Mjikumbushe Mzumbe High School

Mliopita pale miaka ya tisini mwishoni mnamkumbuka mama Karen Scheiffer Mtaalam wa Maths?
Miss.Emma White Physics
Mr.Luku Inorganic Chem huyu alikuwa mdau wa arsenal.
Hivi kina Mwl.Msabila,Mutawajibu,Msuka na wengineo wako wapi.
R.I.P Wibonele
 
Kumbe ndio maana mkuda....watu wa Karume wengi walikuwa "vimatu" na kutoka kanda ya ziwa! LOL

..acha acha kabisa wewe,karume kwa wajanja kule sio mkwawa na mirambo yale mamiti nilkuwa naona kama giza sana na walimu wote wako karibu,karume/shabaan Robert ilikuwa ukijificha hata kama mwalimu anakuja basi utamuona kwa mbali sana,hivi mwalimu chacha,hussein na yule mganda wako wapi?
 
Duh! Mkwawa namba ngapi mzee? miaka hiyo area captain Mkwawa alikuwa Erasto Ngonyani, katibu Kingwala (sio Kingwaba) na Mwl wa kijiji Kuboja...unoko unoko tu na ushindi wa usafi ni lazima. Mvua ikinyesha halafu ukachoma bwenini na viatu, lazima watu wakugombanie....

Unakumbuka "sumu"/pieces/mihogo ya kuchemsha kwa wale wamama pale jirani...!?

...unanikumbusha mbali sana wewe,erasto yuko wapi? nasikia kingwaba ni Dr siku hizi na kuboja nasikia alienda kusoma IDM...huko mkwawa nawakumbuka kina Kafura,Elangwa,ndayo,edward etc sijui wako wapi?
 
Duh! Mkwawa namba ngapi mzee? miaka hiyo area captain Mkwawa alikuwa Erasto Ngonyani, katibu Kingwala (sio Kingwaba) na Mwl wa kijiji Kuboja...unoko unoko tu na ushindi wa usafi ni lazima. Mvua ikinyesha halafu ukachoma bwenini na viatu, lazima watu wakugombanie....

Unakumbuka "sumu"/pieces/mihogo ya kuchemsha kwa wale wamama pale jirani...!?


Namkumbuka Erasto Ngonyani sana tu na ile mihogo ya kuchemsha wakati wa break!! Nilikuwa no. 5 na Diones Majogo, Jonas n.k Namba nne kulikuwa na kina Axel (mwenyekiti wa starehe)..kipindi sana!!


Erasto ni dokta, Kafura ni dokta, Elangwa nilikutana nae loooooooooooooongtime ma-mid west huko, Ndayo na Ed sijui wapo wapi!! Unamkumbuka yule "Okonkwo," na Giatas (Chris) walikuwa wanakuja sana mitaa ya kati kumtembelea Kafura....

Giatas si wakili siku hizi? Mnamkumbuka Ndesa?
 
Namkumbuka Erasto Ngonyani sana tu na ile mihogo ya kuchemsha wakati wa break!! Nilikuwa no. 5 na Diones Majogo, Jonas n.k Namba nne kulikuwa na kina Axel (mwenyekiti wa starehe)..kipindi sana!!

Jamaa huyo kwenye blue, kabla hajapinduka kurudi bongo, nilikuwa nakutana nae kwenye viminuso vya kibongo huko mid west!
Giatas si wakili siku hizi? Mnamkumbuka Ndesa?[/QUOTE]

Machoman ni vigumu kidogo kumsahau........
kijana kwa kuzamia minuso hujambo......
Erasto ni dokta, Kafura ni dokta, Elangwa nilikutana nae loooooooooooooongtime ma-mid west huko, Ndayo na Ed sijui wapo wapi!! Unamkumbuka yule "Okonkwo," na Giatas (Chris), walikuwa wanakuja sana mitaa ya kati kumtembelea Kafura....hiyo ilikuwa late 90's!!
Taratibu taratibu jamani.....
 
Erasto ni dokta, Kafura ni dokta, Elangwa nilikutana nae loooooooooooooongtime ma-mid west huko, Ndayo na Ed sijui wapo wapi!! Unamkumbuka yule "Okonkwo," na Giatas (Chris), walikuwa wanakuja sana mitaa ya kati kumtembelea Kafura....hiyo ilikuwa late 90's!!
ndayo si yule jamaa mrefu na pua ya kuchongoka alienda PCM Pugu?
 
Umfanyie DRE?, kwani ww ni Dr specialist wa njia ya haja kubwa (proctologist)?
 
Aaaaaah wewe ulivyoweka picha ya Irene Uwoya nani kakwambia taratibu!? Au unadhani wote tumefurahia? Hao washkaji kuna hata mmoja unayemjua na kakulalamikia kuwa jina lake limewekwa hapa au ndio kutaka kwako masifa kama kawaida....??

Unaboa sana...grrrrrrrrrrr!!
Dogo Irene celebrity.....punguza munkali kijana wewe mbona uliniita rasta kwa kujifanya unanifahamu.......mimi sipendi sifa kijana kama sifa napenda kwa wazazi wangu basi.

Nahisi unataka nikufanyie DRE (digital rectal examination), maana naona unanifuata fuata sana....!! I will siku tukikutana tena bila gloves.....
Poa wee si dokta muosha huoshwa kama ulifanyiwa ukaki feel kitu basi poa
 
Hey Wazumbe! bado mnaikumbuka CHENG'? Na ADNYA? Mnawakumbuka Mwl Abood (Bus) & Mkhomboti. Hivi sasa wapo wapi na wanafanya nini kama wapo hai.

I was among the LAST normal A-Level students (as today we have SPECIAl students).
 
Nilisikia kuwa mwl Mkhomboti alifariki kama miaka miwili au mitatu iliyopita huko Marekani.
 
Hebrew am very sorry to hear that. Nani ana taarifa zaidi kuhusu hilo, ingaa ilisemekana ni yule mwanaye ailiyekuwa na tundu kwenye moyo (orifice ovale). Plz mwenye maelezo sahihi ayamwage jukwaani.
 
...yule housegirl wa Muyenge alikuwa ni issue kubwa,Minja mnoko na diploma yake ya kufundisha form two yuko wapi? hope na majivuno yake alienda kusoma degree,kideo cha jmosi cha mama Muyenge nakikumbuka sana ila mimi nilikuwa mtaalam wa kushuka IDM kila week..mnamkumbuka dereva wa lori la shule (Morris)?
 
Walahi, mmenikumbusha mengi sana. Kuna jamaa kweli wanaoneka mjini lakini wengine wengi hawajulikani walipo. I hope through this forum tutaendelea kujuzana na kuwasiliana kwa zaidi ndani ya JF.
 
Bila shaka Wana Mzumbe mpo hapa JF, nimetumwa kuwakumbuka wafuatao John Mongela, James Bwana, Michael Thomas Sebastian Sarota, Hassan Rajab Hassan, Patrick Maleva, Anderson Segereti, David Black, Obed Mwakitalika, Clement Mwashambwa, Kwela Mgaya, Theophil Alexander, Njaule Mdendu, Johnson Jasson, Sollomon Shati, Obed Msenga, Charles Nakembetwa, Gideon Mandesi, Isaac Kassanga, Dereck Kassanga, Deus Changala, Timilai Sheshangali, Shemaghembe Ntulwe, Sainet Katulunga, na wengine wengi sana. Waliosoma pale mmeombwa kuongezea majina ya wale mnaowakumbuka.

Kaka wewe umetaja list ya siku nyingi sana hii!!!!
ila kwa miaka ya 2000,sisi tunaweza wakumbuka
Peter Nalitolela,Sunday Dominic,Lusekelo kibona,Rogers Bhalalusesa,Nyantamba,Ungu Ramadhani,Wahab Mohamed.Emil Patrick,Spencer Sanjawa,William Maro,Baraka Daudi,Stephen Kazi,Hamad Juma,Simon Monko,Mathias Monko,Mkata Nyoni,Paschal Magesa,Emmanuel Kimbe,John Sichilima,Alex Kapungu,Wilhad Bilalo,Fredrick Lymo,Moses Kwabi.
ukija kwa Olevel walikuwa vijana balaa pale akina Erick Kabuka,Mathias Monko,Masudi Kisamfu,Stanley Kafu,Latif Amars,Rizik Lameck,Juma Mbega,Frank Andrew Mwakyembe,Idd Davis,David Mwasota,Lusungu wangilisasi,Patrick N.Sungura,Mafuru Kulwijira na wengine wengi sana miaka ya 2000 hiyo.
walimu wengi walihama shule na kupata Kuwa ma-Head Master shule zingine ila Minja hadi leo yupo.
 
Ni furaha kubwa sana kurudi tena kwa mara ya pili ndani ya Jamii Forums, nilipolala i felt Memory ikianza kupata moto nami pia nimekumbuka baadhi ya majina ya Waalimu na Wanafunzi - Ignatus Nangawe, Wabu Matipuka, James Lugembe "Shoka", Francis Mataula, David Magwila, Erasmus Dennis Buberwa, David Athuman "Mchanifu", Kassim Msami, Rodrick Mpogolo, Emmanuel Mahimbo, Geofrey Mhando, Nuru Ndile, William George, Andrew Wawa, Faustine Mduda, Kigobanya, Obed Kayawaya, Peter Billa, Ekwabi Mijungu, Edson Makallo, Joseph Mathias, Paul Kitaly, Mdenye, Mdede, Lemuel Kilallo, Cretus Peter Mnyanga, Lucas, Christopher Shemahonge, Crystogonius Masusu, Wanini Athuman, Kashenge Kimario, Collins Lutenge, Francis Mbenjile, Mussa Sadock, Zhao Ngesile, Baraka, Zephania "Church Man", Abdallah "Mtoto wa Mzinga - Jeshini", Chalesi "Kinara", Shilinde Nzweke, Enock Ndezi "Bob Ndezi", Simon Pasua, Kigume, Ralph Meela, Nolasco Paul Mbepera, Dotto Andrew, Richard Mshyota, Shukuru Basana, Augustine Karadoga, Lupindilwa Luchagula Mulula, Mjusi, Kumalija Mbingu, Mchome, Gilman Nyamubi, Watson Nsaji Mwakyusa, Hanzen Sanga, Phineas, Kinara Maswaga, James Msalika, Nehemia Kamalango'mbe. Majina mengine yanakuja halafu yanapotea kwani ni miaka mingi sana toka mwaka 1991 ni takribani miaka 19 sasa!.

Waalimu - Mwl. Mgonde, Mwl. Chimile (RIP), Mwl. Mikapagalo, Mwalimu Ndiva, Kulikuwa pia na Mwalimu asiyeona jina limenitoka, Head Master

Bagenda, Headmaster Kihawa na Mkewe alikuwa Nesi pale Dispensary.[Headmaster huyu katika zunguka yangu kutafuta mlo alikuwa Wiza Schools - Mbeya ofcourse kama Headmaster, Mwl. Mlelwa mara ya mwisho nilimuona huko Handeni kama Headmaster wa Handeni Secondary
School. Jamani kuna Mwalimu pia jina limenitoka tuliambiwa alikuwa msanifu wa Wimbo wa Shule - "Shule Yetu Mzumbe yasifika sana........,
Malezi ya Mzumbe ni Kimilifu ya Kitanzania........, Elimu ya Mzumbe........ nakuendelea, Mwl. Minangi.

Mganga wa Shule - Jina lake lilikuwa Maganga? Sikumbuki vizuri.

Tulikuwa na Gazeti la Wanafunzi wakora kule ****** - shule ambapo Waandishi na Wachoraji Mahiri walikuwa wanatoa habari nyeti na motomoto kuhusiana na matukio mbalimbali yaliokuwa yakitokea pale shuleni. Katika safari ya maisha kuna wengi ambao tayari wametangulia mbele ya Haki:
1. Raphael Mwatwinza.
2. Conrad Dustan Mnywambele "Sauti ya Kamachumu".
3. Nijimbele Gideon.
4. George Sindani.
5. Lusimba Midaba.
Naambiwa list ni ndefu sana hivyo kwa yeyote mwenye jipya atumuvuzishie - Zuri au Baya.

Msamiati: Mavuzi - Mboga ya Kabichi, Hunde - akina dada wale wanaofanana na baba zao, walikuwa wanagombaniwa sana pale ka mpira wa
kona, Mchanifu - Msanii, Anasa - Maandazi ya mke wa Mwl. Omari [alikuwa Kocha pia] nimewahi kumuona huko Pangani, Mharibifu - msamiati huu ulikuja baada ya mfanyakazi mmoja wa pale shule kuoa mdada ambaye alikuwa hawalingani kiumri hivyo watundu wakaja na usemi huu kuwa ni mharibifu, Killer Kala - Rangi inayoua [Msamiati huu uliletwa na watu wenye msimamo mkali kuhusiana na dada zenu hao kutupeleka kasi hata tuliwahi kama sikukumbuki vizuri tulicheza Bull Dance once na baadae tulifanya partneship na wanafunzi wa Kwilo],
Mbu Jazz Band - Nadhani mwakumbuka wale Mbu pale na Cerebral Malaria [Joining Instructions ilikuwa na phrase tata - Net ni muhimu lakini sio lazima au Net ni lazima lakini sio muhimu, sikumbuki vizuri. Dikodiko - Siku za Jumamosi vijana walikuwa wanakarabati vyakula kwa majiko ya umeme mabwenini, kwa kuchanga na kununua kuku IDM almradi Chakula siku ile kilikuwa kinaleta raha esp. Mirambo Village.

Nisiyoyasahau:
1. Dispensary haikuwa na dawa na mganga naye alikuwa na mambo mengi, kama kawaida wanafunzi tulikuwa na tabia ya kuunga Azimio la Arusha kwenda Mzinga Hospital tena kwa kutoroka siku ya Jumamosi bahati mbaya kufika Hospitali badala ya kupata huduma na kurudi shule Daktari aligoma kabisa kuniruhusu kwakuwa hali haikuwa nzuri, Kimbembe kilikuwa kwa mwenzangu ambaye ndie alinisindikiza atawaambia vipi utawala wa shule, kuna mwanafunzi amelazwa?!.

2. Baada ya pitapita ya Promosheni ya Waalimu pale shule, nadhani baada ya Bagenda kuondoka. Mwl. Chimile (RIP) alipata U-Second Master, sasa wakati ule tayari tulikuwa tunakaribia sana kufanya mithihani, kila mtu alikuwa na excuse zake kutokwenda Assembly mie nikiwa mmoja wao, Si mwakumbuka net zilikuwa lazima zitundikwe juu. Kuna jamaa ule mtego wa Mbu ulishapoteza dira, ilikuwa nyeupe lakini hakuwa akiitendea haki ilibadilika ikawa ndio chaka la wakwepa Assembly ukiireremsha hakuna aliekuwa akikuona basi hilo ndilo lilikuwa chaka langu mpaka muda wa kuingia darasani. Nadhani Mwl. Chimile (RIP) alikuwa anafuatilia kwa karibu sana kwani siku ile nilikamatwa kama Saddam pale pangoni. Nilikuwa bize naendelea kupata shule nadhani alikaa kama dk. 5 mimi nilikuwa simuoni. Alifunua Net akasema nenda Assembly nikapiga Magoti mpaka muda wa Assembly umeisha, Nikaingia Darasani that was it hakuwahi kuniuliza wala kupata Adhabu zaidi ya ile ambayo ilikuwa hardly 10 Minutes.

3. Mnakumbuka enzi za Disco kule Kilei na hata Mzumbe kulikuwa na Madaraja ukumbini from First Class mpaka Third Class huko watu ni muziki kwa kwenda mbele yaani washika mchuma [un-mademu] na mademu kutudanganya majina wengine walikuwa wanapewa majina ya mabasi. Walahi ufisadi ulianza zamani, na visiting day watu wanapeleka mikate na siku hiyo unapiga mswaki sana, nywele unapiga cut iliyokwenda shule si mnawakumbuka vinyozi maarufu. Pale Morogoro kulikuwa na jamaa alikuwa anawatia watu joto kuhusu watoto wa killer Colour - Alex Mikate, Mnamkumbuka.

4. Je, Siku za kazi shambani na Club's day na Prep ya mchana baada ya mlo, Si waalimu wakali walikuwa wanapita kuangalia wanaopiga stori na kulala mchana. Hivyo solution ilikuwa kupanda na kujificha juu ya dari. Kuna jamaa aliteremka nalo, jina silikumbuki vizuri ndio ukawa mchezo huo umepungua.

5. Kuiba machungwa ya shule na kuficha kwenye Ma-locker au viazi na kuchemsha kwa Heater Mwitu [Spring za Vitanda]

6. Uzamiaji wa msosi Mzumbe, Unaoga na kuvaa koti pamoja na kijiko. Kwanini Koti?, Lilikuwa linajenga personality. Ole wako ushtukiwe na
walinzi watakufukuza kama mwizi na kijiko chako mkononi. Tabia hii ilipungua watu wakawa wanakula kwa Ma-poti wao [Home boy] mabwenini pale chuoni.

7. Vita vya kujikomboa kutoka kuvaa Kaptura za kaki hadi kuvaa Suruali nyeusi.

8. Mgomo baridi wa chakula ambacho hakikuwa kizuri especially madondo lakini jamaa zetu wengine wakatusaliti walizidiwa na njaa ikabidi wale tu, nadhani mnawakumbuka.

9. Michezo na vijana wa mazimbu - wapigania uhuru.

10. Siku ambayo vijana walikula doria usiku mzima baada ya kutembelewa na Kina dada wa Msalato Girls. Mnaikumbuka hiyo?. Walilala Mirambo Village Dorm. #4 or #3. Ikaleta manungu'niko kwa dada zetu wa Kilakala.

11. Siku ya Nyali na Nyama au siku ya ugali na kabichi - {Siku ya kabichi ilikuwa siku ngumu sana na haswa kama huna jinsi ya kukarakachua miundo mbinu ili upate mbadala]

12. Siku ya Jumamosi ilikuwa ni kama siku ambayo unajikomboa, kwani baada ya shughuli ya usafi na ukaguzi na matangazo ya hapa na pale,
unakuwa huru ukisubiri misosi ya mitaani au unaenda kubadilisha mkaango mjini au pale mwanzo wa lami ya kupaka kuja chuoni IDM ukila miwa. Jioni unawahi Roll Call halafu wasubiria wali tena ukivuta hisia ya Kideo cha Mwl. Myenge. Wengine watafuata Uzo "gongo" Changalawe. Watu wa dini watakuwa wakisali na kuimba. Almradi Jmosi ilikuwa inasaidia sana kutoa msongo.

Na zile trip za Tangeni zilisaidia sana kuamsha ari ya kufanya kazi kwa bidii, usafi bila viboko.

Ya kukumbuka ni mengi sana i hope wengine watasaidia kuleta raha ya zamani.

Natarajia kusikia mengi kutoka pembe mbalimbazi za dunia hii.

Naomba kuwasilisha.

NB: HuXiang umenena itakuwa ni kitu cha maana kuwa na wavuti dedicated kwa Wazumbe [Alumni].
 
hivi ule utaratibu wa kula maharage kila siku bado unaendelea mzumbe au?????maana sie kule ilburu tulikuwa twapata na mbonga za majani,teh teh teh

Utaratibu huo upo ila siku hizi ni kila siku NYALI(WALI) na ugali ni mchana tu,vijana siku hizi wanakula mikate na Pilau mara mbili kwa mwezi.
 
Kaka wewe umetaja list ya siku nyingi sana hii!!!!
ila kwa miaka ya 2000,sisi tunaweza wakumbuka
Peter Nalitolela,Sunday Dominic,Lusekelo kibona,Rogers Bhalalusesa,Nyantamba,Ungu Ramadhani,Wahab Mohamed.Emil Patrick,Spencer Sanjawa,William Maro,Baraka Daudi,Stephen Kazi,Hamad Juma,Simon Monko,Mathias Monko,Mkata Nyoni,Paschal Magesa,Emmanuel Kimbe,John Sichilima,Alex Kapungu,Wilhad Bilalo,Fredrick Lymo,Moses Kwabi.
ukija kwa Olevel walikuwa vijana balaa pale akina Erick Kabuka,Mathias Monko,Masudi Kisamfu,Stanley Kafu,Latif Amars,Rizik Lameck,Juma Mbega,Frank Andrew Mwakyembe,Idd Davis,David Mwasota,Lusungu wangilisasi,Patrick Sungura,Mafuru Kulwijira na wengine wengi sana miaka ya 2000 hiyo.
walimu wengi walihama shule na kupata Kuwa ma-Head Master shule zingine ila Minja hadi leo yupo.

Umenikumbusha hiyo list ndo ya vijana ambao mimi nawajua enzi za Mzumbe.
 
Wibonele a.k.a Mkombhoti (RIP) alifia Atlanta mwaka 2006.....story zinadai alikuwa na kansa! Maelezo zaidi ni marefu mno, lakini kama una muda piga simu Uzumbeni uongee na Mwl Minja..yeye atakupa story zaidi.

Unamkumbuka Sapila, Fine Art (checkbob na moka zake), Mwl. Amasi, Mwl. Muyenge na mkewe, Mwl Shayo, Mwl. Miyimba wa Agriculture na yule jamaa wa Agroeconomics, Mwl Majumbwa, Mwl. Mpemba na mkewe......

Kideo cha Muyenge kila jumamosi pale dining, form one wanaitwa nguruwe na mambo ya ndabuli (zile bakuli za bati za Tanzania Goverment "TG"). Majina ya kuchekesha kama Mchele Mahela, Machai Namasamaki, Kagari Kamutuka e.t.c......Picnic za Tangeni baada ya ushindi wa usafi na "anasa" za mama Kuboja!! LOL...

Ma-homeboy wanavyogombania kuwa "ma-odali"/"injaji" kule kitchen!! Ugali kwa nguruka (wale samaki wenye chumvi kichizi toka pale gengeni ukipita posta)!! Msee kama mambo safi "menu" kwa Mkombhoti (rip) na baada ya hapo kama mvutaji anakuuzia fegi ya kushushia......

Minja bado yupo.
Sapila,Mtawajibu,Malale,Mtesigwa wamepata Kuwa Head Master kwenye shule za Kata.
Matekele yuko Mzumbe University anapigisha vijana elimu.
 
Back
Top Bottom