Mjue "Christopher dudus" Yesu wa Tivoli Gardens Kingston Jamaica

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,189
9,298
wakuu habari

leo ningependezwa kama tungemjadili mfanyabiashara maarufu toka viunga vya magharibi mwa kingston Jamaica

si mwingine bali ni christopher dudus coke mzaliwa wa Jamaica huku akiwa amezaliwa katika familia ya watoto wanne, yeye dudus na kaka zake wawili na dada yake ambao nao waliuwahi kuwawa kutokana na visa vya serikali
Baba yake ambaye alikuwa anaitwa Lester au maarufu kama Jim brown alikuwa anatafutwa kipindi kirefu cha maisha yake na serikali kutokana madai ya kumiliki genge la mihadarati(drug cartel) lililoitwa shower posses ambapo jina hilo lilitokana na madai ya kuwamiminia risasi watu zaidi elfu moja miaka 1980.lakin alifariki mwaka 1992 kwa moto baada sero aliyokuwa amehifadhiwa kusubiri kupelekwa US kujibu mashtaka ya kuuza madawa ya kulevya kuungua

Kwa mujibu wa serikali ya marekani dudus alirithi biashara aliyokuwa anafanya baba yake iki ni pamoja na biashara ya kampuni za ujenzi na burudani
mara kadhaa mwanasheria wake Tom Tavares Finson alinukuliwa akisema mteja wake ni mfanyabiashara na wala hajihusishi na biashara za mihadarati

Dudus alifanikiwa kujiingiza kwenye siasa za jamaica kwa kupata ushawishi ndani ya chama tawala cha Jamaica Labour Party chini ya waziri mkuu wake Bruce Gordin

Dudus "YESU" wa jiji la kingston kwenye viunga vya Tivoli garden vilivyopo magharibi mwa jiji hilo alikuwa ni mtu mwenye ushawishi uliopindukia kwa jamii inayomzunguka.huku akiwa mstari wa mbele kusomesha maelfu ya wajamaica kwa kutumia pesa zake, ni dudus pekee ambaye alikuwa bingwa wa kuchangia pesa nyingi kwenye shughuli zote za kijamii zilizofanyika Tivoli Gardens huku akiwa mstari wa mbele kuhakikisha watu wa Tivoli wanaishi kwa raha mustarehe kwa gharama zake.

Serikali ya marekani ikaanzisha msako wa kumsaka dudus kwa gharama zozote zile
kwa kile kilichoaminika ni muuzaji mkubwa wa dawa za kulevya katika ukanda wa latin America caribean america hadi uk. ndipo kwa kushirikiana na vyombo vya usalama vya jamaica wakaanzisha msako uliodumu wiki nzima kumsaka dudus ndani ya Tivoli huku vikosi vya serikali vikipata upinzani mkubwa toka kwa wananchi walijidhatiti kufa kwa ajili ya kumuokoa dudus wao. ambapo vijana wa jiji la kingston walishikamana kuhakikisha wanapambana na majeshi lakin sio dudu akamatwe kwani nao walijidhatiti na silaha za kivita kwa ajili ya kumlinda YESU wa Tivoli Gardens.
Hadi muda huu "Coke" yuko gerezani anatumikia kifungo chake cha miaka 23 ambapo alihukumiwa mwaka 2010 huku akiwa ameacha mali zinazokadiriwa kufikia dollar za jamaica milion 300.


asanteni

imeandaliwa na

falcon mombasa
 
unrest in tivoli
 

Attachments

  • IMG_20170406_204617_463.JPG
    IMG_20170406_204617_463.JPG
    17.3 KB · Views: 140
  • IMG_20170406_204455_861.JPG
    IMG_20170406_204455_861.JPG
    31.2 KB · Views: 134
  • IMG_20170406_204512_200.JPG
    IMG_20170406_204512_200.JPG
    15.8 KB · Views: 133
  • IMG_20170406_204541_125.JPG
    IMG_20170406_204541_125.JPG
    20 KB · Views: 174
  • IMG_20170406_204557_981.JPG
    IMG_20170406_204557_981.JPG
    24.6 KB · Views: 168
  • IMG_20170406_204651_832.JPG
    IMG_20170406_204651_832.JPG
    18.2 KB · Views: 122
  • IMG_20170406_204707_118.JPG
    IMG_20170406_204707_118.JPG
    26.2 KB · Views: 136
  • IMG_20170406_204726_372.JPG
    IMG_20170406_204726_372.JPG
    16.8 KB · Views: 128
Ukifuatilia kisa cha Pablo e scoba wao ndo wamepelekea kifo chake ukifuatilia kisa cha Guzman wao ndo wamepelekea kifungo chake na huyu dudus pia wanahusika ...Inamana wao ndo wanajua kupigana na madawa ya kulevya ??? Au marekani hakuna matajiri wanaoingiza ngada ??
mi ninachojua wao hawataki drug dealer waharibu watoto wao, na hao drugs dealer hawapo ndani ya USA kwa mujibu wa maono yao
 
Kwa hizi comments zako unaonesha upeo wako ni wa chini then umekuwa crowded na chuki. Ukijawa chuki uwezo wa kufikiria unakufa. Unabak unaumia wakat unayemchukia haathiriki kwa lolote.ungeelimika kidogo tu ungetoka kwenye ukungu ukaelewa vita ya madawa ya kulevya ikoje

Kwa wema Gani waliokua nao ??? Nawachukia sana Hawa jamaa .
 
Kwa hizi comments zako unaonesha upeo wako ni wa chini then umekuwa crowded na chuki. Ukijawa chuki uwezo wa kufikiria unakufa. Unabak unaumia wakat unayemchukia haathiriki kwa lolote.ungeelimika kidogo tu ungetoka kwenye ukungu ukaelewa vita ya madawa ya kulevya ikoje
sasa tupe somo mkuu tujifunze kwa pamoja
 
Ndani ya Marekani hao drug dealers wapo ila wasichotakakuona ni drug dealers wa nje kutakakulidhibiti soko lao. Na wao ndio wanaofadhili izo operation za kukamatwa au kuuwawa kwa wenzao wa Latin America. Refer to Ignacio Nacho wa SINALOA CARTEL..
 
Ndani ya Marekani hao drug dealers wapo ila wasichotakakuona ni drug dealers wa nje kutakakulidhibiti soko lao. Na wao ndio wanaofadhili izo operation za kukamatwa au kuuwawa kwa wenzao wa Latin America. Refer to Ignacio Nacho wa SINALOA CARTEL..
mi naona unaongea propaganda
 
Back
Top Bottom