Mjue huyu jembe Gary McKinnon

Mjue huyu jembe Gary McKinnon

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Habari za mchana, nitawaletea kidogo habari za mwanateknolojia aliyeitingisha jeshi la Marekani pamoja na serikali kuanzia mwanzo wa mwaka 2000.

Gary McKinnon ni nani haswa? Huyu ni mtaalamu wa masuala ya teknolojia na mpaka sasa inadaiwa ndo mdukuzi hatari zaidi kuwahi kuweka serikali mahala pabaya tena serikali kubwa kama Marekani. Alizaliwa mwaka 1966 tarehe 10 mwezi wa Februari.

Je alifanya nini haswa?

Huyu jamaa aliingia katika mfumo mkuu wa jeshi la Marekani yaani mfumo wote uliounganisha kompyuta zote za jeshi pamoja na ule wa NASA. Kuanzia kipindi cha mwaka 2001 mwezi wa Februari mpaka mwaka 2002 Machi alidukua taarifa za kompyuta zaidi ya 97. Alitumia jina la Solo" na alitumia jumla ya miezi 13 tu kuweza kufanya wizi huo wa taarifa.

Na aliweza kuingia ndani ya mifumo yao kama yeye ndo administrator yaani ndo mwenye mfumo wa kompyuta hizo.

Usalama wa Taifa la Marekani walianza kugundua shida ya mitandao yao pale ambapo huyu mwamba alizima mfumo wa kompyuta zaidi ya 2000 kwa masaa 24. Na alipoziwasha walikuta maneno haya "Your security is crap" kutoka kwa solo yaani bwana Gary McKinnon. Baada ya tukio la Septemba 11 mwaka 2001 huyu mwamba alifuta takwimu za silaha za kijeshi katika kituo cha Earle Naval Weapons, lakini pia aliingilia mawasiliano ya mtandao tena wa kijeshi wa kompyuta zaidi ya 300 na kuzifanya ziwe zito katika kuwasiliana hivyo kupelekea silaha za jeshi kufika zikiwa zimechelewa huko katika kambi ya Atlantic Fleet.

Kushikwa kwake:

Bwana Gary alifanikiwa kushikwa mara baada ya timu ya wanateknolojia kutoka katika kikosi cha Taifa cha UK National Hi-Tech Cime Unit kufanikiwa kupata eneo linalosadikiwa kuwa ndo nyumba ya mchumba wake Gary kuwa ndo laptop ya Gary ilitumika katika kufanya mambo yote hayo. Alihoji na polisi tarehe 19 mwezi Machi mwKa 2002, baadaye alihojiwa tena na kikosi hicho cha NHTCU, na baadaye bwana huyu aikubali kuwa alifanya hivyo kwa sababu zake.

Sababu ya kwanza, ilikuwa ni kwa ajili ya kuangalia teknolojia pamoja na taarifa ambazo zimefichwa Katika uso wa dunia. Hasa hasa tuhuma za kuwepo kwa Aliens pamoja na Nuclear testings.

Sababu ya pili, ni kwamba alikuwa anawaonesha vulnerability ya mitandao yao, kuwa ipo dhaifu, na aliwaonesha dhahiri pale alipozima mfumo wa kompyuta 2000 kwa masaa 24.

Mwisho.

Mwaka 2002 mwezi wa Novemba bwana Gary alisomewa mashitaka saba yanayohusiana na uhalifu wa teknolojia kupitia kompyuta, na Mahakama ya Eastern District of Virginia, na kila tuhuma ilibeba miaka 10 jela. Na kama mahakama ikimkuta na hatia basi Gary angekutwa na adhabu ya miaka 70 jela.

Kesi hii iliingia mgogoro kwani Gary sio Mmarekani ni Mwingereza na pia mifumo yao ipo tofauti, hivyo Uingereza haikuwa tayari kuona raia wao anashitakiwa akiwa Marekani, ilifika mpaka sehemu Uingereza akajaribu kutumia vifungu vya sheria ambavyo kwa uingereza vinafanya kazi ila sio kwa Marekani. Na ilichukua zaidi ya miaka kumi kwa huyu bwana kupata uhuru kwani bi Theresa May alifanya kila liwezekanalo ili huyu bwana akwepe kifungo hicho.

Na mwaka 2012 bwana Gary McKinnon aliachiliwa huru kutokana na kuwa na ugonjwa wa Asperger's Syndrome uliotokana na msongo wa mawazo pia msaada kutoka kwa wabunge wengi wa bunge la Uingereza waliopitisha mswada uliomlinda yeye katika haki za binadamu. Rejea hapa (My son Gary McKinnon has won justice at last | Janis Sharp).
Niishie Hapo kwa leo.

Asanteni sana I Stand to be corrected anywhere.

Unaweza kurejea hapa.
Gary McKinnon reveals detail on NASA data breach and ‘extraterrestrial life’
Gary McKinnon - Wikipedia

Gary McKinnon - RationalWiki
Mshana-jr Malcom-lumumba na wengine.

Sent using Infinix hot 4
 
Sehemu niliyoonesha Kua alikuwa anatumia kuingia katika mfumo wao. Ni chumbani kwake alipokuwa anaishi pamoja na nyumba ya shangazi yake na mchumba wa Gary McKinnon. Thats all sio kwamba alikuwa yupo Marekani ndo akaweza kufanya udukuzi huo. Hapana nisamehe kama nimekupoteza mkuu. Hacking inafanyika sehemu yoyote yaani mtu wa Tanzania unaweza kufanyiwa udukuzi na mtu aliyeko hata China.


Sent using Infinix hot 4
 
Daaah hatare sana


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Jaribu kucheki documentary yake

Sent using Infinix hot 4
 
Jamaa aliweza kuingilia mifumo ya jeshi la Marekani pamoja na NASA akadukua taarifa alizozitaka alafu bado mnatuaminisha jf tuko salama?

Maendeleo hayana chama
 
Jamaa aliweza kuingilia mifumo ya jeshi la Marekani pamoja na NASA akadukua taarifa alizozitaka alafu bado mnatuaminisha jf tuko salama?

Maendeleo hayana chama
Mkuu, huwa unaamini?
 
Back
Top Bottom