Mjomba kasusa...

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Enzi zile ambazo hata mawasiliano ya simu au barua hayakuwa rahisi, ilikuwa haipiti mwezi bila kupokea mgeni kutoka kijijini kwetu na mara nyingi ni ndugu wa mbali na karibu ambao wengi wakija wanasema wanapita kwenda sehemu na wameelekezwa tu nyumbani (kijijini) wafikie kwetu au pengine kama ni ndugu wanasema "wamekuja kupumzika tu, kilimo kigumu huko kijijini".


Wakati ule ilitulazimu sisi watoto kutoka vyumbani na tulale chini sebuleni au barazani ili kupisha mgeni . Hali pia hata ya chakula ilikuwa ngumu kwani kipato cha mzee hakikuwa njema sana hivyo hata kama ilikuwa ratiba ya nyama na "mpunga", ilibidi tuhamishiwe kwenye "ugali wa dona" na maharagwe au "dagaa wa Mwanza" ili kujibana kwa ukubwa ule wa familia(ni zile enzi za sera za uhujumu uchumi).

Mara zote utakuta hata wakiwa wanaondoka ilimlazimu mzee wape nauli kwani siku hizo walidai hata nauli ya kujia walikopa huko kijiji. Hali nilidhani itabadilika baada ya Mzee kustaafu na kurejea kijijini, ambapo hata hivyo alikuwa akiishi kwa kuchekwa na wanakijji kuwa amechezea maisha akiwa kazini mpaka imembidi arudi shoka mbaya huko kijijini utadhani hakufanya kazi.


Wajibu wa kuhudumia ndugu ni kama uliahmia "automatic" toka kwa wazazi na kuja kwetu watoto baada ya wao kuzeeka. Nikiwa bado sijaoa, mjomba alizoe kuja toka kijiji akiwa na biashara ya kule "koroboi" kwenye soko kubwa ambapo aliuza kwa jumla kupitia madalali. Kwa kuwa nilikuwa na vyumba viwili vya kulala alikuwa akilala katika moja ya hicho chumba.

Hata baada ya kuoa, Mjomba aliendelea kuja tu....sasa Mungu katujalia na Mke wangu tuna watoto wawili. Hivi karibuni Mjomba alikuja na cha kusikitisha alikuja na mwanamke ambaye anadai ni "shangazi mdogo" (mimi sikuwahi kumwona wala kusikia).

Kwa kuwa chumba alichozoea kufikia Mjomba walikuwa wakilala watoto na isitoshe hakina "ceiling board", baada ya kujadiliana sana mke wangu tulikubalina kuwa kwa heshima, labda nimuulize kama mjomba atakubali ulala sebulani na huyo "shangazi" alale na watoto chumbani au vipi tuwatafutie nyumba ya kulala wageni (gesti)

Baada ya kumweleza Mjomba , alikuja juu kama mbogo akidai kuwa yeye hawezi kutenganishwa na mkewe na kuwa uamuzi wa kumtafutia gesti ni kumdhalilisha sana kwani yeye hajawahi kulala gesti hata siku moja na mkewe katika maisha yake wakati yupo karibu na ndugu. Ailidai kuwa kama ni kutafuta gesti basi angefanya mwenyewe na sio sisi watoto tumtafutie yeye akalale na mkewe huko...

Akiwa na hasira kali , jioni hiyo hiyo alikusanya mizigo yake na huyo "shangazi", na pasipo hata kuaga akatimka zake na siku iliyofuata tukatapa taarifa kuwa alitafuta ndugu wa kwetu alikuwa akimfahamu akaenda kulala kwake na kusimulia kisa kuwa sisi tulimfukuza na kuapa kuwa kamwe hatakanyaga tena kwetu kwa dharau zile tulizomwonyesha mbele ya mkewe....
 
sitaki kabisa kukaa na ndugu kwa sababu hizo hizo, ukimweleza ukweli atakwambia unaring na kwenda kukutangazia kwa ndugu wengine kuwa umemnyanyuasa
 
Pole ndugu ndo maisha hayo, tupo wengi katika kundi lako.

Yani haya mambo ya extended family yanabore sana. imagn una 2rooms, una watoto2 na housegirl juu, unaletewa watoto 2wa mojmba wasichana wakubwa wa kusoma secondary hujakaa sawa shangazi nae anataka kuleta na ukikataa ndo unachukiwa na ndugu wote. Jamani kwann tunawazibia wenzetu maendeleo maana yani hapo salary yote inaishia chakula bado siku wakiondoka wanaenda kukutangazia mabaya.
 
jamani hawa ndugu wana viroja ..pia mie huwa nashangaa ndugu anaweza jua kabisa una chumba kimoja bado anakuja na dalili za kuondoka kurudi kwake hazionekani na kumuuliza unaondoka lini inakuwa ngumu...
Hili ni tatizo na mpaka leo lipo.
 
Nchi yetu bado haijaendelea ila how can we avoid extended family? maana hata ww unaweza kufa ghafla au ukafa wewe na mkeo watoto wenu wakawa extended family kwa ndugu zenu. Ni tatizo la nchi zote zinazoendelea sio TZ tu, cha muhimu ni kumuomba Mungu akupe uwezo ujenge nyumba yako na kuwekeza kwa familia yako ili waweze kusimama pindi ambapo haupo.
 
Kwa usawa huu wa maisha ya kimbayuwayu...............
Shukuru Mungu mjomba kasusa!!!
Mungu akupe nini tena?
 
Shida ya utegemezi inakuwa kama kufungiana nira.

Kama ukiwa kijijini na unauwezo kwa kimaisha hata kuliko wale wa mjini, bado unadhani wewe huna uwezo. Cha kusikitisha bado utaishi kwa kutaka ufanyiwe vile unavyoona mtima wako unafurahi pasipo kujua mwenzio anaumia vipi ili kujaribu kukukwamua.

Ukiwa huna kazi ya elimu, hata kama upo mjini na unavyanzo vyote bora vya maisha, daima una amini kuwa wale wenye kazi ya kisomi ndio wenye wajibu wa kusaidia ndugu. Hata shida ya jumla ikitokea wewe unakuwa mwepesi kusema, wache wasomi watatatua...na ikiengemea kwa yule mwenye moyo, siku zote inazidi kula kwako hata kama una kipato kidogo.

Wapo wazazi na ndugu wa karibua ambao pia walikwisha fanya kazi, wanajua maisha yalivyo lakini unapojaribu kuwasaidia hata kwa kidogo au ukisema huweiz, wanakuwa wakali kama nyuki na kuona hufai kabisa.

Kuna tabaka jingine la wale ambao waweza kuwa ni ndugu au rafiki wa karibu, utamwonea huruma umasaidie, lakini inakuwa ni kama umempiga gamzi ya ulemavu wa akili. Itakuwa hata kununua mswaki wake ni shida kuu, lakini kama utaamua kuishi nae, hataki kufuata kanuni za jumla,anataka kujiamulia kila kitu kuanzia chakula, muda wa kulala, kazi za kusaidia nk. Ukimuonya, inakuwa ndo kisa hata kama uliishi nae miaka kumi ya wema, yote itafutika siku moja.

Kuna hawa wengine ambao hata kama yupo nje ya nchi, yeye kwake ni fahari kusema "ndugu yangu ni fulani" na atakuwa mwepesi kukusifia kwa kila jambo, hata akipata zake hawezi hata siku moja kusema anunue kibaba cha unga wala soda kuwapa watoto. Ukimjulisha labda siku umeishiwa kama anazo asaidie anakujibu "toka lini bahari ikaazima maji kisimani"...

Wapo wale ambao hawaridhiki kabsaaa na kile anachopewa, hajui una nini lakini ukimpa anapokea na badae utasikia mtaani miji neno kuwa hata kama yeye ni masikini hawezi kupewa msaada wa namna hiyo. Hili ni tabaka la wale ambapo yupo tayari kupokea nguo za ndani za mzungu akaziita mtumba kuliko kumvulia suluali au gauni lako atasema unampa makombo ya nguo na umemdharu..

Upo utegemezi mwingine ambao tunajitakia, kwa mfano mmekubalina na mwezio kumwitisha mdogo wako aje toka mjini ili asome na pia kuwasidia sehemu ya majukumu...baada ya muda, mwenzio nae anasema tumwitishe na mdogo wake wakati akiona kabisa hata pa kulala hakuana...inakuwa sasa ni kisa cha mvutano katika ndoa...Na hawa ndugu wakija, paengine huwa hata lile walilojia hawataki kufanya, ukiwatuma hata kazi ndogo tu wanajibu wao si ma-house boi/house-girl...wanataka kuwa na amri kila eneo kuliko mwenye nyumba.

Wapo wategemezi wangine ambao hatuwezi kuwabainin kirahisi, ni hawa ambao wanataka kila siku tuwe nao kwenye starehe nk. Lakini hata akiwa na kitita chake mfukoni, hawezi kutoa hata senti kununua soda..yeye kila siku hana tu....(aweza kuwa mume, mke, rafiki wa kike au kiume).
 
Atawasalimia kupitia mobile phone.
Mambo ya utandawazi haya!

au kama hana salio atatuma e-mail, na wakitaka kuja wanitaarifu kabla ili nijiandae sio kuvamiana, na aseme anakaa kwa muda gani ili niweze kupanga bajeti, life la sasa limebana sana
 
Back
Top Bottom