake. Aliwaambia nyinyi ni nani who are you. Afrika nzima iliogopa kwa kauli hii ya Kagame.
FB_IMG_1577107548303.jpg

=====

Mjue jasusi Paul Kagame
 
View attachment 1301440

=====

Mjue jasusi Paul Kagame
Mpe credit THE BOLD
Umecopy na kupaste.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kagame Yuko vizuri.Historia imetulia alikuwa focussed hasa.Angekuwa mwingine alizopewa cheo kikubwa jeshini Uganda and Tula tu kuwa Sasa ne kuku kwa mrija na familia yangu

Lakini akajitoa muhanga kukomboa Rwanda .Historia I'm Ni impress nadhani Ni vizuri aandike kitabu

Huyu kagame ni.modern che guavera wa Afrika na mzalendo wa kweli kwa nchi yake

Sikuijua Historia yake vizuri .Lakini baada ya kusoma nimwelewa vizuri Sasa Kama shujaa wa Afrika aliye hai .
 
Back
Top Bottom